Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MBELWA: Kazichapa mara 100, lakini anaishi kama hana rekodi

MBELWA Pict

Muktasari:

  • Licha ya ukubwa wa jina lake pamoja na familia yake katika mchezo huo lakini Matumla aliyeanza kucheza ngumi za kulipwa Aprili 4, mwaka 1993 hakuweza kufikia rekodi ya kucheza mapambano 100  ya ngumi za kulipwa.

MPAKA anaachana na mchezo wa ngumi za kulipwa nchini mwaka 2013, bondia Rashidi Matumla 'Snake Boy' aliishia kucheza mapambano 72 pekee katika mchezo huo huku akibeba mikanda mbalimbali.

Licha ya ukubwa wa jina lake pamoja na familia yake katika mchezo huo lakini Matumla aliyeanza kucheza ngumi za kulipwa Aprili 4, mwaka 1993 hakuweza kufikia rekodi ya kucheza mapambano 100  ya ngumi za kulipwa.

Lakini siyo yeye tu, yupo bondia mmoja anayeitwa Kalama Nyilawila ambaye 2018 aliachana na mchezo huo akiishia kucheza mapambano 47 huku akiwa ameanza kupanda ulingoni 2005.

Hivi unalikumbuka jina la bondia Mada Maugo? Huyu alipigana, lakini amejaliwa kuwa na maneno makali ya kukera kwa wapinzani wake, ila mpaka sasa rekodi yake inasoma amepigana mapambano 49 yaani amebakisha pambano moja pekee kufikia 50 ila kufika 100 bado ana safari ndefu.

MB 01

Watoto wa 2000 ambao wamekuwa maarufu kama kizazi kipya kinachotajwa kwa sasa ndiyo wakati ambao Francis Cheka anaingia kupigana kwenye ngumi za kulipwa.

Cheka alianza kupigana Februari 26, 2000 na mpaka anaachana ngumi 2018 ameishia kucheza mapambano 49 peke yake, lakini hakuweza kufikia 100.

Lakini, miaka saba baadaye kidume kutoka mkoani  Morogoro, Said Mbelwa ambaye amekuwa maarufu kama moto wa gesi ndiyo alikuwa akiufungua ukurasa wake katika mchezo wa ngumi za kulipwa nchini.

Achana na historia ya mikanda aliyowahi kupigania, lakini ndiye bondia pekee nchini mwenye rekodi ya kupigana mapambano mengi zaidi akifikisha 100.

MB 02

Mbelwa ambaye alianza kupigana ngumi za kulipwa Novemba 18, 2007, amefanikiwa kufikisha mapambano 100 akiwa ndani ya ulingoni na bado akiendelea kupigana yaani hajaweka wazi wakati gani ataachana na mchezo huo.

Bondia huyo mwenye rekodi kushinda mapambano 47 kati ya hayo 31 akishinda kwa knockout, amepigwa mara 44 kati ya hizo 20 ikiwa ni kwa knockout na ametoka sare mara sita.

Mbelwa anayepigana kwenye uzani wa light heavy kwa sasa anakamata nafasi ya 15 kati ya mabondia 25 wa uzani huo nchini wakati duniani akiwa bondia wa 927 katika mabondia 1788.

Mwanaspoti limefanya mahojiano maalumu na bondia huyo kutokana na kuwa bondia pekee nchini aliyeweka rekodi ya kupigana mapambano 100, ambapo kwa sasa anafikiria kutangaza kustaafu.

MB 03

Bondia huyo anaeleza kuwa kamwe hawezi kusahau safari yake kwenda Afghanstan kupigana katika nchi ambayo ilikuwa na wakati mgumu wa vita, huku yeye akiificha familia yake juu ya safari hiyo.

"Unajua familia hawakuwa wakielewa naenda wapi zaidi ya wao kujua kama naenda Ujerumani kuna kisiwa fulani ndiyo naenda," anasema Mbelwa na kuongeza:

"Lakini safari yangu ilikuwa Afghanstan. Niliondoka na kocha wangu Mkenya Julius Odhiambo ingawa ilinishangaza maisha ya kule baada ya kutoka nje ya uwanja wa ndege niliona kila aina ya kifaru cha kivita na watu wakitembea na silaha za moto kwa ajili ya kuilinda nchi yao.

"Kiukweli sikuwa na hofu kwa sababu uwanja wa ndege nilikuja kupokewa na rais wa nchi yao, Hamid Karzai  maana hata hoteli ambayo nilifikia ilikuwa karibu na Ikulu yake.

"Binafsi niliishi vizuri katika nchi yao ingawa changamoto ilikuwa kusikia milipuko ya mabomu ilivyokuwa inatokea katika maeneo tofauti ambayo yalikuwa yakijenga hofu japo wenyewe walikuwa kawaida.

MB 04

"Nakumbuka kuna wakati nilipelekwa kutembea kwenye nyumba ya Osama Bin Laden na Mullah Omar, tukasimamishwa na wanajeshi tuliokutana nao njiani kwa ajili ya kutuhoji ila uzuri tulikuwa na maofisa wa Ikulu yao ndiyo ikawa wepesi wetu japokuwa hawakuamini kama nilikuwa bondia.

"Mafanikio ambayo nilipata kule nikaja kuyafanya nyumbani huku Tanzania na mpaka nafikisha mapambano 100 nashukuru Mungu amejalia nimepata nyumba nne kupitia mchezo huu.

:Nyumba tatu zipo Chanika na moja ipo Morogoro na hapa nilipo najiandaa kuachana na mchezo huu kwa sababu rekodi yangu ni kubwa. Nimefikisha mapambano 100 sijapata madhara yoyote ya kiafya sina budi nimshukuru Mungu maana wengine wanapata vilema vya kudumu.

SWALI: Ukiambiwa jambo gani huwezi kulisahau katika hayo mapambano 100 uliyocheza hadi kufikia sasa?

MB 05
MB 05

JIBU: "Naweza kukwambia ni Afghanstan pekee kwa sababu sijawahi kuona mtu amekaa kifuani amebeba mikanda ya risasi miwili na silaha zake mbili nzito kwa ajili ya kulinda nchi yake...siwezi kusahau hadi nakufa hilo jambo.

SWALI: Watu wa Chanika huwa wanachukuliaje wakiona bondia mkubwa, lakini bado unauza chips na kuku wa kuchoma barabarani?

JIBU: "Unachosema ni ukweli hao watu wapo, wajinga wapo na welevu wapo lakini wanatakiwa kufahamu kwenye maisha nilianzia kwenye ufundi wa magari makenika mwaka 1991, niliachana nayo nikahamia kwenye udereva magari.

"Niliendesha gari kuanzia 1993 hadi 1997 niliachana na gari za kawaida na kuhamia kwenye mabasi, na Chanika nzima wanashangaa maana kuna muda dereva, mara muda mwingine ni mwamuzi wa soka halafu wakija kwenye ujasiriamali wananikuta.

"Hata ukienda Mbezi mawakala wananijua kwa sababu basi ambalo nilikuwa naendesha lilipata ajali Michungwani 2004 na liliuwa watu watatu sasa baada ya kumaliza kesi ndiyo niliamua kuachana na magari.

"Lakini kwenye mpira nimechezesha makombe mbalimbali na nilikuwa ni mmoja kati ya mwamuzi niliyekuwa naogopwa na wachezaji wote.

"Sasa ukiangalia hayo ndiyo uhalisia wa maisha yangu sijagui kazi ingawa wapo baaadhi mabondia wenzangu wakubwa kama Dullah Mbabe na Mada Maugo huwa wanasema nimeweza vipi kuuza chips na kuku wa kuchoma wakiwa wao hawawezi kutokana na kuona aibu."