Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kikipigwa hapa atapasuka mtu

Kapombe ni kidume kweli

IKITOKEA ikapigwa mechi kati ya wachezaji wazawa wazoefu na wanaokuja kwa kasi, inaweza ikawa ya kiufundi zaidi na ushindani wa aina yake.

Mwanaspoti linakuchambulia kikosi cha wazoefu na chipukizi wanaokipiga Ligi Kuu Bara, huku ndani yake kukiwepo funzo la namna baadhi yao walivyoweza kumudu na kiwango.

Kuna wazoefu na chipukizi wengi waliyopo Ligi Kuu na wanaochambuliwa ni baadhi yao.


KASEJA VS MSHERY

Kipa wa KMC, Juma Kaseja ana uzoefu wa kutosha na Ligi Kuu Bara, unaotoa somo mbele ya chipukizi, kujifunza jinsi ya kutunza viwango vyao.

Tangu aanze kucheza Ligi Kuu amefikisha miaka 22, alianza 2000-2003 akiwa na Moro United, 2003-2012 Simba, 2014/15 Yanga, 2015-2017 Mbeya City, 2017/18 Kagera Sugar na 2018-2022 KMC.

Umuhimu wa Kaseja kwenye timu zinazomsajili unatoa funzo kwa kipa wa Yanga, Abdultwalib Mshery na wengine wenye umri kama wake, kujifunza nidhamu ya mkongwe huyo, ili vipaji vyao viishi muda mrefu.


KAPOMBE VS NATHANIEL

Miaka 11 ya beki wa Simba, Shomari Kapombe kuwepo Ligi Kuu si haba, jambo linaloweza kutoa somo kwa wanaokuja nyuma yao, mfano namba mbili wa Ruvu Shooting, Nathaniel Chilambo na wengine wanaocheza nafasi hiyo.


LUHENDE VS MSINDO

Beki wa Kagera Sugar, David Luhende ni kati ya mabeki namba tatu wazoefu ligi kuu na bado wanadunda na kiwango cha juu, miongoni mwa wanaokuja nyuma yake ni Pascal Msindo wa Azam FC anayefanya vyema.


DAUD VS MWAIKENDA

Beki namba nne wa Mtibwa Sugar yupo kitambo kwenye ligi kuu. Dickson Daud na bado anakipiga, katika namba yake yupo Lusajo Mwaikenda wa Azam FC anayejifunza uzoefu.


YONDANI VS JOB

Beki wa Geita Gold , Kelvin Yondani ana miaka zaidi ya 16 ligi kuu na bado ana mpira mkubwa mguuni, katika nafasi hiyo kuna Dickson Job wa Yanga anayefanya vyema kwenye nafasi hiyo.


NYONI VS ABDULRAZACK

Nidhamu ya kiraka wa Simba, Erasto Nyoni ndiyo iliyomfanya adumu kwa kiwango zaidi ya miaka 10 kwenye Ligi Kuu, nafasi ya kiungo mkabaji yupo mchezaji wa Namungo FC Abdulrazack Hamza anayeitwa hadi Stars.

Nyoni aliwahi kuliambia Mwanaspoti kwamba “Nafurahi sana ninapoona wanakuja chipukizi wenye vipaji vikubwa, wanaoweza kulitumikia taifa letu.”


LYANGA VS TEPSI

Winga wa Geita Gold, Danny Lyanga ni kati waliyocheza muda mrefu ligi kuu, katika nafasi yake kunakuja chipukizi wengi akiwemo wa Azam FC, Tepsi Evance anayekuja kwa kasi na anaonyesha uwezo.


SURE BOY VS ANDAMBWILE

Kiungo wa Yanga, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ ni kati ya mastaa wenye uzoefu na Ligi Kuu kwa zaidi ya miaka 10, katika nafasi hiyo anaibuka nyota mwingine kutoka Mbeya City, Aziz Andambwile anafanya vizuri.


BOCCO VS SOPU

Japokuwa nahodha wa Simba, John Bocco hajafunga hadi sasa kwenye Ligi Kuu, anabebwa na rekodi ya mabao 142 aliyofunga ndani ya misimu 14, katika nafasi yake yupo Abdul Sopu wa Coastal Union anayesaka uzoefu.


CHOMBO VS PAUL

Mshambuliaji wa Biashara United, Ramadhan Chombo ‘Redondo’ ana miaka zaidi ya 10 Ligi Luu na amekuwa akionyesha kiwango kizuri, katika nafasi hiyo, yupo Oscar Paul wa Prisons, anayekuja kwa kasi.


NONGA VS NKANE

Straika wa Mbeya City, Paul Nonga ni kati ya wachezaji wazoefu ligi kuu na sasa wanakuja chipukizi wengine wanaofanya vyema kama Denis Nkane wa Yanga.

Kutokana na uwepo wa kikosi cha wakongwe na chipukizi kwenye ligi kuu, staa wa zamani wa Yanga, Fredy Mbuna anasema kinasaidia kuleta changamoto ya ushindani.

“Wakongwe watataka kulinda heshima yao, chipukizi nao wajitume kujenga majina yatakayoishi mbele ya wanaokuja nyuma yao, hilo litaibua ushinda mkali na wenye funzo baina yao.” anasema.

Hoja yake ilikwenda sambamba na ya beki wa zamani wa Simba, Athuman Kasongo aliyesema chipukizi wanapata somo la kujua wakongwe wana nidhamu ndiyo maana bado wapo kwenye gemu. “Wajitathimini kama wataweza kuwa na kiwango kama cha wakongwe wanaocheza nao hadi sasa, wakiwa na maswali hayo watajifunza kujitunza.”