Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mamadou Lamine Camara ametufikirisha wengi kwa mengi

HISIA Pict

Muktasari:

  • Mamadou Lamine Camara akiwa na futi 6 na inchi 4 alikuwa amesimama katikati ya uwanja akiwatuliza viungo wa Simba ambao walikuwa wanahaha wasijue kitu cha kufanya uwanjani. Aliwatuliza kina Yusuf Kagoma, Jean Charles Ahoua, Fabrice Ngoma na mastaa wengine wa Simba.

KILOMITA 606 kutoka katika Jiji la Casablanca unafika Berkane na Jumamosi usiku kwa ajabu kabisa RS Berkane ilikuwa imesimamisha mnara katikati ya uwanja. Hapana, haukuwa mnara, alikuwa mchezaji.

Mamadou Lamine Camara akiwa na futi 6 na inchi 4 alikuwa amesimama katikati ya uwanja akiwatuliza viungo wa Simba ambao walikuwa wanahaha wasijue kitu cha kufanya uwanjani. Aliwatuliza kina Yusuf Kagoma, Jean Charles Ahoua, Fabrice Ngoma na mastaa wengine wa Simba.

Camara alinikumbusha Patrick Vieira, mmoja kati ya wachezaji ambao walifanya niipende zaidi Arsenal. Wakati huo, Vieira akiwasili Arsenal akiwa kama Camara, beki wa zamani wa Arsenal na nahodha wa timu hiyo wakati huo, Tony Adams alisikika akisema: “Kocha ametuletea mchezaji ana miguu kama mbu, lakini ana nguvu na akili zilizopitiliza.”

Nilimuona Camara katika ule wa Uwanja wa Manispaa ya Berkane nikamkumbuka Patrick Vieira. Mwembamba kama alivyo, akiwa ameenda hewani kama alivyo. Camara aliyafanya maisha ya Berkane kuwa rahisi usiku ule.

Achana na bao lake la kwanza nenda katika mambo mengine. Alifanya ‘tackling’ kwa usahihi. Alipiga pasi kwa usahihi na hakupoteza pasi yoyote. Sana sana nilikoshwa na pasi zake za mipira mirefu. Mmoja ulizaa bao la tatu la Berkane ambalo lilikataliwa na VAR. Alikuwa chini kisha juu. Alikuwa kila mahala akifanya kila jambo kwa usahihi.

HISI 01

Baadaye, kama ilivyo kwa Watanzania wengine, Camara alitufikirisha vitu vingi. Huwa tunakaa hapa na kujadili kwanini wachezaji wetu hawachezi nje kwa maana ya Ulaya. Kumbe kuna mchezaji kama Camara ambaye naamini nchi hii hakuna ambaye anamfikia, lakini anacheza Morocco.

Sawa, Morocco ina mpaka na Ulaya, lakini Ulaya ni Ulaya na Afrika ni Afrika. Camara anacheza soka lake la kulipwa Afrika. Kuna vijana ambao lazima wakate tamaa wakimuona Camara anacheza Afrika. Kama una ndoto ya kucheza Ulaya jifikirie kwanza. Kiwango chako cha mpira na nidhamu yako. Papo hapo kumbuka kwamba Camara ana vyote hivyo, lakini anacheza Afrika.

Ana pasipoti nzuri ambayo inaonyesha ana umri wa miaka 22, lakini bado yuko Afrika. Kitu hicho kinanishangaza pia kwake  mwenyewe Camara. Kwa miaka 22 na kwa kiwango kile kuendelea kuwa Afrika basi ni kupoteza muda. Sijui yeye na washauri wake wanafikiria nini.

Najua anatoka Afrika Magharibi na anajua anachofanya ila niliwahi kufanya mahojiano na Mbwana Samatta akiwa Genk akaniambia kwamba anajuta kwenda Ulaya akiwa na umri wa miaka 23. Camara ana miaka 22 na sijui anafikiria nini kuhusu hatima yake lakini wote tunashangaa namna ambavyo kiukweli amepoteza muda wake mpaka leo kuwa Afrika.

HISI 02

Ni kweli Berkane watakuwa wanamlipa pesa nzuri, lakini Ulaya ni Ulaya. Na ukimaliza kumtazama Camara pia watazame wachezaji wengi wa Berkane. Ni mafundi sana. Hata ustaadhi Yassine Lebhiri naye yupo Afrika.

Kijana yeyote ambaye anasoma makala hii ndio ajue namna gani inabidi aongeze bidii katika kazi yake. Ni kweli kuna mambo mengi yanaweza kuwepo katika kucheza Ulaya. Bahati, wakala mzuri, nidhamu bila ya kipaji na mengineyo. Lakini vijana waende kwanza katika fomu ya Camara. Wapambane.

Baada ya hapo kuna jambo jingine la kujadili. Namna ambavyo wenzetu wamebarikiwa. Camara ni kiungo wa Senegal ambaye aling’ara katika michuano ya Chan. Hata hivyo, kuna mambo mawili ya kutatanisha kuhusu yeye na timu ya taifa ya wakubwa.

Kuna taarifa mbili kutoka Wikipedia. Ya kwanza inasema ameichezea timu ya wakubwa mechi mbili. Ya pili ukichimba kwa ndani inakwambia hajawahi kuichezea timu ya wakubwa. Labda kama alihusishwa katika mechi za Olimpiki ambazo vijana wanachanganyika na watu wazima.

Hapo Camara anatufikirisha tena. Fikiria mchezaji kama yeye haitwi timu ya taifa ya Senegal wakati huohuo ana uhakika wa kuanza katika kikosi cha kwanza cha Taifa Stars kwa miaka 14 mfululizo kama hatapata majeraha. Jiulize, nafasi yake wanacheza kina nani hapo Senegal kama yeye wanamuona hawezi kuitwa au kuanza. Inafikirisha.

Taifa Stars inapofungwa na Senegal mashabiki huwa hawaaangalii ni namna gani wenzetu wametuacha mbali. Wanasahau mfano kama huu wa kina Camara na mwisho wa siku tunaishia kudai kwamba kina Samatta hawajitumi katika kikosi cha Taifa Stars.

Tunasahau kwamba hivi ndivyo viwango ambavyo wenzetu wamejiwekea. Kwa Kizungu huwa wanaita ‘levels’. Hapo ndio unaona ugumu wa Taifa Stars kufuzu Kombe la Dunia. Hapo ndio unaona kwamba hata michuano ya kufuzu Afcon ingekuwa inaendeshwa kwa miundo ya kizamani, basi bado Taifa Stars ingepata shida sana kufuzu.

HISI 03

Kitu kingine kinachotufikirisha kwa Camara ni kwa hawa jamaa zetu wa Kariakoo pamoja na ndugu zao - Azam. Kuna aina ya wachezaji bado hatujafikia kuwa nao. Camara ni mfano wake. fikiria analipwa kiasi gani pale Berkane na fikiria akiuzwa kwenda kwingineko atauzwa kiasi gani.

Nasikia Al Ahly wamekuwa wakimhitaji lakini watalazimika kuweka mezani zaidi ya Dola 3 milioni kwa ajili ya kuinasa saini yake. Ni klabu gani hapa kwetu inaweza kuweka mezani kiasi hicho cha pesa kwa ajili ya kuinasa saini yake?

Wote tunafahamu kwamba kama Berkane itachukua ubingwa wa Shirikisho ni kwa sababu inastahili. Ubora wao ni wa hali ya juu. Kama na sisi tunataka kufikia kiwango chao, basi tuanze kukusanya wachezaji wa aina yao. Kuanzia kwa wachezaji weusi walio nao hadi Waarabu kama Yassine kama tunaweza.