Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu za hasira, vurugu katika dabi

Wachezaji wa Atletico Madrid na Real Madrid wakizozana katika mchezo wa Dabi ya Madrid iliyopigwa wiki iliyopita

Muktasari:

  • Dabi ya Kariakoo hubeba hisia mbalimbali kwa mashabiki kabla na baada ya mchezo huo, hata kama matokeo ya mchezo yanakuwa sare au suluhu.

SIKU zijazo mashabiki wa soka nchini watakuwa katika Uwanja wa Mkapa kushuhudia mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga inayotarajiwa kupigwa Oktoba 19.

Dabi ya Kariakoo hubeba hisia mbalimbali kwa mashabiki kabla na baada ya mchezo huo, hata kama matokeo ya mchezo yanakuwa sare au suluhu.

Lakini wakati unaposikiliziadabi hiyo ifike, siku sita zilizopita barani Afrika kulikuwa na mechi kali ya kuwania Super Cup iliyopigwa Septemba 27 kati ya mahasimu wa Misri, Zamalek na Al Ahly zinazoshikilia mataji ya Afrika.

Al Ahly ni mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika na Zamalek wababe wa Kombe la Shirikisho kwa msimu uliopita na ndizo zilizokuwa lazima zikutane kwa mujibu wa kanuni za mashindano na mechi ilikwenda kupigwa Riyadh, Saudi Arabia ikiwa ni kwa mwaka wa pili.

Mchezo huo ambao ni moja ya dabi kali ya watani soka wa Misri ilishuhudiwa Zamalek ikitwaa ubingwa kwa ushindi wa penalti 4-3 baada ya kufungana bao 1-1 katika dakika za kawaida.

Mchezaji wa Zamalek (aliyesimama) na wa Aly Ahly katika mchezo wa Super Cup uliopigwa Saudi Arabia, hivi karibuni.

Kukutana kwa timu hizo zenye upinzani wa jadi kama inavyojulikana kuwa dabi huwa ni kawaida kuwepo matukio yenye kubeba hisia na kwa mashabiki na wachezaji.

Dakika za mapema tu wachezaji wa Zamalek walimzunguka refa kwa hasira wakimkaripia kuwa ametoa penalti isiyo halali na waliamua kutoka uwanjani kwa hasira na kususa kutokana na kutokubaliana na uamuzi wake.

Busara na ushawishi vilitumika kuwarudisha uwanjani na kuendelea na mchezo ambao baadaye ndio walikuja kukomboa na hatimaye kuja kushinda katika penalti.

Ukiacha mchezo huo wa Dabi ya Mafarao, kule Hispania katika Ligi Kuu (La Liga) Jumapili iliyopita kulikuwa na Dabi ya Madrid kati ya Atletico Madrid na Real Madrid.

Katika mchezo huo uliopigwa nyumbani kwa Atletico Madrid dakika ya 64 Real Madrid ilipata bao la kuongoza kupitia beki wa kati Mbrazili Eder Militao. 

Kwa dakika chache mchezo ulisimama kutokana na mashabiki kumshambulia kipa wa Real Madrid, Thibaut Courtois kwa kutupa vitu kadhaa kikiwamo chenye ncha kilichomgonga. Hasira hizo za mashabiki zilitokana na kitendo cha kipa huyo kushabikia bao hilo kwa mashabiki mahasimu wa Atletico Madrid ambao walijibu mapigo kwa mtindo usio sahihi.

Hali hiyo ilikuwa ni hatari kwa afya ya kipa huyo pamoja na wachezaji wengine kwani vitu vyenye ncha kali vinaweza kuwasababishia majeraha mbalimbali mwilini.

Tukio hilo lilimlazimisha refa kusimamisha mchezo na wachezaji wote kwenda katika vyumba vya kubadilishia nguo ili kulinda usalama wao.

Ilichukua takribani dakika 15 hali hiyo kutulia na huku jitihada za makocha, viongozi na wachezaji wa Atletico kuwasihi mashabiki watulie ili mchezo uendelee.

Hali ilitulia na mchezo ukaendelea, lakini kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone ambaye huwa hatulii katika mechi zake alikuwa akiwapa ishara mashabiki kushangilia zaidi ili kuwapa hamasa wachezaji wao wafunge mabao.

Utulivu huo baadaye ulizaa matunda na kufanikiwa kukomboa bao walilokuwa wametangulia kufungwa ambalo walifunga dakika za mwisho za majeruhi 90 +5 hivyo mchezo huo kwisha kwa kufungana bao 1-1.

Kama ilivyo kwa wachezaji wa Atletico ni aina ya mastaa ambao wako kama kocha wao. Huwa ni wakali kitabia na kimchezo. Hali hiy ni kawaida kupata kadi nyekundu.

Dakika za mwishoni ilishuhudiwa mchezaji Marcos Llorente akipewa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya Fran Garcia dakika ya 90 +9 Mara kadhaa refa alikuwa akilazimika kutoa kadi za njano kuwaonya wachezaji wapande zote kwa kuwa mara kadhaa walikuwa wakikwaruzana na kurushiana maneno.

Haya matukio yalikuwa yakifafana sawa na yale ya Dabi ya Mafarao katika mchezo wa Super Cup ambapo nao kadi za njano zilitembea kwa wachezaji.

SABABU YA MATUKIO HAYA
Hasira na kughadhabika kirahisi na kufanya matendo yasiyo ya kawaida katika dabi huwa ni kawaida katika mechi kutokana na kubeba hisia kali kwa wachezaji na mashabiki. 

Mtu anapopenda kitu chake kinakuwa ndani ya mwili. Hisia hubeba mapenzi mazito ya kitu. Katika hisia hizo huwa kuna kulipuka kirahisi pale mtu anapochokozwa na kuudhika.

Kitabibu binadamu hasira hutokea na huwa ni sehemu ya mwili kujihami dhidi ya tishio toka nje ya mwili.

Mwili unapopata mapokeo ya ubongo hutafsiri na kuamrisha kuzalishwa kwa kichochezi cha Adrenaline ambacho huambatana na hasira.

Uwepo wa hali hiyo ndiyo huzaa hasira ambapo ni hisia hasi ambazo zinaweza kuleta mabadiliko katika mwili ikiwamo kufanya matukio kwa nguvu kama kupiga au kutukana.

Wakati wa kushtuka na kupata hasira ikiambatana na uwepo wa kichochezi cha Adrenaline inaweza kumsaidia mtu kujihami na hatari kwa kuwa na nguvu zisivyo za kawaida. Hali hiyo ndiyo inausaidia mwili wa binadamu kuweza kuokoka katika majanga au hatari mbalimbali.

Kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone akimtuliza kipa wa Real Madrid, Thibaut Courtois baada ya kurushiwa kitu chenye ncha kali na mashabiki waliodaiwa kuwa wa Atletico Madrid katika mchezo baina ya timu hizo.

Lakini, ukiwa katika maeneo ya uwanja mathalan katika mchezo kupandwa kwa hasira na kushindwa kudhibiti hatimaye mambo hufanya matukio pasipo kufikiri ikiwamo kama ile ya kurusha vitu uwanjani au kutoka nje na kususa.

Jumatano iliyopoita, Atletico ilitangaza kumfungia maisha shabiki aliyekamatwa kumrushia Courtous kitu chenye ncha. Lakini mashabiki nao wakataka mchezaji huyo adhibiwe kwa uchokozi.

Hasira isipodhibitiwa inakuwa ni hasara kwa mwili kwani inaweza kuusukuma kufanya kitu cha kudhuru wengine ikiwamo kupiga na kujeruhi.

MBINU ZA KUTULIZA
Zipo mbinu kadhaa za kutuliza hasira ikiwamo mathalan katika mchezo huo wachezaji wote walitolewa uwanjani ili wale mashabiki walioudhika wapoe. Miongozo ya Fifa ndiyo inaelekeza kuwaondoa wachezaji panapokuwa na viashiria vya fujo.

Watu wenye ushawishi kuwatuliza, kocha wa Atletico, Simeone alifanya kazi ya zaidi kuwatuliza mashabiki ambao baadhi walivaa mask kuficha sura zao.

Vilevile viongozi na kocha wa Real Madrid nao walionekana kushawishi hali hiyo itulie ili mchezo uendelee.

Mmoja wa wachezaji wenye ushawishi na kupendwa na kuheshimiwa na mashabiki alivuka kwa walinzi wa uwanjani na kwenda karibu kwa mashabiki na kuwaomba watulie ili mchezo uendelee. 

Wakati wachezaji wa Zamalek walipomzonga mwamuzi, wakasusa na kutoka nje ya uwanja ushawishi wa baadhi ya wachezaji na viongozi ndivyo vilisaidia kuwatuliza na  hatimaye walirudi na kutuliza akili ambapo walishinda mechi.

CHUKUA HII
Hasira isipodhibitiwa ikipitiliza inaweza kusababisha mwathirika kupatwa na mshtuko na kuanguka. Mpira unabeba hisia kali ila ni muhimu kudhibiti hasira ili usifanye mambo yasiyofaa.