Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maajabu ya Maxi Nzengeli Yanga

Muktasari:

  • Ukiangalia mara nyingi mechi za Yanga zinapochezwa, watatajwa zaidi wachezaji kama Stephane Aziz Ki na Pacome Zouzoua, hiyo ilikuwa msimu uliopita, lakini msimu huu majina ya Prince Dube na Clatous Chama nayo yameongezeka kwenye chati hiyo.

KATIKA timu kuna wachezaji wana nyota ya kuonekana na wengi pindi mechi zinapochezwa, lakini wengine hawana vitu hivyo, ukiona wanatajwa basi ni kwa uchache sana.

Ukiangalia mara nyingi mechi za Yanga zinapochezwa, watatajwa zaidi wachezaji kama Stephane Aziz Ki na Pacome Zouzoua, hiyo ilikuwa msimu uliopita, lakini msimu huu majina ya Prince Dube na Clatous Chama nayo yameongezeka kwenye chati hiyo.

Kutajwa kwa wachezaji hao kunatokana na kile wanachokifanya uwanjani, kama sio kufunga basi wamehusika katika kupatikana kwa mabao.

Licha ya kwamba wengine nao wanaweza kufanya kama hivyo, lakini kutajwa kwao inaweza kuishia ndani ya mchezo pekee, baada ya hapo ni kama hakuna kilichotokea.

Maxi Mpia Nzengeli, ni miongoni mwa wachezaji wachache wa Yanga wasiotajwa sana, lakini ukimuangalia kwa jicho la tatu anafanya kazi kubwa kikosini hapo kuliko mastaa wote.

Kichambuzi anaonekana mtulivu, anayetumia akili kubwa kupenya ngome ya adui. Anatajwa kama shujaa asiyeimbwa na staa mwenye muendelezo wa kiwango chake muda wote ndani ya dakika 90 msimu kwa msimu. Anatengeneza na kufunga.

Nyota huyo ambaye huu ni msimu wake wa pili ndani ya Yanga, ameonekana kuanza vizuri akiendeleza kile alichokifanya msimu uliopita alipojiunga na timu hiyo akitokea AS Maniema ya kwao DR Congo.

Mzaliwa huyo wa Mji wa Mushie nchini DR Congo, ana maajabu yake ndani ya uwanja ambayo ukiwa unaangalia mechi unaweza usiyaone haraka mpaka utakapokuwa makini kumfuatilia.


AMEUFUNGUA MSIMU

Msimu huu wa 2024/25, unaweza kusema Maxi ndiye ameufungua kwa upande wa Yanga kutokana na kile alichokifanya mpaka sasa.

Yanga ikiwa tayari imecheza mechi tano za kimashindano, mbili Ngao ya Jamii, mbili zingine Ligi ya Mabingwa Afrika na moja Ligi Kuu Bara, Maxi amefanikiwa kufunga mabao mawili ambayo yote unaweza kusema ni ya kufungua msimu ndani ya kikosi hicho.

Wakati wa mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii, bao lake pekee lilitosha kuipa Yanga ushindi wa 1-0 dhidi ya Simba, wakaenda fainali kuchukua ubingwa mbele ya Azam.

Maxi bao lake hilo lilikuwa ni la kwanza kufungwa ndani ya kikosi cha Yanga kwa msimu huu 2024/25 katika mechi za kimashindano. Achana na zile za pre-season.

Licha ya kwamba hakufunga katika zile mechi mbili za kimataifa dhidi ya Vital’O, lakini Maxi amekuja tena kufungua msimu wa Yanga ndani ya ligi kuu kwa kufunga bao la kwanza waliposhinda 2-0 dhidi ya Kagera Sugar.

Anakuwa miongoni mwa wachezaji wa Yanga kutoka DR Congo waliofanikiwa kufunga mabao ya kwanza ya msimu ndani ya ligi kwa misimu ya karibuni baada ya Heritier Makambo aliyefanya hivyo msimu wa 2018/19 dhidi ya Mtibwa Sugar na Fiston Mayele msimu wa 2022/23 dhidi ya Polisi Tanzania.


KIPENZI CHA KOCHA

Wakati mashabiki hawamuimbi sana, lakini ukifuatilia namna Kocha Miguel Gamondi anavyoipanga timu yake utabaini kwamba Maxi ni kipenzi cha kocha.

Hiyo inatokana na kwamba, kwenye nafasi yake ya kiungo mshambuliaji, msimu huu katika mechi tano za kimashindano kikosi cha kwanza ameanza mara nne, moja akikaa benchi ilikuwa dhidi ya Vital’O ambayo Yanga ilishinda 6-0.

Kukaa kwake benchi katika mechi hiyo kunatokana na kazi kubwa iliyofanyika mechi ya kwanza ambapo alianza waliposhinda 4-0, hivyo Gamondi alihitaji kumpa muda kidogo wa kusubiri mchezo wa kwanza wa ligi kwani ndiyo injini yake.


YUPO KAMA HAYUPO

Wakati mechi ikiwa inaendelea unaweza kusema Maxi hayupo uwanjani, lakini amekuwa msaada mkubwa kwa timu hiyo kuziba mianya ya ushambuliaji kwa wapinzani.

Uwezo wake mkubwa wa kucheza maeneo mengi ya uwanja ndiyo kunambeba zaidi katika hilo kwani anaitumia vizuri sana kasi aliyonayo inayomfanya kufika kwa haraka maeneo yenye hatari.


UWEZO WA KUKABA

Maxi ana uwezo mkubwa wa kukaba, hali hiyo inamfanya Kocha Gamondi kumtumia katika mifumo yake mbalimbali hasa ule wa 3-5-2.

Katika mchezo wa juzi Alhamisi dhidi ya Kagera Sugar, Yanga ilimkosa beki wake wa kulia Yao Kouassi ambaye ni majeruhi, Gamondi akabadili mfumo na kutumia mabeki watatu nyuma ambao ni Dickson Job, Bakari Mwamnyeto na Ibrahim Bacca.

Chadrack Boka ambaye naye ni beki akicheza kushoto, alipewa majukumu ya kuwa ‘wing back’ kama ilivyo kwa Maxi aliyekuwa upande wa kulia na kuifanya kazi vizuri.

Kitu hicho ndicho kinambeba Maxi kwani amekuwa akitumika katika mifumo mingi ndani ya Yanga tangu msimu uliopita, wakati mwingine anachezeshwa kabisa beki wa kulia ikihitajika kufanyika hivyo.


KUSHAMBULIA YUMO

Ukiachana na kukaba kazi ambayo pengine ni ngeni kwa mawinga wengi, pia Maxi ni mzuri katika kufungua. Anapopata nafasi akiwa karibu na goli la wapinzani, ni nadra sana kushindwa kufungua.

Angalia kilichotokea dhidi ya Simba, alifunga bao ambalo alikuwa kwenye sehemu ngumu, kipa Moussa Camara hakufanikiwa kumzuia.

Yanga wakiwa wanashambulia, ni nadra sana kumkosa Maxi akiwa eneo la wapinzani, mara nyingi anautanua uwanja kwa kuwavuta wapinzani na kwa uharaka sana anaingia ndani kuongeza nguvu.

Simba walikutana na balaa hilo kwani bao alilowafunga katika Ngao ya Jamii, alianza kuutanua uwanja akipigiana pasi na Duke Abuya, kisha akaingia ndani kucheza ‘one two’ na Pacome Zouzoua, mabeki wakiwa bize kumkaba Prince Dube, Maxi akapata mwanya kuachia shuti kali lililopita katikati ya miguu ya Kipa Camara, nyavu zikatikisika.


ANAONGEA KWA VITENDO

Huku watu wakiwa hawamtaji sana, lakini yeye ameamua kuongea kwa vitendo kwani msimu uliopita ambao ulikuwa wa kwanza kwake, alifanikiwa kushuka nafasi ya pili kwa wachezaji wenye mabao mengi ndani ya kikosi cha Yanga katika Ligi Kuu Bara.

Maxi ambaye kiuhalisia ni winga, alifunga mabao 11, akizidiwa 10 na kinara Stephane Aziz Ki.

Pia winga huyo msimu uliopita katika mechi ya hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Asas Djibout ikiwa mechi hiyo imepewa jina la Maxi Day, alifanya balaa kubwa.

Yanga ilishinda 5-1, huku Maxi mwenye siku yake akaweka kambani chuma mbili, bao la kwanza la mchezo na la mwisho.


SIMBA WANAMJUA VIZURI

Katika misimu mawili sasa ndani ya Yanga, mashabiki wa Simba wanamjua Maxi vizuri sana kutokana na kuwaumiza walipokutana uwanjani.

Msimu uliopita wakati Yanga ikishinda 5-1 dhidi ya Simba, Maxi alifunga mabao mawili, kisha msimu huu kwenye Ngao ya Jamii, akafunga bao pekee la ushindi, hivyo jumla ya mara nne walizokutana zikiwa mechi mbili za Ngao ya Jamii msimu uliopita na huu kisha mbili za Ligi Kuu Bara, amefanikiwa kufunga mabao matatu.


MSIKIE MWENYEWE

“Mimi kitu muhimu kwangu ni kazi, inapotokea sijacheza mechi vizuri nikirudi Nyumbani nafanya mazoezi nikiamini Kesho nitaenda kufanya vizuri.  Nilichojifunza ni kufanya kazi kisha kukaa kimya,” amesema Maxi.