Lolote litatokea Simba, Yanga

ZIMESALIA saa chache kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa rasmi saa 5:59 usiku na unaambiwa lolote linaweza kutokea ndani ya ya muda huo kwa Simba na Yanga wakati mabosi wa klabu hizo wakihaha kukamilisha dili za kushusha nyota wapya wa kuimarisha vikosi vya timu hizo.
Dirisha hilo lililofunguliwa tangu Desemba 16 litafungwa usiku wa leo, huku ikielezwa Yanga na Simba pamoja na klabu nyingine zikiwamo Azam wakimalizana na nyota walionao ili kupisha majembe mapya ambayo walikuwa wakiwapigia hesabu ili kufunga hesabu za usajili.
Simba na Yanga kila moja zinahaha kusaka mastraika wa kutatua tatizo la upatikanaji mabao hasa kwa kukabiliwa na mechi ngumu mbili za mwisho kwa kila mmoja katika makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ili kuvuka kwenda robo fainali na makocha wa timu hizo wanasikilizia tu kwa sasa.
Licha ya kuwa ngumu kupatikana kwa majina ya mastaa waliopo kwenye rada ya timu hizo kulingana na mapendekezo ya makocha Abdelhak Benchikha na Miguel Gamondi, Mwanaspoti litaendelea kuwahabarisha kila dili zitakazokamilika kupitia mitandao yetu ya kijamii kabla dirisha halijafungwa.
Mabosi wa klabu za Ligi Kuu vikiwemo vigogo hivyo wanapambana kuwatoa baadhi ya mastaa wao kwa mkopo au kuachana nao jumla ili kutoa nafasi kwa majembe mapya, ambao baadhi yao tayari wapo vikosini, kwani Simba, Yanga na Azam zimeshatambulisha wachezaji kadhaa hivi karibuni.
Yanga tayari imemshusha Mghana Augustine Okrah na Shekhan Ibrahim kutoka JKU, huku Simba ikimtambulisha viungo watatu, akiwamo Msenegali Babacar Sarr na wazawa Saleh Masoud Karabaka kutoka JKU na Ladack Chasambi (Mtibwa Sugar), huku Edwin Balua kutoka Tanzania Prisons ikielezwa dili limetiki na wanasubiri kumwachia leo hii, sambamba na kukamilisha dili la wengine.
Azam yenyewe imeshatangaza majembe matatu mapya ya kigeni akiwamo kipa Mohamed Mustafa kutoka El Merrikh ya Sudan na Wacolombia wawili, Franklin Navarro naYeison Fuentes, huku ikielezwa walikuwa mbioni kuongeza kifaa kingine kipya kabla dirisha halijafungwa usiku wa leo.
Wakati tukisubiri kuwaletea kila kinachoendelea kwenye dakika hizi za mwisho kabla ya dirisha hilo la usajili kufungwa usiku, hapa chini ni dili zilizokamilika kwa klabu zote za Ligi Kuu Bara na wale wachezaji waliondoka kwenye timu hizo.
AZAM FC
Walioingia
Franklin Navarro (Cortulua FC), Mohamed Mustafa (Al-Merrikh), Yeison Fuentes (Leones FC).
Waliotoka
Idris Mbombo (Nkana FC).
YANGA
Walioingia
Shekhan Ibrahim Khamis (JKU), Augustine Okrah (Bechem United).
Waliotoka
Crispin Ngushi (Coastal Union), Denis Nkane (Dodoma Jiji).
SIMBA
Walioingia
Saleh Karabaka (JKU), Babacar Sarr (Huru), Ladaki Chasambi (Mtibwa Sugar), Edwin Balua (TZ Prisons).
Waliotoka
Nassoro Kapama, Jimmyson Mwanuke (Mtibwa Sugar), Shaaban Idd Chilunda (KMC), Hamis Abdallah (haijafahamika), Ahmed Feruz (haijafahamika), Mohamed Mussa (haijafahamika).
COASTAL UNION
Walioingia
Salum Aiyee (Mbuni), Crispin Ngushi (Yanga).
Waliotoka
Justin Ndikumana (Mtibwa Sugar), Juma Mahadhi (haijafahamika), Fran Golubic (haijafahamika), Balama Mapinduzi (Mashujaa), Yakubu Abdullah (haijafahamika), Daud Mbweni (haijafahamika), Abdulswamad Kassim (haijafahamika), Konare Malienne (haijafahamika), Henock Mayala (haijafahamika).
DODOMA JIJI
Walioingia
Robinson Kamura (Kakamega Homeboyz), Apollo Otieno (KCB), Denis Nkane (Yanga).
Waliotoka
(Haijawekwa wazi).
TABORA UNITED
Walioingia
(Haijawekwa wazi).
Waliotoka
(Haijawekwa wazi).
NAMUNGO FC
Walioingia
(Haijawekwa wazi).
Waliotoka
Reliants Lusajo (Mashujaa), Shiza Kichuya (JKT TZ).
SINGIDA FG
Walioingia
(Haijawekwa wazi).
Waliotoka
Bruno Gomes, Marouf Tchakei, Kelvin Nashon,. Joash Onyango, Elvis Rupia na Abubakar Khomeny (wote wametua Singida Fountain Gate)
TANZANIA PRISONS
Walioingia
George Sangija, Tariq Simba (Geita Gold), Abdulkarim Segeja (Copco FC), Jacob Benedicto (Mbeya Kwanza), Feisal Mfuko (Majimaji), Ally Msengi (Moroka Swallows).
Waliotoka
Edwin Balua (Simba), Yusuph Mlipili (haijafahamika).
IHEFU
Walioingia
Manu Labota Bola (FC Lupopo), Bruno Gomes, Marouf Tchakei, Kevin Nashon . Joash Onyango, Elvis Rupia na Aboubakr Khomein (wote kutoka Singida Fountain Gate)
Waliotoka
Charles Ilanfya, Rashid Juma (Mtibwa Sugar), Nassor Saadun, Juma Nyosso (Geita Gold), Never Tigere (haijafahamika).
KMC
Walioingia
Abdallah Said ‘Lanso’ (Mlandege), Akram Muhina (KVZ), Shaaban Idd Chilunda (Simba).
Waliotoka
(Haijawekwa wazi).
JKT TANZANIA
Walioingia
Yacoub Suleiman Ali, Gamba Idd Matiko (JKU), Shiza Kichuya (Namungo FC).
Waliotoka
John Mwanda (Pamba FC).
GEITA GOLD
Walioingia
Ramadhan Kapera (Mbeya Kwanza), Nassor Saadun, Juma Nyosso (Ihefu), Erick Mwijage (West Armenia).
Waliotoka
George Sangija, Tariq Simba (TZ Prisons).
MTIBWA SUGAR
Walioingia
Justin Ndikumana (Coastal Union), Charles Ilanfya, Rashid Juma (Ihefu), Nassoro Kapama, Jimmyson Mwanuke (Simba), Laurent Alfred (Kagera Sugar).
Waliotoka
Ladaki Chasambi (Simba).
MASHUJAA FC
Walioingia
Nyenyezi Juma (Inter Star), Emmanuel Mtumbuka (Stand United), Balama Mapinduzi (Coastal Union), Abrahaman Mussa (Ruvu Shooting), Reliants Lusajo (Namungo), Ibrahim Ame (Huru), David Uromi (Moroka Swallows).
Waliotoka
Mohamed Hamis ‘Demba’ (Mbeya City).
KAGERA SUGAR
Walioingia
(Haijawekwa wazi).
Waliotoka
Laurent Alfred (Mtibwa Sugar).