Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ronaldo anafanya hivi mapumzikoni akijiuguza

DOKTA Pict

Muktasari:

  • Ndani ya Uwanja wa Alianz wakiwa nyuma kwa mabao 2-1 alifunga bao la kusawazisha dakika ya 61 kwa kuunganisha vyema krosi ya Nuno Mendes ambaye ni beki wa kushoto na nyota wa mchezo huo.

USIKU wa Jumapili, Cristiano Ronaldo ‘CR7’ aliiongoza Ureno kunyanyua taji la Ligi ya Mataifa Ulaya 2025 baada ya kuifunga Hispania kwa mikwaju ya penalti 5-4 jijini Munich, Ujerumani.

Ndani ya Uwanja wa Alianz wakiwa nyuma kwa mabao 2-1 alifunga bao la kusawazisha dakika ya 61 kwa kuunganisha vyema krosi ya Nuno Mendes ambaye ni beki wa kushoto na nyota wa mchezo huo.

Bahati mbaya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 40 anayekipiga Al Nassar ya Saudi Arabia dakika ya 87 alipata majeraha pasipo kufanyiwa faulo, kwani ghafla akiwa katikati ya uwanja alishika mapaja na kukaa chini. Alilazimika kutolewa kutokana na kupata maumivu makali ya misuli ya nyuma ya paja na nafasi yake ilichukuliwa na Gonçalo Ramos.

DOKT 01

Ingawa mpaka sasa haijawekwa wazi kwa kina ameumia kwa kiasi gani, kitendo cha kutoka na kutembea akichechemea ni dhahiri kuwa majeraha ni ya kuchanika misuli kwa wastani.


SABABU ZA MAJERAHA HAYO

Umri wa miaka 40 pamoja na kutumika sana mara kwa mara ni moja ya kihatarishi cha kupata majeraha hayo yanayojulikana kama hamstring muscle injury. Sababu kubwa ni misuli hiyo ya nyuma ya paja ndio inayofanya kazi sana wakati wa kucheza na huku pia nguvu nyingi zikitumika kukunjua na kuituliza misuli.

Misuli hiyo ndio inamfanya mchezaji kupiga mashuti, kukimbia kwa kasi, kuruka au kunyoosha mguu. Hii ndio sababu aina hii ndio inaongoza kuwapata wanasoka wengi duniani. Mkali huyo wa mabao akiwa anacheza mechi yake ya 221 ameweka rekodi ya kufunga mabao 138, ilisemekana hakuwa katika utimamu wake tangu wakati anajiunga na timu hiyo.

Kucheza mashindano hayo au mechi ngumu kama ile huku akiwa hujapona asilimia 100 ni moja ya sababu ya kupata majeraha ya misuli.

Ronaldo alisema alifika fainali hiyo akiwa na jeraha, lakini alipambana na uchungu, na kufunga bao muhimu hatimaye ikalazimika muda wa ziada na baadaye penati. Wakati anafunga bao hilo dakika ya 61 alionekana mguu wake ulinyooka kuzidi kiwango cha kawaida na kufanikiwa kuunganisha krosi hiyo ingawa mguu ulikita chini kwa nguvu na kuelemewa na uzito wa mwili, hali iliyochangia kujijeruhi.

Ingawa majeraha aliyokuwa nayo awali yalipona, lakini aliweza kuwa na ustahimilivu huku akicheza kwa tahadhari.

DOKT 02

Kuitwa timu ya taifa kulitokana na ukweli kuwa uwepo wake ni mbinu ya kisaikolojia kuwatisha wapinzani, lakini pia kuongeza hamasa na ari ya ushindi katika timu.

Hata katika mchezo huo alionekana akicheza zaidi eneo la ushambuliaji zaidi kuliko kutokea pembeni. Hii ilikuwa ni mbinu sahihi kwa umri na historia ya majeraha yake na kutumika sana katika ngazi ya klabu.


VITU ANAVYOFANYA MAPUMZIKONI

Ronaldo sasa amepumzika muda mwingi ili kuuguza majeraha na kupona kwa wakati. Baada ya majira ya kiangazi, haijaeleweka endapo atashiriki Kombe la Dunia la Klabu la Fifa. Anahusishwa na timu kadhaa zinazoshiriki shindano hilo, na huku pia anahitaji kufanya uamuzi kuhusu mkataba wake unaoisha katika timu ya Al-Nassr ya Saudi Pro League.

Vilevile anauguza jeraha la misuli akiwa mapumzikoni, huku maendeleo yake yakisubiriwa kwa hamu na klabu mbalimbali.

Katika kuta zake za mitandao ya kijamii kuna video inayomuonyesha akiwa katika mji wenye baridi kali na theluji, na katika nyumba aliyofikia anaonekana akitumbukia katika kibwawa chenye maji ya baridi ambayo yako chini ya nyuzijoto-1.

Pembeni yake anaonekana kuwapo mwalimu wa viungo aliyekuwa akimpa maelekezo ya kutumbukia na kuingiza mwili wote katika maji hayo. Hiyo kitabibu ni sahihi kabisa, kutumbukiza mwili katika mabwawa au mapipa ya baridi kali ni moja ya njia zinazotumiwa na wataalamu wa afya ya viungo vya mwili kukabiliana na majeraha.

DOKT 03

Kuuweka mwili katika maji ya baridi kunafifisha maumivu na uvimbe, hivyo kumfanya mhusika kujisikia vizuri.

Ronaldo ni mmoja wa wachezaji ambaye anajali utimamu wake wa mwili ikiwamo kuupigania kuwa fiti asilimia 100. Hutumia mbinu nyingi kujiweka imara, huku wakati wa kujiuguza hufanya huduma binafsi ikiwamo kuoga katika mabwawa na bafu zenye baridi kali, mazoezi ya gym na huduma za sauna.

Anamiliki mashine maalumu ijulikanayo kitabibu kama Pressure Chamber au Barocamera ambayo hutumika kuharakisha uponaji wa majeraha ya mwili ikiwamo misuli. Hufanya kazi kwa kutoa hewa halisi ya oksijeni ambayo mtu aliyepo ndani ya mashine hiyo huweza kuvuta. Hii ni faida kwa seli za mwili kuweza kupata kiwango kikubwa cha oksijeni halisi hatimaye kuharakisha uponaji wa majeraha.

Pia huwa na jopo la wataalamu binafsi maalum kwa usingaji wa mwili ambao kila baada ya mechi au mazoezi magumu hufanya huduma hiyo kati ya saa 2-3. Hii inasaidia uponaji wa haraka wa vijeraha na kuondokana na mkazo wa misuli na uchovu.

Maeneo anayotumika kupumzika na kulala ni yenye mandhari tulivu. Hii inachochea uponaji wa haraka wa majeraha kwani mwili haufanyi mambo yanayoweza kutonesa jeraha. Itakumbukwa kuwa kanuni ya kupumzika huwa ni saa 6-8 kwa usiku mmoja bila usumbufu wowote.

Maeneo ambayo Ronaldo anajiachia ni yale ambayo yanaipa akili na mwili burudisho. Ni muhimu sana mchezaji anapotoka katika majukumu magumu kupata utulivu wa kiakili. Hii inasaidia mwili kupata nafasi ya kujijenga na kujisahihisha. Vilevile husaidia kinga ya mwili kuimarika hivyo kuharakisha uponaji wa jeraha.

DOKT 04

Ronaldo ni mmoja wa mastaa ambao wanajulikana kwa kuhusudu kula minofu ya samaki na mazao ya baharini. Vyakula hivyo ni moja ya lishe bora ambayo ina kiasi kikubwa cha protini. Kitabibu protini ndio inayohitajika kwa ajili ya ujenzi wa mwili ikiwamo misuli. Vilevile misuli haiwezi kufanya kazi ya kukunjuka na kujikunja bila protini.

Pia mwamba huyo hula milo midogomidogo ya katikati ikiwamo matunda na juisi za asili, maji yenye madini na vinywaji vya kimchezo ambapo ndani yake huwa na virutubisho mbalimbali. Hapa unapata picha namna ambayo Ronaldo anavyojiuguza na kutunza utimamu wa mwili akiwa na umri wa miaka 40, lakini bado yuko imara licha ya kupata aina hiyo ya majeraha.


CHUKUA HII

Kanuni kuu ya msingi wa utimamu wa mwili ni mchezaji kufanya mazoezi na mafunzo, kula lishe inayozingatia kanuni za lishe za wanamichezo, kulala, kupumzika na kuburudika. Kanuni hiyo inahitaji nidhamu ya hali ya juu na kuzingatia miiko ya kulinda utimamu kwa kuepuka mienendo na mitindo mibaya ya kimaisha ikiwamo ulaji holela, matumizi ya pombe na tumbaku.