Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Yanga atua Ismaily ya Misri

Muktasari:

  • Hamdi alijiunga na Yanga katikati ya msimu ulippita  akitokea Singida Black Stars akichukua mikoba ya Sead Ramovic na kuiongoza timu hiyo kwenye mechi 12 za ligi.


BAADA ya kuipa Yanga mataji matatu aliyekuwa kocha wa Yanga, Miloud Hamdi atambulishwa katika klabu ya Ismaily ya Misri kwa mkataba wa mwaka mmoja.


Hamdi alijiunga na Yanga katikati ya msimu ulippita  akitokea Singida Black Stars akichukua mikoba ya Sead Ramovic na kuiongoza timu hiyo kwenye mechi 12 za ligi.


Kocha huyo anajiunga na Ismaily na makocha wawili wasaidizi Hammadi Saghier ambaye ni kocha msaidizi raia wa Ubelgiji na Marouane Silimani, kocha wa viungo  kutoka Tunisia.

Hamdi msimu huu akiwa Yanga amebeba makombe matatu ikiwa ni Kombe la Muungano,  Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho (FA).

Chanzo cha kuaminika kutoka kwa meneja wa kocha huyo ambaye hakutaka jina lake liwekwe wazi kimeliambia Mwanaspoti kuwa Ismaily imepanga kumlipa Hamdi mshahara mara mbili zaidi ya ule anaoupata Yanga.

“Ni kweli Hamdi anaenda kuifundisha Ismaily SC”