Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

RESPECT: Wabongo waliobeba mikanda ya heshima

Muktasari:

  • Achana na ngumi za ridhaa, ambazo kawaida mabondia wanakuwa wanacheza raundi tatu pekee, kwenye ngumi za kulipwa ni tofauti kwani huanzia mapambano ya raundi nne, sita nane kumi na 12 ambayo wanaume au wanawake huvuja jasho la kutosha kabisa.

NGUMI za kulipwa zimekuwa na heshima ya kipekee nchini licha ya kupitia misukosuko kadhaa. Tafiti nyingi ambazo siyo rasmi zinaonyesha mchezo huu unakamata nafasi ya pili kwa kuwa na wafuatiliaji wengi baada ya soka kutokana na upekee wake.

Achana na ngumi za ridhaa, ambazo kawaida mabondia wanakuwa wanacheza raundi tatu pekee, kwenye ngumi za kulipwa ni tofauti kwani huanzia mapambano ya raundi nne, sita nane kumi na 12 ambayo wanaume au wanawake huvuja jasho la kutosha kabisa.

Hata hivyo, mbali ya sheria hizo, wikiendi iliyopita heshima kubwa imewekwa kwa mabondia nchini waliocheza mapambano ya kimataifa na kuweka rekodi za ushindi.

Abdul Ubaya aliweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kushinda Urusi kwa Knockout ya raundi pili katika pambano la raundi sita dhidi ya Mrusi, Ibragim Estemirov kwenye Mji wa Moscow na Innocent Evarist alishinda Mkanda wa Ubingwa wa Mabara (WBF) dhidi ya Michael Kannler wa Ujerumani pambano lililopigwa Cairo, Misri wikiendi iliyopita.

Pia hapa nchini kulikuwa na mapambano mengine na Morogoro lilikuwepo la ‘Homa ya SGR’ na  Dar es Salaam ‘Chite Ukae’ kwenye Ukumbi wa Manyara Park, Tandale.

Ukiangalia kwa ukubwa bado Tanzania katika mchezo wa ngumi za kulipwa mabondia wake wanashindwa kufikia ukubwa wa kuwania mikanda mikubwa yenye hadhi kama International Boxing Federation ‘IBF’, World Boxing Council ‘WBC’ World Boxing Association ‘WBA’ na World Boxing Organization ‘WBO’.

Hadi sasa Tanzania ina mabondia saba pekee waliowahi kushinda mikanda hiyo mikubwa inayotambulika na kupewa heshima kubwa kimataifa hata hivyo, kuna wanaoishikilia na wengine waliwahi kupokonywa kutokana na kushindwa kutetea.



Fadhili Majiha - WBC Afrika
Bondia namba moja Tanzania katika ‘Pound for Pound’, na bingwa wa mkanda wa Baraza la Ngumi Duniani, kwa ukanda wa Afrika ‘WBC’ Afrika’ Fadhili Majiha ndiye bondia wa kwanza nchini na Afrika kushinda mkanda wa ubingwa huo tangu WBC wauzindue rasmi.

Majiha ambaye kwa sasa ana hadhi ya kumiliki nyota nne katika rekodi yake ya mapambano 51, akiwa ameshinda 33 na 15 kwa Knockout na amepigwa mara 14 kati ya hizo tatu amechapwa kwa Knockout huku manne akitoka sare.

Bondia huyo kwa mara ya kwanza kushinda mkanda wa ubingwa wa WBC Afrika, alimtandika kwa pointi Bongani Mahlangu wa Afrika Kusini, Oktoba mwaka jana kabla ya kuutetea kwa mara ya kwanza dhidi ya Sabelo Ngebiyana wa Afrika Kusini, Julai mwaka huu.

Majiha pia ndiye bondia pekee anayeshikilia rekodi ya kushinda mkanda wa WBA kwa kumchapa Mkenya nchini kwao, Gabriel Ochieng pamoja na kuutetea kwa kumchapa Rofhiwa Nemushungwa wa Afrika Kusini.



Ibrahim Mafia -WBC Afrika
Nahodha wa Mafia Boxing Gym, Ibrahim Mafia ni bondia namba tatu kwa ubora nchini katika ‘pound for pound’, na wa pili kushinda mkanda wa WBC Afrika baada ya kushindwa mara ya kwanza na Sabelo Ngebiyana baada ya pambano lao kumalizika kwa sare.

Mafia ambaye kwa sasa ana hadhi ya nyota tatu na nusu, Oktoba 10 mwaka huu alishinda mkanda wa ubingwa huo baada ya kumtandika kwa Knockout ya raundi ya tisa, Enoch Tetteh wa Ghana.

Rekodi yake imepaa na nakufikisha mapambano  12,  akishinda 11, kati ya hayo nane ni kwa knockout, hajawahi kupigwa huku akipanda hadi nafasi ya 20 kati ya mabondia 1126 wa uzani wa Bantam duniani na nchini akiwa wa pili kati ya mabondia 50 wa uzani wake.



Hassan Mwakinyo - WBO Afrika
Novemba 16, mwaka huu Hassan Mwakinyo atapanda ulingoni kutetea mkanda wake wa ubingwa wa WBO Afrika kwa mara pili jijini Dar es Salaam.

Mwakinyo ndiye bondia pekee ambaye anashirikilia rekodi ya kushinda mkanda wa ubingwa wa WBO Afrika na licha ya umiliki wa mkanda huo, aliwahi kushikilia mkanda wa ubingwa wa mkanda wa Afrika ABU mara kadhaa kabla ya kugoma kutetea na matokeo yake akavuliwa.
Pia aliwahi kushinda mkanda wa ubingwa wa WBA, Botswana ambao hakuwahi kuutetea mahali popote.

Kwa sasa anakamata nafasi ya nne kati ya mabondia bora wa Tanzania akiwa na hadhi ya nyota tatu na nusu. Amecheza jumla ya mapambano 26, ameshinda 23 kati ya hayo, 13 ni kwa Knockout na amepigwa mara tatu, kati ya hizo mbili ni kwa Knockout.

Ni mbondia wa 23 kati ya 1871 duniani kwenye uzani wa middle wakati nchini akiwa wa kwanza kati ya 46 wa uzani huo.


Maono Ally -  WBC Youth
Mwaka 2018, bondia aliweka rekodi ya kuwa bondia wa kwanza Mtanzania kushinda mkanda wa ubingwa kutoka Baraza la ngumi duniani (WBC) lakini alishinda mkanda wa ubingwa wa WBC Youth Afrika Kusini kwa kumtandika kwa Knockout, Luka Pupek kutoka Crotia, lakini alishindwa kuutetea na kuvuliwa.

Amecheza jumla ya mapambano 25, akishinda 15, kati ya hayo 11 ni kwa Knockout na amepoteza tisa, kati ya hayo matano ni kwa Knockout na sare mara moja.
Kwa sasa anakamata nafasi ya tano kati ya mabondia 28 wa uzani wake wa super Walter wakati duniani akiwa wa 492 kati ya 2104.


Saleh Mkalekwa - ABU
Ni mmoja wa mabondia wasiotajwa sana lakini amewahi kushinda mikanda mikubwa yenye heshima kimataifa na aliweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kushinda mkanda wa ubingwa wa umoja wa Afrika ABU, mwaka 2018 kwa kumtwanga Andreas Valavanis wa Misri, pambano lililopigwa Kenya.

Mkalekwa anayepigana Uzani wa walter, amecheza mapambano 30, akishinda 17, kati ya hayo sita ni kwa Knockout, amepigwa mara 13 na kati ya hizo, sita Knockout.
Anakamata nafasi ya 1001 kati ya mabondia 2410 duniani katika uzani wake, huku nchini anakamata nafasi 22 kati ya 54.



Tony Rashid - ABU
Mwaka 2019, aliweka rekodi ya kushinda ubingwa wa ABU uzani wa Super Feather kwa kumchapa kwa Technical Knockout Siboniso Gonya raundi ya 10 katika pambano la raundi 12.

Tony akatetea kwa mara ya kwanza jijini Dar, mwaka 2021 mbele ya Bongani Mahlangu lakini akapoteza kwa Technical Knockout ya raundi 12 kabla ya kurudiana tena na Bongani mwaka 2022 na kurejesha mkanda wake wa ABU kwa ushindi wa pointi.

Mwaka 2023 akaupoteza tena jijini Dar kwa Sabalo Ngebiyana wa Afrika Kusini pambano ambalo matokeo yake yaligubikwa na utata kutokana na ndani ya ulingo, Tony alitangazwa mshindi kabla ya ABU wenyewe kupitia rais wa shirikisho hilo kumtangaza Sabelo siku ya pili yake kama bingwa mpya ABU kutokana na ‘score’ kugundulika kukosewa katika uwekaji wa pointi za Sabelo ambazo alipewa Tony.

Tony ambaye atapanda ulingoni Novemba 16, mwaka huu dhidi ya Steven Bwagasi wa Botswana kwenye Ukumbi wa Warehouse, Masaki amecheza jumla ya mapambano 22, akishinda 16, kati ya hayo 11 ni kwa knockout na amepigwa mara tatu, kati hizo mbili ni kwa Knockout huku akitoka sare mara tatu.



Dullah Mbabe - WBO Pasific Asia
Majina yake halisi akiwa ni Abdallah Pazi. Mwaka 2019 alishinda mkanda wa WBO Pasific Asia nchini China kwa kumchapa kwa Technical Knockout ya raundi pili katika pambano la raundi 10, Zulipikaer Maimaitiali raia China katika uzani wa super middle.

Mbabe licha kushinda ubingwa huo, hajawahi kutetea hadi anavuliwa na rekodi yake hadi sasa inaonyesha amecheza mapambano 51, ameshinda 35 kati ya hayo, 30 ni kwa Knockout na amepigwa mara 14, kati ya hizo, tatu ni kwa Knockout huku akitoka sare mara moja.

Bondia huyo anakamata nafasi ya saba kati ya mabondia 28 nchini wa uzani wa super middle, wakati duniani akiwa anakamata nafasi ya 280 kati ya 1638.


Pius Mpenda-WBC Peace
Licha ya mkanda wake wa ubingwa WBC Peace alioshinda mwaka jana Uturuki kwa kumchapa Dauren Yeleussinov wa Kazakhstan haupo kwenye orodha ya mikanda ya inayotambuliwa na Baraza la Ngumi Duniani kwa kuwa ulitumika kwa lengo la kuhamasisha amani mashariki ya kati.

Hata hivyo, ni mmoja wa mabondia wanaoshikilia mikanda iliyotoka WBC na rekodi ya kucheza mapambano 13, akishinda 10 kati ya hayo matano ameshinda kwa Knockout na amepigwa mara tatu kati ya hizo moja ni kwa Knockout.