Prime
Mashabiki wamjibu Robertinho

KATIKA toleo la juzi Alhamisi, mchambuzi wetu Oscar Oscar aliandika uchambuzi uliokuwa na kichwa cha habari “Kwa Bocco... Robertinho aache kutudanganya”. Mashabiki kupitia namba yetu ya simu walituma maoni kwa mamia wakionyesha hisia tofauti lakini wengi wakitoa ya moyoni kwamba wanataka kuona mabadiliko kikosini. Kutokana na muitikio kuwa mkubwa tumechapisha baadhi ya meseji hizo;
Bocco awekwe benchi
KWA usajili wa Simba hii ya msimu huu hata timu akipewa Juma Mgunda na Seleman Matola tunachukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara, aache kumtumia John Bocco awatumie Moses Phiri na Jean Baleke, Simba inaweza kufunga mabao zaidi ya matano katika mechi moja.
Ajaba Ndogoro
Umri umemtupa
UMRI wa Bocco ni kweli umepita na Phiri anabaniwa sana.
Fredy wa Arusha
Uwezo umepungua
UKO sahihi uwezo wa Bocco umepungua.
Modestus, Kigamboni
Kocha aachane na Bocco
KOCHA anatuongopea na kuiabisha Simba wakati kuna wachezaji wengi kama Shabani Chilunda na Bocco na wengine ambao hawapi nafasi na wangeweza kuisaidia timu.
Mohamed, Morogoro
Umelenga, Bocco sio
MWANANGU umelenga penyewe Simba imekosa kusonga mbele kwa tatizo moja tu na la kocha kutowaanzisha wachezaji muhimu kwani mbele anatakiwa awe Clatous Chama, Phiri, Baleke, Saido Ntibanzonkiza, Kibu adui hawezi kuchomoka.
Kasongwa, Kyela Mbeya
Awe Baleke, Phiri
KWANINI mechi kubwa za kimataifa kocha anamwanzisha Bocco badala ya wachezaji wenye uwezo na ni vijana kama Baleke na Phiri na wanaweza kuleta matokeo ya haraka ila wanakuwa benchi.
Masanja, Simiyu
Bocco asubiri matokeo
OMBI langu kwa benchi la ufundi ni waanze sasa kuwatumia wakina Phiri na Baleke, Bocco wampumzishe apewe nafasi timu ikiwa na matokeo. Kila la Kheri kwenye mechi ya Ihefu.
Msamara, Ubungo
Simba tunawaheshimu
NAWAPONGEZA wachezaji wa Simba kwa kuheshimiana na kulinda walichopata.
Paul Tobiko, Kiteto
Huyu sio Bocco yule
NDUGU yangu pole na kazi ni kweli ndugu yetu kipenzi cha mashabiki Bocco sio yule wa Azam ila naomba aheshimiwe na kupewa maua yake na apewe hata timu ya watoto awakuze.
Andrew Mwangosi, Mbeya
Kocha awe makini
USHAURI kwa kocha wa Simba aangalie kwa upya maamuzi yake ya kumuanzisha Bocco kipindi cha kwanza. Jackson Elia, Arusha
Viongozi wanampanga Bocco
BOCCO kuwa nje inawezekana kuwa ni maamuzi ya viongozi kumtaka acheze maana kwa akili ya kawaida huwezi kumuacha Phiri nje na kumchezesha yeye.
Muhsin Mkami, Ilala
Inauma sana
ROHO inaniuma Phiri anawekwa benchi kocha atamfanya apoteze ubora wake wa kufunga.
Jamal Kihiyo
Msipoe-lewa tutaa-ndamana
KAMA kocha hataacha kum-chezesha Bocco sisi kama mashabiki tutaanda-mana mbona wapo wakina Chilunda na Phiri.
Abedy Gidion, Mwanza
Bocco abaki kwenye historia
KOCHA asiangalie historia ya nyuma ya Bocco kweli tunamheshimu lakini kwa sasa wamuache tunaumia kwa sababu uwezekano wa kumtoa Al Ahly tulikuwa nao kabisa.
Ruhondo
Phiri apewe nafasi
KWELI Bocco kachoka wapewe nafasi Baleke na Phiri.
Babu Mbishi, Ilala
Kocha anammaliza Phiri
NAUMIA sana kuona kocha anaua uwezo wa Phiri.
Miriam Karia
Robertinho ana shida
SIMBA kocha anashida maana anawanyima wengine nafasi na kuwapa wazee.
Said, Dar
Kocha anawaridhisha mabosi
KOCHA aache kusikiliza viongozi maana anacheza na akili zao ili kuwaridhisha ila kuna wachezaji wazuri zaidi ya Bocco.
Peter Kibula, Kimara
Akae benchi tu
BOCCO aanze benchi na Phiri aanze kocha akifanya hivyo tunatoboa.
Yusuf, Morogoro
Kocha asipobadilika, tutambadilisha
TIMU ikianza kupoteza kwaajili ya maamuzi yake mabaya basi ajue mashabiki watamzomea na kutomtaka tena hivyo asipobadilika watu watambadilikia.
Raymond Mwasemeleke, Tandika
Kocha anatudanganya
NAUNGANA nawe ulichapisha mawazo yako yakibebwa na kichwa cha Bocco, kocha aache kutudanganya na acheze wachezaji wengine.
Maswale, Msamvu Morogoro
Bocco ana kitu
KWENYE maoni kuhusu Bocco, sio kwamba asipangwe kucheza kabisa na haiwezekani akawa hana hata vichache vya manufaa wakati aliisaidia timu Algeria kuliko hata Shomari Kapombe na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’.
Msomaji wetu
Bocco hayuko fiti
NAUNGANA na wewe kwa asilimia 100 kocha anatudanganya anawaweka nje washambuliaji wa maana anamuweka Bocco ambae hayuko fiti.
Msomaji wetu
Shida ni Robertinho
USIWE mnazi, achambuliwe kwanza Kocha ndio mbovu kuliko huyo Bocco.
Msomaji wetu
Ribertinho awe mkweli
NAKUUNGA mkono kuhusu Bocco, kocha asitudanganye.
Msomaji wetu
Bocco anatupa presha
NAUNGA mkono juu ya Bocco kwani umri wake umeenda sasa na mashabiki tukiona amepangwa matumbo yanapata moto fuatilia hata vibandani au uwanjani utagundua hilo.
Msomaji wetu
Bocco apewe nyepesi
NIMEKUPENDA Oscar kwa uchambuzi wako, ila ningetamani kuona Bocco anapewa mechi nyepesi ili amalize safari ya soka kwa heshima maana kuna mashabiki wengine watasahau aliyoyafanya na kuanza kumzomea hali itakayoshusha thamani yake. Msomaji wetu
Asingemwanzisha Bocco
KOCHA alikosea kumuanzisha Bocco na Ahly kwani hesabu zake za kipindi cha kwanza ndicho kilichoifelisha Simba kukosa matokeo wala sio sababu ya ukubwa wa wapinzani waliokutana nao.
Msomaji wetu
Mashabiki tuna shida
MASHABIKI tuna matatizo tulimsakama Kibu Denis hadi akashuka uwezo hivyo hata Bocco tumuache ijapokuwa ni kweli kuwa kuna vitu vimepungua kwake.
Msomaji wetu
Onana, Bocco shida
KWELI Onana hana umakini bado na Bocco hamna kitu.
Msomaji wetu
Bocco waachie Phiri, Baleke
UNA mawazo mazuri ya kujenga Simba yetu amwachie Baleke na Phiri pia awaachie Onana na Saido pia umri umeenda aingizwe dakika 70.
Msomaji wetu
Viongozi Simba ndo shida
DIRISHA dogo Simba wamuache Bocco akafundishe vijana na viongozi wa Simba pia ni matatizo kwani inaonekana wana vipaumbele vyao. Msomaji wetu
Ni kweli eti
MIMI ni shabiki tangu 1970 na ulichosema kuhusu Bocco ni cha kweli. Msomaji wetu
Bocco awaachie wengine
BOCCO anawabania wengine nafasi kwani ameshapitwa na wakati. Msomaji wetu
Viongozi Simba wanazingua
NI swala la Viongozi kwani wanampangia kocha wachezaji wa kucheza maana kwa uzoefu tu wa kawaida huwezi kumchezesha Bocco kipindi cha kwanza.
Msomaji wetu
Kocha unazingua
KOCHA anatukera sana mashabiki kwani hawa wengine wanashida gani?
Msomaji wetu
Sio Bocco, hata Onana
KOCHA anatud anganya sio Bocco tu hata Onana huwezi kuwaingiza hao na kumuacha Phiri benchi huo ni uharibifu wa
timu Msomaji wetu