Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lamine Yamal anavyofukuzia rekodi ya kipekee Ballon d’Or

LAMINE Pict

Muktasari:

  • Hata hivyo, kama atabeba tuzo hiyo kwa umri wake wa miaka 17, jambo hilo litamfanya ashike namba ngapi kwa wachezaji wenye umri mdogo kuwahi kushinda tuzo hiyo ya ubora duniani.

BARCELONA, HISPANIA: FUNDI wa boli na kinda wa Barcelona, Lamine Yamal amekuwa akitajwa kama mmoja wa wachezaji wanaopewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo ya Ballon d’Or mwaka huu wa 2025.

Hata hivyo, kama atabeba tuzo hiyo kwa umri wake wa miaka 17, jambo hilo litamfanya ashike namba ngapi kwa wachezaji wenye umri mdogo kuwahi kushinda tuzo hiyo ya ubora duniani.

Wachezaji kama Johan Cruyff, Marco van Basten, Eusebio na Cristiano Ronaldo walibeba tuzo hiyo kabla ya kufikisha umri wa miaka 25, lakini bado hawapo kwenye orodha ya wachezaji wenye umri mdogo zaidi kushinda tuzo hiyo ya ubora. Tangu tuzo ya Ballon d’Or ilipoanzishwa kwa mara ya kwanza 1956, hii hapa orodha ya wachezaji wenye umri mdogo waliowahi kushinda tuzo hiyo kwa wakati huo.

LAM 01

5. Oleg Blokhin – miaka 23, mwezi na siku 25

Blokhin alishinda tuzo hiyo mwaka 1975, akiwashinda kwenye kinyang'anyiro Franz Beckenbauer na Johan Cruyff waliomaliza nafasi ya pili na tatu mtawalia. Fowadi huyo kwa kipindi hicho alikuwa akikipiga Dynamo Kyiv wakati huo anashinda tuzo hiyo na alishinda ubingwa wa Soviet Top League, UEFA Cup Winners Cup na UEFA Super Cup ndani ya mwaka huo. Alishinda tuzo hiyo alipokuwa na umri wa miaka 25, mwezi 1 na siku 25 – alikuwa mdogo kwa miezi chache sana na kipindi Cristiano Ronaldo aliposhinda Ballon d’Or.

LAM 02

4. George Best – miaka 22, miezi 7 na siku 2

Aliposhinda Ballon d’Or mwaka 1968, Best alikuwa mchezaji kijana zaidi kushinda tuzo hiyo kwa wakati huo  – rekodi ambayo ilidumu kwa karibu miaka 30. Winga huyo wa Manchester United alikuwa hazuiliki kwa kipindi hicho alipokuwa kwenye ubora wake na kufanikiwa kushinda tuzo hiyo. Wakati Best anashinda tuzo hiyo alikuwa na umri wa miaka 22, miezi saba na siku mbili.

LAM 03

3. Lionel Messi – miaka 22, miezi 5 na siku 7

Supastaa wa dunia, Lionel Messi alishinda tuzo yake ya kwanza ya Ballon d’Or mwaka 2009 baada ya kusaidia Barcelona kushinda mataji yake matatu makubwa ndani ya msimu mmoja. Baada ya kushinda tuzo hiyo, Messi alisema hakuwa anatarajia kabisa kuibuka na ushindi kwa mwaka huo licha ya timu yake ya Barcelona ilibeba mataji yote matatu makubwa iliyoshindania mwaka huo. Kwa kipindi hicho alipoweka rekodi hiyo ya kuwa mchezaji wa tatu mwenye umri mdogo kushinda Ballon d’Or, Messi pia anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji wa pili kwenye umri mkubwa kushinda tuzo hiyo, alipobeba na miaka 36.

Mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kubeba Ballon d'Or ni Stanley Matthews, miaka 41.

LAM 04

2. Michael Owen – miaka 22 na siku 4

Wakati anashinda tuzo ya Ballon d’Or mwaka 2001, staa wa England, Michael Owen aliweka rekodi ya kuwa mchezaji namba mbili mwenye umri mdogo zaidi kushinda tuzo hiyo. Akicheza chini ya Kocha Gerard Houiller, straika huyo alikuwa balaa kubwa uwanjani kwenye msimu wa 2000-01 na alifunga mabao 24 na kushinda mataji ya Kombe la FA, Kombe la Ligi, Ngao ya Jamii, Super Cup na Kombe la UEFA.

Owen alisema hakuwa anaamini kabisa kwa mara ya kwanza aliposikia taarifa hizo kwamba ni yeye ndiye aliyeshinda tuzo hiyo ya ubora kabisa duniani.

LAM 05

1. Ronaldo Nazario – miaka 21, miezi 3 na siku 5

George Best ndiye aliyekuwa anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kushinda Ballon d’Or, rekodi ambayo ilidumu kwa zaidi ya miaka 29 hadi hapo, straika wa Kibrazili, Ronaldo alipoibukia mwaka 1997.

Baada ya kumaliza nafasi ya pili mbele ya Matthias Sammer mwaka 1996, straika huyo wa Kibrazili huyo alishinda tuzo ya Ballon d'Or mwaka 1997, alipovuna pointi 154 mbele ya Predrag Mijatovic, aliyeshika nafasi ya pili. Katika michuano yote katika msimu wa 1996-97, Ronaldo alifunga mabao 47 katika mechi 49 kipindi hicho akiichezea Barcelona kabla ya kutimkia zake Inter Milan.

Tangu wakati huo, Ronaldo ndiye anayeendelea kushikilia rekodi ya kushinda Ballon d’Or akiwa na umri mdogo zaidi, kitu ambacho Yamal anaweza kukivunja mwaka huu.