Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Samatta katika njia ya Ronaldo

Muktasari:

  • Lakini mazingira yalivyokuwa, ilimlazimu kukubali uamuzi mgumu na kuhamia Al-Nassr ya Saudi Arabia.

WAKATI mwingine maisha hulazimisha kufanya maamuzi magumu, hata kama moyo hautaki. Miaka miwili nyuma, mshindi mara tano wa Ballon d’Or, Cristiano Ronaldo, alilazimika kuondoka Manchester United, licha ya kuwa aliamini angekuwa msaada mkubwa kwa mashetani wekundu wa Old Trafford.

Lakini mazingira yalivyokuwa, ilimlazimu kukubali uamuzi mgumu na kuhamia Al-Nassr ya Saudi Arabia.

Leo, tunamshuhudia Mbwana Samatta, nahodha wa Taifa Stars, akiwa katika hali ya kufanana na ile aliyokuwa nayo Ronaldo kipindi cha nyuma.

Samatta ambaye kwa muda mrefu alikuwa na hadhi ya mchezaji muhimu kwenye timu kubwa barani Ulaya, sasa anacheza soka la kulipwa Ugiriki akiwa na PAOK.

Hata hivyo, mazingira yake katika timu hiyo ya Ugiriki hayana tofauti na aliyokuwa nayo Ronaldo huko Manchester United, anashindwa kupata namba ya kudumu kikosi cha kwanza.

Kila mwaka, Samatta amekuwa akifanya mabadiliko katika maisha yake ya soka, akiwa mchezaji wa kwanza wa Tanzania kucheza katika michuano mikubwa ya Ulaya, kama vile Ligi ya Mabingwa, Europa League na Europa Conference League. Alipiga hatua kubwa alipojiunga na Aston Villa, akifanya historia kama mchezaji wa kwanza wa Tanzania kucheza Ligi Kuu England. Alicheza pia fainali ya Kombe la Ligi ya England huko Wembley mwaka 2020, akifunga bao dhidi ya Manchester City, klabu ambayo iliongozwa na Pep Guardiola.


MUDA WA MAAMUZI

Kushindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha PAOK, timu aliyosajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili kutoka Fenerbahce na mkataba huo unamalizika mwaka 2025.

Hii ni hali ambayo haikuwa inatarajiwa kwa mchezaji ambaye msimu uliopita, alitwaa ubingwa wa Ligi Kuu Ugiriki.

Katika msimu huu, Samatta amekosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza na amecheza mechi tano tu katika mashindano yote. Hii ni ishara tosha kocha wa sasa wa PAOK, Răzvan Lucescu, anaonekana kutomhusisha sana na mipango ya timu. Hali hii inamfanya Samatta kuwa kwenye njia ile ile aliyopita Ronaldo, anahitaji kufanya maamuzi magumu ili kuhakikisha anabaki kwenye soka la ushindani.


NINI KINAHITAJIKA

Samatta ni mchezaji ambaye ameshacheza mashindano makubwa na ameweka rekodi nyingi kwa Tanzania. Amecheza katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, Europa League na Europa Conference League.

Hata hivyo, akiwa na umri wa miaka 31, Samatta anakutana na changamoto mpya. Je, bado anaweza kufanya vizuri kwenye soka la ushindani barani Ulaya? Jibu ni wazi. Ndiyo. Samatta bado ana uwezo mkubwa wa kucheza katika ligi kubwa za Ulaya, lakini kwa sasa huenda akaona ni bora kutafuta changamoto mpya katika nchi ambazo ushindani wake ni mdogo, huku akijua kuwa umri wake unakwenda kasi.


MWENZAKE ALICHOFANYA

Ronaldo alijua kuwa ili kuendelea kucheza kwenye kiwango cha juu, alilazimika kuchukua hatua kubwa. Aliondoka Manchester United na alikwenda Al-Nassr, na kama ilivyo kwa Ronaldo, Samatta anahitaji kuchukua maamuzi magumu.

Samatta anaweza kuona kuwa hatua ya kwenda Saudia inaweza kumfaa, kama ilivyokuwa kwa Ronaldo, ambaye licha ya kuwa na umri mkubwa, alifunga mabao mengi na kuwa mfungaji bora wa Ligi ya Saudia msimu uliopita akiwa na Al-Nassr.

Kama Ronaldo alivyokuwa na ujasiri wa kuhamia Saudia na kufanya vizuri, Samatta pia anafaa kujiuliza, “Ni lini nitafanya uamuzi kama huu?”

Ingawa soka la Ulaya linaweza kuwa na ushindani mkubwa, soka la mashariki ya kati linatoa fursa kubwa kwa wachezaji wa kigeni, huku likiwa na mkwanja wa kutosha.


WASIKIE WADAU

Nyota wa zamani wa Yanga, Credo Mwaipopo, ambaye kwa sasa anaishi Sweden, alielezea matumaini yake kwa Samatta, bado ana uwezo mkubwa wa kuendelea kucheza soka la ushindani kwa miaka mitatu hadi minne mbele.

“Samatta ana uwezo wa kucheza kwa miaka mingine minne, lakini atahitaji kufanya maamuzi magumu. Anaweza kufanikiwa zaidi kama akiamua kuondoka PAOK. Zaidi ya yote, anahitaji kuwa na timu itakayomwonyesha imani,” anasema Mwaipopo.

Kwa upande mwingine, Haji Mnoga, ambaye kwa sasa anacheza Salford City ya League Two nchini Uingereza, alizungumza kuhusu hali ya Samatta, akisisitiza ni wakati wa mchezaji huyo kufanya maamuzi makubwa kuhusu mustakabali wake.

“Kama Samatta anataka kuendelea kufanya vizuri, lazima atafute timu itakayompa nafasi ya kuonyesha uwezo wake. Umri si kikwazo kwa mchezaji kama yeye, lakini lazima apige hatua mbele,” anasema Mnoga.