Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Misosi hatari kwa wachezaji

Muktasari:

  • Lishe isiyo sahihi kwa mchezaji inaweza kusababisha mchezaji kupungua nguvu kupata majeraha kwa urahisi na kushindwa kuwa makini kisaikolojia wakati wa mchezo.


MWILI wa binadamu unahitaji nishati ya kutosha kabla ya kuingia kwenye shughuli yenye matumizi makubwa ya nguvu kama ulivyo mchezo wa soka.


Lishe isiyo sahihi kwa mchezaji inaweza kusababisha mchezaji kupungua nguvu kupata majeraha kwa urahisi na kushindwa kuwa makini kisaikolojia wakati wa mchezo.


Kwa mujibu wa ripoti ya The Sun mchezaji maarufu Cristiano Ronaldo amekuwa akipendea kutumia uji, ndizi na mayai kila asubuhi kabla ya mechi.

Mwanaspoti imezungumza na wachezaji na madaktari ambao wamefunguka vyakula wanavyokula huku madaktari wakitaja vyakula gani sahihi na madhara ya vyakula visivyo sahihi kwa wachezaji saa chache kabla ya mechi.

Mchezaji wa Dodoma Jiji, Idd Kipagwile anasema timu ndogo kuzingatia suala la lishe ni changamoto kubwa, lakini kwa mchezaji anayetambua umuhimu anajiongeza mwenyewe.

“Kwa hapa Dodoma Jiji huwa tunafuata ratiba ya chakula kwa siku hasa timu inapokuwa kambini siku zote kuna kuwa na ugari na wali  hivyo mchezaji anakula anachopendezwa nacho kwa siku husika,” anasema na kuongeza;

“ratiba huwa inabadilika lakini sio mara kwa mara chakula mara nyingi ni kile kilesi unajua bajeti za timu zetu naomba kukiri kuwa huwa hatufuati taratibu maalu siku za mechi ninachofahamu ambacho madaktari wengi wamekuwa wakishauri ni kula tambi na nyama nyeupe siku ya mechi lakini ndio ivyo timu nyingi hazizingatii hili.”

Kipagwile anasema timu ni nyingi zisizo fuata maelekezo hayo hasa timu ndogo huku akikiri kuwa kinachofuatiliwa zaidi ni matokeo mazuri bila kujali wachezaji wamekula nini huku akitolea mfano Azam FC timu ambayo ameitumikia kuwa hiyo kwa asilimia kubwa wanazingatia.

“Kwa asilimia kubwa tunakula tu ili kujaza matumbo lakini vyakula vingine havina faida kwetu sisi wachezaji, madaktari wengi hawatoi elimu lakini pia timu hazichukulii umakili swala la chakula lakini sizilaumu nafikili ni kutokana na bajeti,” anasema.

Kiungo Abal Kassim Suleiman wa Pamba Jiji  anasema timu nyingine wachezaji wanakula kutokana na namna wanavyoandaliwa ilimradi chakula kiingie tumboni.

“Chakula hatuchagui sisi lakini mara nyingi tunakula wali kuku lakini pia tambi zinakuwepo na matunda kama tikiti maji au chungwa lazima viwepo pamoja na maji mengi,” anasema na kuongeza:

“Ugali na wali ni vitu ambavyo vimekuwa vikijirudia mara kwa mara kwenye ratiba ya chakula hasa tukiwa kambini kujiandaa na mechi husika na huwa tunakula saa sita mchana kama mechi ni saa kumi jioni.”

Nahodha wa Azam FC, Lusajo Mwaikenda anasema siku ya mechi kwa upande wake amekuwa akikwepa zaidi kutumia vyakula vya mafuta na ni muumini mkubwa wa kuzingatia lishe kulinda kipaji chake.

“Mimi kama mimi binafsi naogopa sana kula vyakula vyenye mafuta mengi na pia kwa ujumla kama timu wanaepuka sanaa kuweka vyakula vya aina  hiyo siku ya mechi,” anasema.

Kiungo wa Kagera Sugar aliyewahi kuitumikia Simba miaka ya hivi karibuni na kuhamia timu nyingine anasema, timu ndogo chakula wanakula tu ili washibe na ndio maana wachezaji wanakosa nguvu tofauti na wale wa timu za Simba, Yanga na Azam.

“Huku ni ngumu sana kuzingatia lishe kwa sababu ya bajeti ya timu lakini chakula kinapatikana ili masuala ya kuzingatia ni mchezaji kujiongeza mwenyewe tofauti na timu kubwa,” anasema na kuongeza:

“Kitu muhimu zaidi kama maji na matunda ndio kinazingatiwa zaidi nyama ugari vinalika tu kutegemea na ratiba siku hiyo imeangukia nini nafikiri elimu ya lishe itolewe kwa viongozi na wapishi ili kuondoa changamoto iliyopo.”

Beki wa Coastal Union, Lameck Lawi anasema wao wanapendelea kula wali nyama - chakula ambacho kwa mujibu wa daktari sio sahihi hasa nyama kwa sababu inachelewa kusagika tumboni.

“Tunakula kwa sababu ndio chakula tunakuwa tumeandaliwa wakati huo na huwa tunakula saa sita hadi saba kabla ya mechi ambayo inachezwa saa kumi siku hiyo ili kutoa muda wa kusagika kwa chakula hicho kabla ya mchezo,” anasema.

Kiraka wa Tanzania Prisons, Salum Kimenya anasema kwa upande wao saa chache kabla ya mechi huwa wanapendelea kula matunda ambayo yanawaongezea sukari na maji maji mwilini.

“Huwa tunakula ndizi na ‘apple’ kwa sababu ni matunda yenye faida kubwa mwilini muda mchache kabla ya mechi,” anasema.


WASIKIE MADAKTARI

Daktari wa zamani wa Yanga, Shecky Mngazija anasema wachezaji hawaruhusiwi kula vyakula vyenye mafuta mengi kwa sababu vinanenepesha na vina uwezo wa kumuongezea uzito mchezaji.

“Mchezaji hapaswi kula ili kujifurahisha au kujaza tumbo ni muhimu kuzingatia mlo sahihi ili aweze kucheza kwa ubora kwanza mbali na vyakula vya mafuta lakini pia hapaswi kula vyakula vyenye sukari,” anasema na kuongeza:

“Mbali na vyakula vya mafuta pia mchezaji hatakiwi kula vyakula vyenye uchachu kwasababu vinasababisha gesi tumboni lakini pia vyenye pilipili sio sahihi pia inaongeza gesi ikizidi inajaza tumbo.”

Anasema pia sio sukari yote ni nzuri kwa mchezaji huku akibainisha kuwa sukari inaongeza uzito kwa mchezaji kama sio asili hivyo wachezaji wanapaswa kuzingatia hilo.

“Lakini pia nyama nyekundu sio sahihi kwa mchezaji saa chache kabla ya mechi labda kwa sababu haisagiki halaka tumboni kitu sahihi ni kuku au samaki.” Anasema.

Akizungumzia vyakula sahihi, Mngazija anasema mboga mboga mchemsho wa kuku na vitu vya sukari  ya asili mfano kwenye miwa au asali ni muhimu kwa mchezaji saa chache kabla ya mechi na maji ya kunywa muhimu sana kwasabasu misuli inapata nguvu.

Anasema wachezaji wanahitaji nguvu kwa asilimia kubwa hivyo wanawapa kipaumbele kwenye vyakula vya wanga kwa asilimia 70, protini 15%, mafuta 10%, madini na vitamini 5%.

“Wachezaji wanatakiwa kupewa vyakula vya wanga kama mihogo, mahindi kwa kuwa vina wanga mwingi, pia matunda, maji na mboga za majani kwa wingi kwa kuwa tunaamini afya bora ndio mtaji wa wachezaji kwa kufikisha malengo ya timu,” anasema Mngazija.

“Mbali na maji ambayo ni muhimu kinywaji pekee tunachowashauri kutumia kwa wingi ni juisi ya matunda asilia na hawapaswi kuweka sukari yoyote kwa kuwa sukari haturuhusu kutumia pasipo kuichemshwa jikoni.

“Vinywaji vya kuongeza nguvu ‘energy’ na soda haturuhusu kabisa kwa sababu soda zinabeba sukari nyingi sana ambazo ni hatari kwa afya zao hasa mapigo ya moyo na uzito,” anafafanua Mngazija.

Daktari wa Namungo, Richard Yomba anasema sheria ya FIFA ina kauli tatu kuhusu chakula mchezaji haruhuwi kucheza na njaa, hana kitu tumboni sheria hiyo ndio inawafanya wachezaji wahakikishe wanakula saa chache kabla ya mechi.

“Mchezaji anakula ili asiwe na njaa sio kwamba chakula anachokila siku hiyo ndio kitampa nguvu ya kucheza, hapana na ndio maana mchezaji anatakiwa kula kidogo saa chache kabla ya mchezo,” anasema.

Anasema mchezaji hatakiwi kula chakula chenye sukari ambayo sio asili na kuweka wazi kuwa na ndio maana mataifa makubwa yaliyoendekea kisoka yamekuwa yakitengeneza sukari ya moja kwa moja akitokea mfano wa kinywaji aina ya eneji ambacho ameweka wazi kuwa kina sukari na protini.

“Mchezaji kwa siku anatakiwa kula protini kwasababu ina kazi nyingi mwilini, vitu muhimu ambavyo anatakiwa apate juisi ya miwa ambayo ina sukari ya asili lakini pia anashauliwa kunywa chai ya langi yenye kahawa ina faida mwilini hasa kichwani inaondoa uchovu, damu kufanya kazi,” anasema na kuongeza:

“Mchezaji akinywa chai robo na biskuti mbili saa chake kabla ya mechi itamsaidia kwa sababu chai inafaida nyingi, kama sio chai ndizi kwasababu ina sukari ya moja kwa moja, wakati wa kutoka mapumziko apple linafaa kwa sababu lina maji maji.”

Daktari Azam FC, Mbaruku anasema anatakiwa kula chakula chepesi fresh juice, tende, matunda kipande cha keki, biskuti, ugali, nyama saa nne kabla ya mchezo husika.

“Mechi ya saa moja, binadamu yeyote anahitaji mlo kamili kwa wanamichezo vyakula vinavyotia nguvu, mchele, ngano, muhogo lazima apate protini misuri inatumika sana kwenye Suala la nyama ya ng’ombe ni protini 99% hivyo ni muhimu kwa mchezaji licha ya mmeng’enyo wake kuchelewa.”

Anasema vitu vingine muhimu madini na vitamini anapata kwenye matunda mbogamboga ambayo amesisitiza kuwa hayatakiwi kukosekana.

“Mchezaji mahitaji yake ni makubwa supriment mbalimbali ambazo zina vitamini madini mbalimbali mlo kamili nyama, samaki ni sehemu ya mlo ukiacha kula nyama basi upate samaki, maharage, kunde mbaazi hakuna ubaya kula kwa kiasi,” anasema na kuongeza:

“Chai ya rangi haina kitu muhimu zaidi ya kahawa ambayo ina vichocheo vya kusisimua mwili na kwenye michezo mchezaji anatakiwa kuchangamka.”

Daktari Mashujaa Samuel Wambura anasema: “Kabla ya mechi kuanza ndizi na apple, ndio vitu sahihi zaidi kwa mchezaji kula na vitu ambavyo haviruhusiwi ni pamoja na ugali hairuhusiwi kiafya haijakaa vizuri mmeng’enyo wake unachelewa,” anasema.

Lakini alitokea ufafanuzi suala la nyama ya ng’ombe ambayo licha ya kuwa na protini nyingi lakini ina madhara kwa mchezaji kula saa chache kabla ya mechi kutokana na mmeng’enyo wake kuchelewa.

‘’Mchezaji anatakiwa kula chakula saa sita mechi saa kumi watu hawashauliwi kula sana vitu muhimu ni ndizi za kuiva, wali kiasi na kuku au samaki,” snasema.


CHAKULA SAHIHI

Sukari ndiyo kama mafuta au petroli, inayotumiwa na mwili kuendesha mambo mbalimbali ukiwamo utendaji wa ubongo na shughuli za kimwili.

Sukari huweza kuhifadhiwa katika ini na misuli na kutumika baadaye kama nishati ya akiba pale mwili unapohitaji kufanya shughuli mbalimbali ikiwamo kutembea, kukimbia, kuongea na kufikiri.

Ukiacha wanga, protini ya kwenye misuli na mafuta ya mwili ni chanzo cha kupata sukari (nishati). Kama utakula kiasi kidogo cha wanga mwili itabidi itumie vyanzo vya protini na mafuta kupata sukari.

Kama utakula wanga ya kutosha ina maana ile protini ya kwenye misuli haitatumiwa kama chanzo cha sukari badala yake protini itabaki katika kazi yake yakujenga.

Mchezaji anaweza kula chakula cha wanga kama tambi au wali kiasi na mboga za majani. Hapa anapaswa kuchanganya na kiasi kidogo cha chakula chenye protini ambacho hakina mafuta na samaki wa kuchemsha anapendekezwa zaidi.

Saa moja kabla ya kucheza maz­oezi au muda mfupi kabla ya kupa­sha misuli moto, mchezaji anawe­za kula matunda kama ndizi mbivu mbili au moja ama tufaa (apple)


MUDA WA KULA KABLA YA MECHI

Mchezaji anatakiwa kula chakula saa tatu kabla ya mchezo na hiy ina maana kwamba kama mechi inanaza saa 10:00 jio­ni mchezaji an­apaswa kula saa 7:00 mchana lakini pia wataalamu wa lishe wanasema inapaswa kuwa zaidi ya hapo.

Kwamba, mche­zaji inafaa zaidi apate chakula saa tatu na nusu kabla ya kufan­ya mchezo, hii ina maana muda unao­faa zaidi ni saa 6:30 mchana ili acheze vizuri.