Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kilichombeba Usyk kwa Joshua

Usyk ampa neema Anthony Joshua

ALFAJIRI ya kuamkia juziJumapili, ulimwengu wa masumbwi, ulishuhudia pambano kali la marudiano uzito wa juu (heavyweight), baina ya mabondia Oleksandr Usyk na Anthony Joshua.

Pambano hilo lilikua la marudiano baada ya lile lililofanyika mwaka jana, Septemba mjini London, Uingereza ambalo Usyk alimchapa Joshua kwa pointi za majaji wote watatu (unanimous decision).

Matokeo ya pambano la kwanza ndio yaliyoongeza msisimko zaidi wa pambano hili la marudiano, wengi wakitarajia kuona kama Joshua atalipiza kisasi na kurudisha mikanda yake ya IBF, WBA na WBO ukiachana na ule wa IBO ambao pia uliunganishwa baina yao, lakini ikawa tofauti na matarajio hayo.

Joshua, bondia Muingereza, licha ya kuajiri makocha wawili wapya kuelekea pambano hilo la pili, bado haikusaidia kulipiza kisasi mbele ya Usyk, aliyeshinda kwa mara nyingine na kutetea mikanda hiyo minne aliyoitoa kwa ajili ya nchi yake Ukraine.

Usyk alichanga vyema karata zake kuhakikisha haingii kwenye mtego wa Joshua. Majaji wawili waliompa Usyk ushindi huo mtawalia, wakimpa pointi 115-113 na 116-112. Jaji mmoja akampa ushindi Joshua kwa pointi 115-113.


KILICHOMFELISHA

Kushindwa kwa Joshua kwenye pambano hili kulitokana na kuweka matarajio makubwa zaidi kiasi cha kujipa presha ya kulazimisha kushinda kwa haraka, jambo ambalo lilikua kazi bure kwani mpinzani wake Usyk alishamsoma na kuweka zaidi umakini mwanzoni mwa pambano.

Umakini huo ulimsaidia zaidi Usyk ambaye alitunza nguvu na mikimbio yake bila kuchoka na alijipanga namna ya kumdhibiti na kushambulia kwa hesabu kulingana na raundi.


‘KO’ ILIKUA NGUMU

Kutokana na umakini aliouweka Usyk, ilimfanya akwepe jaribio kubwa ambalo Joshua alijipanga la kutaka kushinda kwa Knockout ‘KO’ hata kabla ya pambano alishakaririwa kutaka ushindi wa aina hiyo.

Ili kufanikisha jaribio hilo, Joshua alianza pambano kwa lengo hilo lakini bado hakufanikiwa kumuingiza kwenye mtego mpinzani wake Usyk, ambaye alianza kumuonyesha uhalisia wake kwenye raundi ya nne na kuendelea hadi raundi ya 10 ndipo akambadilikia na kuanza kumrushia ‘makonde’ mengi (combination) zilizomfikia Joshua.


PRESHA, UCHOVU

Presha ilikuwa kubwa zaidi kwa Joshua, kitendo cha kushindwa kwa lengo kubwa la kumpata Usyk kwenye ‘KO’, kilimtoa kwenye reli kiasi cha kudanganyika na mitego ya Usyk kufunguka ili aanze kushambulia, uchovu nao haukumuacha salama!


RAUNDI TATU ZA USYK

Hatimaye baada ya kumuingiza Joshua kwenye mtego wa kumfuata akiwa tayari amechoka na kufanya makosa ya kurusha ngumi bila uhakika wa kulenga, ushindi wa Usyk ulianza kujionesha wazi kabisa kwenye raundi tatu za mwisho, kuanzia ya 10 hadi ya 12.

Raundi hizo, Usyk ndipo alipofanikiwa zaidi kuandikisha pointi nyingi kwa kumpata Joshua ambaye alishachoka na aliingia kwenye njia ya kichapo hicho alichostahili. Baada ya kujitahidi kwenye raundi za mwanzo zilizompa angalau pointi kadhaa lakini sio kama alizoandikisha Usyk mwishoni.


REKODI KWA USYK

Oleksandr Usyk amejihakikishia ubingwa wa uzito wa juu duniani kwa kumshinda Joshua kama ilivyokuwa kwenye mkataba wa pambano baina yao, ambalo liliweka takwa la marudiano. Ameshinda na sasa ndiye bingwa wa dunia kwenye uzito wa juu akiwa na mikanda minne ya WBA, IBF, IBO na WBO huku akiweka rekodi ya kushinda mapambano yote 20 aliyopigana kwa ujumla bila kupoteza hata moja.


BADO TYSON FURY

Ushindi huo mbele ya Joshua, umempa jeuri Usyk ya kumtaka bondia mwingine Muingereza, Tyson Fury ambaye anashikilia mkanda mmoja uliobaki kwenye uzito wa juu duniani, WBC unaotolewa na kamisheni nyingine kwenye uzito huo, ambao sasa anautaka na anamtaka mwenye nao, Fury.

Usyk aliweka wazi kuwa, haitakua sawa kupigana tena na Joshua na anamtaka Tyson Fury.

Awali promota wa Fury, Bob Arum alikiri , bondia wake alikuwa anasubiri kwanza pambano hili la pili baina ya Usyk na Joshua ndipo atatangaza msimamo wake wa kustaafu jumla au kurudi ulingoni.

Mauricio Sulaiman, Rais wa WBC anasubiri pia msimamo rasmi wa Tyson Fury kupitia maandishi, ambapo ana hadi Agosti 26 kuthibitisha kama amestaafu au atarudi ulingoni.