Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Geita Gold walitaka bao la Manula

Geita Gold walitaka bao la Manula

MBEYA. STRAIKA wa Geita Gold, George Mpole amesikiliza kwa umakini gumzo kuhusu bao lake lililokataliwa dhidi ya Simba na kutamka wazi kuwa atafunga mengine na ndoto yake msimu huu ni kusaka rekodi.

Katika mchezo wa Simba na Geita Gold kulizuka gumzo baada ya bao la Mpole alilofunga kukataliwa na mwamuzi, Martin Sanya akidai kabla ya mfungaji kupiga kichwa alimsukuma Shomari Kapombe na Simba ilishinda mabao 2-1 Uwanja wa Mkapa.

Maamuzi hayo yalionekana kuwa gumzo kwa mashabiki na wadau wa soka, huku wakitofautiana mtazamo ambapo baadhi wakisema lilikuwa bao sahihi, wengine wakisema halikuwa sahihi.

Hata hivyo Mwanaspoti imezungumza na nyota huyo wa zamani wa Mbeya City, Polisi Tanzania na Biashara United na kueleza uhalisia, malengo na ndoto zake katika soka.

Anasema yeye anafahamu kwamba lilikuwa ni bao sahihi kwani hata kama alimgusa Kapombe ila haikuwa ni kwenye mazingira ya kufunga bao hilo.

Anasema alitumia mbinu zake ikiwa ni kumzidi Kapombe urefu baada ya kuusoma mpira ulivyokuwa juu na kumuacha hatua moja mpinzani wake na kujitwisha mpira huo hadi wavuni.

Mchezaji huyo anasema pamoja na kwamba lilikataliwa lakini yeye anaamini lilikuwa bao sahihi, hivyo kama refa aliamua alivyotaka hana shida na atafunga mengine kwani ligi haijaisha.

“Lilikuwa lilikuwa bao sahihi kabisa, kwa sababu kabla ya mpira nilikuwa sambamba na Kapombe lakini ile inapigwa krosi nilimuacha hatua moja nikaona mpira unakuja juu na mimi ni mrefu kuliko mpinzani. anasema

“Kwahiyo ile unakaribia tayari nilikuwa nimeshamuacha Kapombe na kuupokea mpira kichwani ukazama golini, mimi ni straika na jukumu langu ni kufunga mabao,” anasema Mpole.

Straika huyo anaeleza kuwa ikiwa ni msimu wake wa nne anacheza Ligi Kuu, lakini bado anaumizwa na kutofunga mabao kwani hajawahi kuzidi mawili.

Anasema kuwa msimu huu anauona kama wa neema kwani tayari ameshafunga mabao matatu jambo ambalo linampa nguvu katika kusaka heshima ya ufungaji bora.

“Kwa misimu mitatu iliyopita tangu nianze kucheza Ligi Kuu sijawahi kuzidi mabao mawili, ila msimu huu naona nimefikisha matatu, hivyo inanipa nguvu kusaka ndoto yanguî anasema Mpole.

Anaeleza hatua ya benchi la ufundi kumuamini kumpa namba, inamfanya kuwa na matumaini kufikia malengo huku akifafanua kuwa nidhamu ndio kila kitu kwake.

Anaeleza kwamba kwa sasa anajiona mwenye mafanikio kwani katika mechi saba alizocheza dakika 90, hajaoneshwa kadi ya njano na kwamba mafanikio yake ni ya timu kwa ujumla.

“Nidhamu ndio kila kitu, lakini mafanikio yangu ndio ya timu kwa ujumla ukizingatia ndio msimu wake wa kwanza Ligi Kuu, napambana kuona msimu huu nafika mbali,” anasema Mpole.