Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mipango Simba ikijipanga inatoboa!

Mipango Simba ikijipanga inatoboa!

WAWAKILISHI wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika, Simba wamepangwa kwenye kundi D la mashindano hayo ambalo litakuwa pia na timu za RS Berkane ya Morocco, Asec Mimosas (Ivory Coast) na US Gendarmerie Nationale ya Niger.

Timu mbili zitakazomaliza katika nafasi mbili za juu kwenye kundi hilo zitatinga hatua ya robo fainali ya mashindano hayo ya pili kwa ngazi ya ukubwa barani Afrika.

Ni kundi ambalo linajumuisha timu tatu zenye uzoefu mkubwa wa mashindano ya klabu Afrika ambazo ni Simba, Berkane na Asec Mimosas kutokana na ushiriki wao na mafanikio ambayo zimewahi kuyapata hapo nyuma ingawa wapo Gendarmerie ambao ni wageni katika hatua hiyo wakiwa ndio kwanza wanaanza kuchomoza katika medani ya soka barani humu.

Mwanaspoti linakuletea dondoo na wasifu wa timu hizo tatu ambazo zimepangwa pamoja na Simba katika kundi D, ili kukupa taswira ya ugumu na wepesi ambao wawakilishi hao wa Tanzania watakutana nao katika harakati za kutimiza malengo yao.


RS Berkane

Iliasisiwa mwaka 1938 wakati huo ikiitwa Association Sportive de Berkane na mwaka 1971 ilibadilisha jina na kuanza kuitwa Renaissance Sportive de Berkane (RS Berkane).

Inatumia jezi za rangi ya machungwa na bukta nyeupe wakiwa nyumbani na ugenini wanatumia jezi nyeusi na bukta za rangi ya machungwa na jezi yao ya tatu ni rangi nyeupe yenye ufito wa rangi ya machungwa mikononi.

Timu hiyo inatumia Uwanja wa Manispaa wa mji wa Berkane kwa mechi zake za nyumbani ambao unaingiza jumla ya mashabiki 10,000.

Mafanikio makubwa kwa timu hiyo ni kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2019/2020 na kumaliza katika nafasi ya pili ya taji la Caf Super Cup mwaka 2021 huku ikiishia nafasi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2018/2019.

Inanolewa na kocha Florent Ibenge kutoka DR Congo na kikosi chake kinaundwa na idadi kubwa ya wachezaji wazawa huku wa kigeni wakiwa watano ambao ni Tuisila Kisinda na Chadrack Lukombe (DR Congo), Clatous Chama (Zambia), Issoufou Dayo (Burkina Faso) na Mamadou Camara (Senegal)


Asec Mimosas

Simba imeshawahi kukutana na Asec Mimosas mara nne katika mashindano ya kimataifa ambapo imeibuka na ushindi mara moja huku timu hiyo ya Ivory Coast ikiibuka na ushindi mara tatu.

Asec Mimosas iliasisiwa mwaka 1948 na imekuwa ikitumia Uwanja wa Taifa wa FÈlix-HouphouÎt-Boigny unaoingiza takribani mashabiki 50,000 uliopo jijini Abidjan kwa mechi zake za nyumbani.

Ni timu iliyozalisha idadi kubwa ya mastaa wanaotamba duniani kupitia kituo chake cha kulelea vipaji na miongoni mwao ni Bonaventure Kalou, Didier Zokora, Emmanuel Eboue, Bakari Kone, Gervinho, Salomon Kalou, Romaric, Boubacar Barry, Didier Ya Konan, Kolo Toure na Yaya Toure

Jezi ambazo Asec Mimosas inazitumia kwa mechi za nyumbani zina rangi ya njano na michirizi yenye rangi nyeusi wakati ugenini inavaa jezi nyeusi zenye mchoro wa umbo la mstatili la njano kifuani.

Kwa sasa timu hiyo inanolewa na kocha Cesar Lambert Amani Yao ambaye ni raia wa Ivory Coast na ina mchezaji mmoja tu wa kigeni ambaye ni Clement Pitroipa kutoka Burkina Faso.

Imewahi kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1998 lakini pia katika nyakati tofauti imewahi kufika hatua ya fainali, nusu fainali, robo fainali na makundi ya mashindano ya klabu Afrika.


US Gendarmerie Nationale

Iliasisiwa mwaka 1996 hivyo ndio kwanza ina umri wa miaka 25 tangu ilipoanzishwa.

Wanatumia Uwanja wa General Seyni Kountche unaoingiza jumla ya mashabiki 35,000 ulioko katika mji mkuu wa Niger, Niamey kwa mechi zao za nyumbani.

Inafundishwa na kocha Zakariou Ibrahim ambaye ni mzawa na kikosi chake kinaundwa na idadi kubwa ya wachezaji wazawa.

Mafanikio makubwa kisoka kwa USGN ni kufika hatua ya makundi ya mashindano hayo msimu huu.


Mipango tu

Kama Simba itakomaa kwenye mechi tatu mfululizo za awali, kama ilivyofanya msimu uliopita kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, itakuwa na nafasi kubwa ya kusonga mbele kundini sambamba na timu moja wapo kati ya Asec na Rs Berkane.

Hata hivyo, Simba haipaswi kuwachukulia poa wapinzani wao, ili kuepuka aibu iliyowahi kuwakuta mbele ya UD Songo ya Msumbiji au Jwaneg Galaxy ya Botswana waliovaana nao raundi za kwanza misimu tofauti na kukwama wasisonge mbele.

Kitu muhimu kama alivyonukuliwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mulamu Nghambi ni kuanza maandalizi mapema kabla ya kuanza kitimtimu cha mechi hizo za makundi ambao inashiriki baada ya kuchemsha kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ikizuiwa na Jwaneng.