Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SPOTI DIKTA: Pep Guardiola kujijeruhi usoni iko hivi

Dokta Pict
Dokta Pict

Muktasari:

  • Ikumbukwe pia klabu hizo zote katika misimu yao mitatu wamekuwa na mafanikio makubwa ikiwamo kuwa mabingwa wa ligi zao mara tatu mfululizo.

KABLA ya kufikia mwanzoni mwa wiki hii klabu ya Manchester City ya nchini England ilikuwa na hali ya kimfanano na klabu ya hapa nchini Yanga kwa timu hizo kupata matokeo mabaya mfululizo katika mechi zao za siku za karibuni.

Ikumbukwe pia klabu hizo zote katika misimu yao mitatu wamekuwa na mafanikio makubwa ikiwamo kuwa mabingwa wa ligi zao mara tatu mfululizo.

Lakini mwanzoni mwa wiki hii hali ilikuwa tofauti, Yanga ilipata ushindi wakati Man City ilifungwa mabao 2-0 na Liverpool hivyo kuendelea na matokeo mabaya katika mechi saba mfululizo, ambazo imepoteza sita na sare moja.

Lakini jambo moja ambalo wengi waliliona mitandaoni ni picha iliyopigwa wiki iliyopita ikimuonyesha kocha wa Man City, Pep Guardiola akiwa na kijijeraha cha mkato puani.

Vile vile alikuwa na alama za mikwazuro ya kucha za vidole pamoja na michubuko ya juu juu eneo la kichwani katika uso na upara wake.

Majeraha hayo aliyapata katika mechi ya wiki iliyopita katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) waliotoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya timu ya Fayenoord ya nchini Uturuki.

Masahibu hayo yaliwakuta na kuwa timu ya kwanza katika historia ya Ligi ya Mabingwa kushindwa kushinda mchezo baada ya kuongoza kwa mabao matatu au zaidi katika dakika ya 75.

Matokeo haya yalimkasirisha sana Pep hasa kutokana na timu yake ilikuwa ikiongoza mabao 3-0, lakini hapo baadaye mambo yalibadilika na mabao hayo kukombolewa likiwamo lile la dakika ya 89.

Hali hiyo ilimpa hasira sana, kocha huyu ambaye anapokuwa hali hiyo ni kawaida kujisugua sugua kichwani kama ishara ya kukasira na huku akiwaza nini cha kufanya.

Lakini katika siku hiyo hali ilikuwa tofauti kwani wakati anahojiwa na wanahabari mara baada ya mchezo huo alionekana akiwa na alama za mikwruzo ya makucha katika uso na huku kukiwa na kimchaniko katika kichuguu cha pua.

DK01
DK01

Kijidonda hikcho pia kiliendelea kuonekana katika mchezo wa EPL  uliochezwa siku ya jJumapili dhidi ya Liverpool katika dimba la Anfield ambako walifungwa tena 2-0 hivyo kushindwa kurejea katika nafasi ya 2 katika msimamo wa EPL.

Katika mechi aliyojijeruhi Pep alionekana kuchanganyikiwa tangu bao la kwanza lilipoingia. Meneja huyo alikuwa ameweka mikono yake kichwani nusura ajikune kwa kutoamini kilichotokea.

Mikwaruzo na michubuko ilionekana baadaye kichwani mwake wakati wa mahojiano na media baada ya mechi kumaliza.

Alisema kuwa, Man City tumepoteza mechi tano mfululizo na hii inaweza kuwa mechi ya kukatisha tamaa zaidi, kwa kiasi fulani hatukuwa bora alielezea jinsi ilivyotokea.

Akaongeza zaidi “Kidole changu hapa” alionyesha kijeraha cha puani na kucha ya kidole. Guardiola alisema, kisha akaongeza tena kwa mzaha, “Nataka kujidhuru”. “Usiku mwema.” Alisema huku akiondoka katika eneo la mahojiano na wanahabri.


Hali ya hasira iko hivi

Jicho la kitabibu la ‘Mwanaspoti Dokta’ linalitazama tukio hilo la Pep kujikwaruza kama ni tatizo la kiakili na kitabia. Ni ishara ya kuwa alikuwa ameumizwa kihisia, yuko katika hali ya huzuni na hasira kali.

Lakini pia matokeo ya kufungwa mfululizo yanamtia zaidi simanzi kwani ni hivi karibuni tu ametoka kusainishwa mkataba mpya. Kwa hali kama hayo ni vigumu kukosekana hali ya shinikizo la akili.

Kupata matokeo kama hayo, ni hali ambayo hajaipata kwa muda mrefu, yeye hana uzoefu wa kufungwa fungwa. Ni uzoefu mpya kwake ambapo mwili unapopata hali hiyo unaweza kunyumbulika na hatimaye kujibadili kuweza kuendana na hali ya huzuni na hasira kali.

Na ndio maana hata katika mechi ya Jumapili dhidi ya Liverpool pamoja na kufungwa tena lakini hakujikwaruza na kujijeruhi. Hii ni dhahiri mwili umenyumbalika na kubadilika na kuzoea hali ya kuumizwa kihisia.

Hasira na kughadhibika kirahisi na kufanya matendo yasiyo ya kawaida katika soka huwa ni kawaida kawapata makocha kiasi cha kuwachanganya kiakili.

DK02
DK02

Hata aliyewahi kuwa kocha Manchester United, Sir Alex Furgerson aliwahi kubutua kiatu kwa hasira katika vyumba vya kubadili nguo. Kiatu kilipaa na kumpiga David Beckham usoni.

Kitabibu hasira hutokea na huwa ni sehemu ya mwili kujihami dhidi ya tishio kutoka nje ya mwili. Mwili unapopata mapokeo ubongo hutafsiri na kuamrisha kuzalishwa kwa kichochezi cha Adrenaline ambacho huambatana na hasira.

Uwepo wa hali hiyo ndipo huzaa hasira ambapo ni hisia hasi ambazo zinaweza kuleta mabadiliko katika mwili ikiwamo kufanya matukio kwa nguvu kama kupiga au kutukana au kujidhuru pasipokujua.

Kama alivyojikwaruza na kujijeruhi, kisaikolojia imempa hali ya unafuu, ni kama vile kuna kitu kizito akili mwake amekipeperusha.

Wakati wa kushtuka na kupata hasara ikiambatana na uwepo wa kichochezi cha Adrenaline inaweza kumsaidia mtu kujihami na hatari ikiwa mwili kuwa na nguvu isivyo kawaida.

Hali hii ndio inausaidia mwili wa mwanadamu kuweza kuokoka katika majanga au hatari mbalimbali. Lakini kwa upande wa Pep yeye alitumia hali hiyo kujikwaruza na hatimaye kujidhuru.

Lakini ukiwa katika maeneo ya uwanjani kupanda kwa hasira na kushindwa kudhibiti kunaweza kusababisha kufanya matukio pasipo kufikiri ikiwamo kujikwarua au kujipiga au kujidondosha na kutua na magoti.

Hasira isipodhibitiwa inakuwa ni hasara kwa mwili kwani inaweza kumfanya mtu kushindwa kujidhibiti au kushindwa kuwa na uamuzi mzuri kama ilivyokuwa kwa Pep.

Ingawa hali hiyo haijawa tishio sana, lakini kama hali hiyo itaendelea, Pep anahitaji tiba ya akili kutoka kwa wanasaikolojia na madaktari wa afya ya akili.