Nestory afananishwa na Alphonso Davies

BAYERN Munich imezishinda baadhi ya klabu kubwa barani Ulaya kwa kupata saini ya mzaliwa wa Tanzania, Nestory Irankunda ambaye anatajwa kuwa na kasi kama Alphonso Davies anayehusishwa kuondoka kwa miamba hiyo ya soka la Ujerumani.

Irankunda ambaye alizaliwa Kigoma kwenye kambi ya wakimbizi, ni kijana mwenye umri wa miaka 17 ambaye, Januari 2022 alikuwa mchezaji wa sita mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya A-League alipopata nafasi kwenye kikosi chake cha Adelaide United akiwa na umri wa miaka 15 tu.

Akimuongelea kinda huyo, mtaalamu wa kuwasoma wapinzani wa Bayern Munich, Michael Niemeyer alisema, “Anaonekana kuwa na kasi kama umeme, nadhani ni Davies mtupu tusubiri tumuone.”