Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mondi amleta Chama Simba

Chama: Muda utaongea, afunguka kila kitu agusia mkwanja wa Yanga

Muktasari:

KWA kipindi cha miaka miwili, msanii wa Bongo Fleva kutoka WCB Wasafi, Diamond Platnumz ametumia takribani Sh1 bilioni kununua vito vya madini vikiwamo pete, cheni na saa ya mkononi pekee.

KWA kipindi cha miaka miwili, msanii wa Bongo Fleva kutoka WCB Wasafi, Diamond Platnumz ametumia takribani Sh1 bilioni kununua vito vya madini vikiwamo pete, cheni na saa ya mkononi pekee.

Hivi karibuni Diamond aliweka wazi pete na cheni alizovaa mkononi zilifikia Dola 277,000 wastani wa Sh 637.8 milioni, ikiwa ni utamaduni wake wa kutaja bei ya vito anavyovaa.

Kiasi hicho cha fedha ni pungufu ya Sh98.1 milioni ya dau ambacho timu ya Simba walimuuza mchezaji wao, Clatous Chama, lakini kwa jumla vito vya Diamond vinazidi dau hilo kwa Sh262.1 milioni.

Kwa mujibu wa gazeti hili, viongozi watatu wa Simba walieleza Chama aliuzwa kwenda RS Berkane ya Morocco kwa dau la Dola320,000 wastani wa Sh735.9 milioni.

Utakumbuka msimu wa 2020/21, Chama alikuwa na kiwango bora, alicheza michezo 28 na kutoa pasi za mwisho za mabao 15, akifunga mabao manane, hivyo kwa jumla akihusika katika mabao 23. Hilo linamfanya kuhusishwa na tetesi za kusajiliwa na timu ya Yanga katika dirisha dogo la usajili mwezi ujao.

Sasa Diamond anadai pete tano alizovaa vidoleni ambazo kwa kuangalia herufi ya kila pete zinatimiza neno Simba ambalo ni jina lake la utani, zimegharimu Dola 100,000 wastani wa Sh230.2 milioni, cheni za mkononi zimegharimu Dola 177,000 wastani wa Sh407.5 milioni. Hivyo kuleta jumla ya Dola277,000 karibu Sh637.8 milioni.

Ikumbukwe baada ya kumaliza shoo zake Marekani, Agosti 2019 Diamond alichapisha video mtandaoni ikimwonyesha akiingia dukani na kununua cheni za almasi kwa gharama ya Dola 21,000 karibu Sh48.7 milioni.

Mwimbaji huyo kupitia Insta Story alionyesha risiti aliyopatiwa mara baada ya kufanya manunuzi hayo. Kabla ya hapo, aliwahi kujigamba vitu anavyovaa kama urembo huwezi kuvipata sehemu yoyote Tanzania.

Baada ya hapo alionekana amevaa saa ya kifahari iitwayo Richard Mille (RM) ambazo zinatengenezwa nchini Uswis tangu mwaka 2001 na kampuni hiyo iliyoundwa na Dominique Guenat na Richard Mille.

Sasa Diamond alivalia saa hiyo aina ya RM 011 Felipe Massa Red Baden ambayo bei yake inatajwa ni Dola 141,000 karibu Sh327 milioni.

Kwa muktadha huo, kama saa hiyo ya RM 011 Felipe Massa Red Baden aliinunua kwa fedha zake, basi kwa kipindi cha miaka miwili Diamond atakuwa ametumia Sh1 bilioni ukiwa umejumlisha na zile Sh 637.8 milioni na Sh48.7 milioni za hapo awali.

Hakuna ubishi baada ya tetesi nyingi, kiasi hicho cha fedha alichotumia Diamond aliyeshinda na kutunukiwa tuzo zaidi ya 45 katika muziki, kinaweza kumrejesha nchini Chama ambaye Oktoba 21, 2021 alifanikiwa kushinda tuzo za TFF 2020/21 kama kiungo bora wa Ligi Kuu Bara akiwa amewashinda Feisal Salum na Mukoko Tonombe wote wa Yanga.