Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

NYUMA YA PAZIA: Jamie Carragher, tuzibe masikio au tuendelee kumsikiliza?

PAZIA Pict

Muktasari:

  • Carragher amedai Mohamed Salah wa Liverpool ni mchezaji mkubwa, lakini anaangushwa na timu ya taifa anayochezea huku akidai haichezi katika michuano mikubwa. Anamaanisha Misri na anamaanisha kushinda michuano ya Afcon hakumpi Salah nafasi ya kuwa Mwanasoka Bora duniani.

JAMIE Carragher amekalia kitimoto kwa sasa. Amesemaje? Amedai michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) sio michuano mikubwa. John Obi Mikel amekuja juu kweli kweli. Waafrika wengi wamekuja juu kweli kweli. Binafsi sijielewi.

Carragher amedai Mohamed Salah wa Liverpool ni mchezaji mkubwa, lakini anaangushwa na timu ya taifa anayochezea huku akidai haichezi katika michuano mikubwa. Anamaanisha Misri na anamaanisha kushinda michuano ya Afcon hakumpi Salah nafasi ya kuwa Mwanasoka Bora duniani.

Carragher ni malaika au shetani? Anasema kweli au hapana? Hadi nitakapofika mwisho sitakuwa na jibu la msingi, lakini Carragher amenitafakarisha kitu. Kuna vitu ndani ya uwanja ambavyo inabidi tutafakari kwa makini zaidi. Kuna vitu nje ya uwanja inabidi tutafakari.

Ndani ya uwanja wachezaji wa Afrika wanaotamba Ulaya wanakuwa sio wale wakirudi katika timu zao za Afrika. Si kwamba hawapambani. Hapana. Kukusanyika kwao pamoja hakuleti ladha ile ile ambayo huwa wanaipeleka Ulaya.

PAZ 01

Unamtazama Mo Salah wa Liverpool halafu unamtazama Mo Salah wa Misri. Ni watu wawili tofauti. Sio kwamba Salah akiwa na Misri hajitumi, hapana, anajituma sana, lakini hauoni makali yake. Kwa nini hauoni makali yake? Kwa sababu amezungukwa na wenzake kutoka Afrika.

Kinachoshangaza ni wenzake nao utasikia wanacheza Ulaya. Hata hivyo, mkusanyiko wao hauwafanyi watoe kitu kile kile ambacho wanatoa Ulaya kila wikiendi. Bukayo Saka wa England ni sawa na Bukayo Saka wa Arsenal.

Wazungu au wale wa Amerika Kusini wakikusanyika wanakuwa wale wale tu. Sisi tunapokusanyika, hata kama ni wachezaji wa hali ya juu, lakini hatuleti ladha ile ile. Leo kama michuano ya Euro na Afcon ikichezwa kwa wakati mmoja nadhani watu wengi watapenda zaidi kutazama michuano ya Euro.

PAZ 02

Hii ni kutokana na kasi ya mchezo, maarifa, tempo, mazingira ya mechi, viwanja, idadi kubwa ya mashabiki waliopo uwanjani na mambo mengine. Weka mechi ya Ufaransa dhidi ya Denmark kisha weka mechi ya Ghana dhidi ya Cameroon utaona ni vitu viwili tofauti.

Weka mechi ya Brazil na Peru kule Amerika Kusini, kisha weka mechi ya Senegal na Algeria huku Afcon utaona ni vitu viwili tofauti. Huu ni ukweli ambao tunashindwa kujiambia licha ya kwamba tunamuona Carragher ni mbaya.

Labda kwa mastaa wetu kushindwa kutupa ladha kama ile ile ambayo huwa wanaitoa Ulaya, ndiyo maana hadi leo Afrika haijawahi kutwaa Kombe la Dunia wala kufika fainali ya michuano hiyo mikubwa zaidi kisoka duniani.

PAZ 03

Kombe la Dunia limewahi kutwaliwa na timu za Amerika Kusini na Ulaya tu. Hata hivyo, katika michuano mikubwa mbalimbali ambayo Waafrika wanashiriki na klabu zao za Ulaya huwa wanatwaa mataji haya kama kunywa maji tu.

Ukiorodhesha majina ya mastaa ambao wametwaa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na klabu mbalimbali za Ulaya ni kubwa. Kuanzia zama zile za kina Rabah Madjer, Abeid Pele, kina Finidi George na wengineo kibao. Hadi leo Waafrika wanatwaa michuano hiyo.

Tatizo ni mkusanyiko wa wenyewe kwa wenyewe tukiwa huku. Kwa nini kiwango hakiwi kile? Wakati mwingine timu ambazo zinakusanya wachezaji wengi wanaocheza Ulaya huwa wanafungwa na timu za kawaida tu.

PAZ 04

Itazame Ghana ambayo haijafuzu hata michuano ya Afcon pale Morocco. Mastaa wake ni hawa kina Thomas Partey na Mohamed Kudus wanaotamba Ulaya. Kaangalie walikuwa katika kundi gani kiasi cha kushindwa kutinga Afcon. Utaishia kucheka tu.

Tazama kikosi fulani cha Misri ambacho hakikuwa na wachezaji wanaocheza Ulaya kina Mohamed Aboutrika namna kilivyotwaa michuano ya Afcon mara tatu mfululizo. Kilifanya hivyo mbele ya nchi ambazo zilikuwa na wachezaji wengi wanaotamba Ulaya kina Nigeria, Senegal, Ivory Coast, Ghana na wengineo. Mpira wa Afrika haueleweki.

Tukiachana na ndani ya uwanja nadhani nje ya uwanja pia hatujafanya vyema. Sawa, tunakusanya mastaa wakubwa wanaotamba Ulaya lakini usidhani kama Wazungu wanawasha televisheni zao kufuatilia sana michuano hii.

PAZ 05

Kitu kibaya ni michuano hii inafanyika Januari wakati ligi mbalimbali zikiwa zimeshika kasi. Wazungu hawawezi kuhamisha rimoti zao kuacha kufuatilia ligi mbalimbali kubwa Ulaya na kutazama pambano la Ivory Coast dhidi ya Ghana.

Hakuna vituo vikubwa vya Televisheni vya Ulaya na Amerika Kusini ambavyo vitapambana kuwania kuonyesha moja kwa moja mechi za Afrika. Kinyume chake sisi huwa tunapambana kutafuta haki ya kuonyesha michuano ya Euro. Huu ni ukweli mchungu.

Sijui ni kipi ambacho kinafanya wasipambane, lakini naamini ni kwa sababu ya viwango vinavyoonyeshwa na timu zetu za huku. Hakuna mvuto mkubwa katika michuano yetu. Kabla hatujamvamia sana Carragher lazima tukubali kuna hata mastaa wetu huwa wanajitoa katika timu zao za taifa kuelekea katika michuano ya Afcon.

Wapo wengine wengi ambao wanashiriki kwa shingo upande kwa hofu ya kuonekana sio wazalendo kwa mataifa yao. Lakini kitu kinachotuachia maswali ni namna ambavyo ushiriki wao katika michuano ya Afcon unaacha pengo kubwa kwa timu zao za Ulaya. Wakija huku wanaonekana ni wachezaji wa kawaida lakini wakirudi kwao wanakuwa moto kweli kweli.

Huwa natabasamu kuona namna staa wa kimataifa wa Guinea, Serhou Guirassy anavyosumbua sana mabeki pale Bundesliga lakini katika mechi zetu dhidi ya Taifa Stars alibanwa vilivyo na Dickson Job na Ibrahim Bacca.