Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mil 400 zilivyomnyima kiungo ulaji Azam FC

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Kiungo huyo raia wa Somalia, amepiga stori na Mwanaspoti na kuzungumza mengi katika maisha ya soka tangu atue hapa nchini msimu wa 2023-2024 akitokea Kibra United ya Kenya, jambo analojivunia maishani. Tiririka!

KIUNGO nyota wa KMC, Ibrahim Elias 'Mao' ameelezea safari ya miaka miwili katika soka la Tanzania, huku moja ya jambo kubwa analolielezea ni kitendo cha kushindwa kuichezea Azam FC sababu ikiwa ni kiasi cha Sh400 milioni.

Kiungo huyo raia wa Somalia, amepiga stori na Mwanaspoti na kuzungumza mengi katika maisha ya soka tangu atue hapa nchini msimu wa 2023-2024 akitokea Kibra United ya Kenya, jambo analojivunia maishani. Tiririka!


SH400 MILIONI ZAMKOSESHA DILI

Nyota huyo aliyejaaliwa kipaji kikubwa anasema ilibaki kidogo tu ajiunge na Azam FC kabla ya kutua KMC, ingawa ilishindikana kutokana na mkataba wake kuhitajika kuvunjwa kwa Sh400 milioni.

"Msimu wa 2021–2022 nilikuja hapa Tanzania nikiwa na timu ya Horseed ya Somalia wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Azam, baada ya hapo viongozi wao walinihitaji, ila kwa bahati mbaya ikashindikana," anasema.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

"Tulikubaliana kila kitu, ila shida ikawa mazungumzo na timu nayochezea kuhitaji kiasi cha Sh400 milioni ili nivunje tu mkataba wangu. Kwa kipindi kile ilikuwa ngumu na ndipo dili likashindikana nikaamua kubakia tena kwa msimu mwingine."


URAFIKI NA MOALLIN

Mao anasema mmoja wa makocha atakayebaki katika kumbukumbu zake nzuri maishani ni Abdihamid Moallin aliyewahi pia kufanya naye kazi akiwa na Horseed ya Somalia, kisha kuungana tena KMC.

"Kuna watu walikuwa wanasema hata kucheza kwangu mara kwa mara ilitokana na uwepo wake. Niwaambie tu Moallin anapenda sana mtu anayejituma na huwa haangalii urafiki kwenye kazi. Atabakia mtu muhimu kwa sababu amenifundisha mambo mengi."


MZALIWA WA KENYA

Nyota huyo anasema yeye ni mzaliwa kabisa wa Kenya ila wazazi wake ni watu wa Somalia, japo baadhi yao wamekuwa hawajui jambo hilo, ingawa anafurahia malezi aliyoyapata katika nchi hizo mbili tofauti kwa sababu zimemkuza kimwili na kiakili.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

"Nilianza kuichezea timu ya vijana ya Kenya chini ya miaka 17 na 20, ila baada ya kuonyesha kiwango kizuri Somalia pia wakanihitaji ili nikaichezee, hivyo nikaamua kwenda kuichezea kwa sababu wazazi wangu wote wawili ni wazaliwa wa huko," anasema.


CHIMBUKO LA 'MAO'

Anasema jina hilo sio A.K.A kama wengi ambavyo wamekuwa wakimuita isipokuwa ni la Babu yake aliloamua kumpa, kwa sababu ya malezi bora aliyompatia, kuanzia jinsi ya kuishi na watu, kujiamini na kutokata tamaa katika maisha ya upambanaji.

"Ni moja ya Babu yangu ambaye siku zote anabaki katika kumbukumbu ya maisha yangu ndio maana napendaga kutumia Ibrahim Elias 'Mao', amenifundisha mambo mengi ya uwajibikaji ambao hadi leo kwangu najivunia maishani kila sehemu ninayoenda."


BONGO PATAMU

'Mao' anasema Tanzania ni nchi nzuri kuishi ambapo hakuna mtu anayeweza kutoka sehemu yoyote akashindwa kwa sababu ya ukarimu na uhuru wa watu wake, huku akiweka wazi ni tofauti na Kenya na Somalia ambao wengi wao wanaishi kivyao vyao.

"Tanzania ina watu wakarimu sana, kwa mara ya kwanza wakati nakuja nilipata changamoto kwa sababu hakuna niliyezoeana naye ila kadri nilivyoishi hapa nilijikuta nikipata marafiki wengi, jambo hilo lilinifanya nipende mazingira ya hapa."

New Content Item (1)
New Content Item (1)

HUMWAMBII KITU NA MIHOGO

Anasema anapenda sana kula mihogo iwe ya kuchemsha au kukaanga kwani imekuwa ratiba yake ya siku zote na kufurahia aina ya upikaji wake, huku akieleza mbali na hilo ila anafurahia ugali na samaki na amekuwa akiishi kwenye mazingira hayo.

"Tangu nipo Kenya huwa napenda sana kula mihogo na samaki, nimekuja Tanzania nikaipenda pia, imekuwa ni kawaida yangu na nimekuwa nikiishi katika mazingira hayo, licha ya hayo ila nazingatia mwili wangu usiongezeke zaidi ya hapa nilipo."


LIGI YA BONGO BAB'KUBWA

Nyota huyo anasema Ligi ya Tanzania imepiga hatua kubwa tofauti na nchi za Kenya na Somalia, huku akiweka wazi sababu ni kutokana na usimamizi mzuri, udhamini ambao ndio siri inayowafanya wachezaji wengi kutamani kupata nafasi ya kuichezea.

"Nchi zote mashabiki wanapenda mpira ila shida inakuja kwenye kujitangaza na kwenye maslahi binafsi, hapo ndipo Tanzania imepiga hatua kubwa tofauti na nchi za Kenya na Somalia, wachezaji wanavutiwa kutokana na sababu hizo ambazo ni muhimu."


MAJERAHA YAMTIBULIA

Mao anasema msimu huu umekuwa ni mgumu kwa sababu ya kusumbuliwa na majeraha ya nyama za paja yaliyomuweka nje kwa miezi miwili, ingawa anashukuru ameanza kurejea taratibu, licha ya kukiri ushindani umekuwa mkubwa na nyota wengine waliopo.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

"Nilitamani sana kufanya vizuri msimu huu tofauti na uliopita, ila majeraha ya mara kwa mara yameniharibia. Jambo zuri nalofurahia ni kurejea tena mazoezini na ninapambana kwa hali na mali ili nirudi kwenye kiwango changu bora," anasema.

Anasema haitakuwa rahisi kuingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza kutokana na ushindani wa nafasi uliopo, huku ishu nyingine ni kushindwa kuonekana na kocha mpya, Kally Ongala, jambo linamfanya kupambana zaidi mazoezini.

"Ongala amekuja katikati ya msimu na ndio kipindi ambacho nilikuwa nauguza majeraha yangu, ninafanya kila liwezekanalo ili nimshawishi kwenye uwanja wa mazoezini nipate nafasi ya kucheza, licha ya ukweli kwamba ushindani ni mkubwa sana."


ISHU YA MKATABA MPYA

Anasema mkataba wake na KMC unamalizika mwishoni mwa msimu huu ingawa hajafikia uamuzi wa kuamua kubaki au kutafuta changamoto sehemu nyingine, japo mazungumzo na viongozi wa timu hiyo yanaendelea vizuri licha ya kutofikia muafaka.

"Kama nitabaki au kuondoka kila kitu kitajulikana mwisho wa msimu huu. Kwa sasa malengo yangu ni kuhakikisha naipambania KMC ifanye vizuri. Nafurahia sapoti na ushirikiano uliopo baina yetu, hivyo tusubiri kwanza kuona kitakachotokea mbele."

New Content Item (1)
New Content Item (1)

MUVI NDIO MPANGO MZIMA

Tofauti na ufundi wa kucheza soka ambao nyota huyo amekuwa nao, mchezaji huyo anasema anapenda sana kuangalia muvi kila akimaliza majukumu yake uwanjani kwa siku husika, kwani sio mtu wa kupenda kwenda kujirusha kwenye kumbi mbalimbali za starehe.

"Nikimaliza mazoezi au mechi huwa napenda kukaa chumbani na kuangalia muvi mbalimbali, hii inanisaidia hata kama nikiwa na siku mbaya kazini kwa sababu ndio muda najichanganya na mambo mengine, tofauti na hapo pia napenda kulala," anasema.


SIMBA, YANGA FRESHI

Mao anasema hawezi kufunga milango ya kuzichezea timu kubwa hapa nchini za Simba na Yanga, kwani katika maisha kila siku hakuna anayejua kesho yetu, hivyo kama ikitokea mojawapo kati ya hizo itakayomtaka ataangalia pia uwezekano huo.

"Sikuwahi kufikiria kama ipo siku nitacheza Tanzania ila limetokea hilo. Haya ni maisha na hakuna anayejua kesho yetu, ikitokea kupata nafasi hiyo au sehemu nyingine nitafurahia pia kwa sababu kila jambo linalotokea ni la Mwenyezi Mungu," anasema.