Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dodoma Jiji v Simba Ilikuwa kama vita Jamhuri

Muktasari:

BAADA ya kuandamwa na kutofunga kwenye mechi tatu mfululizo msimu huu, hatimaye Simba walifungua akaunti ya mabao kwenye mchezo uliopita dhidi ya Dodoma Jiji uliochezwa Uwanja wa Jamhuri.

BAADA ya kuandamwa na kutofunga kwenye mechi tatu mfululizo msimu huu, hatimaye Simba walifungua akaunti ya mabao kwenye mchezo uliopita dhidi ya Dodoma Jiji uliochezwa Uwanja wa Jamhuri.

Baada ya mechi tatu, bao la kwanza la msimu huu kwa Simba lilifungwa na straika Meddie Kagere aliyeingia kutokea benchi kuifungia timu yake bao pekee la kwenye mchezo uliokuwa mgumu uwanjani.

Kagere alifunga bao hilo dakika ya 69 ya mchezo akipokea pasi ya kichwa kutoka kwa Chris Mugalu ambaye aliuwahi mpira mrefu uliodunda ukitokea kwa kipa Aishi Manula aliyepiga mpira mrefu.

Ushindi huo ulikuwa muhimu kwa Simba ambao sasa wameshusha presha kwa kuanza msimu vibaya walipofungwa mechi mbili za awali na TP Mazembe - mchezo maalumu wa Simba Day na ule waliofungwa na Yanga bao 1-0 kwenye Ngao ya Jamii.

Mwanaspoti lililokuwepo Uwanja wa Jamhuri lilishuhudia kila kitu na hayaa ni miongoni mwa yale yaliyojiri kwa ukubwa kuelekea mchezo huo na mchezo wenyewe pamoja na baada ya kumalizika kwa mtanange.

UGUMU WA MECHI

Mchezo huo ulitawaliwa na ubabe kama sio undava tangu mwanzo kabisa ambapo kila timu ilionekana kukamia husasan Dodoma Jiji ambao walionekana kutumia nguvu zaidi kuwakabili Simba.

Ugumu huo ndio ulisababisha kuumia kwa wachezaji watatu wa Simba kina Ousmane Sakho, Kennedy Juma na Tadeo Lwanga ambao walishindwa kuendelea na mchezo na kuwalazimu makocha wa Simba wafanye mabadiliko yasiyo ya kiufundi.

Simba iliingiza wachezaji wanne ambao ni John Bocco, Hennock Inonga, Rally Bwalya na Meddie Kagere waliongia kwa awamu tatu tofauti.


PRESHA KUBWA

Kila timu ilionekana kuwa na presha kutokana na sababu kubwa mbili - ambazo ni kuhakikisha zinafanikiwa kuibuka na ushindi kwenye mchezo kutokana na namna kila zilivyocheza na pia presha kutoka nje kwa mashabiki na wadau waliokuwa wakitaka ushindi kwa hali.

Wenyeji Dodoma Jiji walikuwa na presha ya kutaka kuibuka na ushindi wakitambua kuna ahadi ambayo ilitajwa wangepata endapo wangeshinda au kutoka sare na Simba.

Upande wa Simba wao presha ilitokana na kutopata matokeo kwenye mechi zote tatu zilizopita, jambo lililosababisha waingie kusaka ushindi mapema ili wajihakikishie matokeo na kufuta nuksi ya kutofunga mechi zilizotangulia.


KAGERE NA KISMATI

Katika kuonyesha kuwa na bahati nzuri na Uwanja wa Jamhuri, mshambuliaji Meddie Kagere anaendelea kuwa na kawaida ya kufunga bao kwenye uwanja huo kutokana na msimu uliopita pia kufunga bao katika kila mchezo aliocheza.

Kagere, msimu uliopita, alifunga mabao matatu kwenye Uwanja wa Jamhuri yakiwemo mawili aliyofunga dhidi ya JKT Tanzania kwenye ushindi wa mabao 4-0, huku pia akifunga bao moja kwenye ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji.

Bahati hiyo aliiendeleza mbele ya Dodoma Jiji - tena kwenye mchezo wa ligi msimu huu alipoingia na kuifungia bao pekee juzi ikiwa ni bao lake la nne anafunga kwenye mechi tatu alizocheza kwenye Uwanja wa Jamhuri.


N-CARD BADO TATIZO

Tangu mchezo wa Dodoma Jiji dhidi ya Ruvu Shooting uliochezwa Septemba 28, hadi ule wa juzi Dodoma Jiji dhidi ya Simba uliendeleza changamoto kubwa ya kuingia uwanjani kupitia mfumo wa kadi maalumu (N-Card) ambao haukuwepo msimu uliopita.

Mfumo huo ambao unatumika kwenye mechi za Dar es Salaam, kwa Dodoma ulikuwa na changamoto kwa wapenzi wengi wa soka ambao hawajawahi kuutumia, hali iliyochangia baadhi ya mashabiki kushindwa kukata tiketi na kuingia uwanjani.

Baadhi ya mashabiki walisikika wakilalamikia mfumo huo kuwa tatizo kwao kuutumia jambo ambalo liliwafanya baadhi yao kuamua kuondoka kwenda kutazama kwenye runinga.


KADI NYEKUNDU

Dakika ya 44 kipindi cha kwanza kilishuhudia kadi nyekundu kutoka kwa mwamuzi Joackim Akamba wa Iringa aliyompa mshambuliaji Anuary Jabir wa Dodoma Jiji kwa kumpiga kiwiko beki wa Simba, Kennedy Juma.

Kadi hiyo ililalamikiwa na wachezaji wa Dodoma Jiji pamoja na benchi la ufundi la timu hiyo chini ya kocha Mbwana Makata, na hata mashabiki na viongozi wa timu baada ya mchezo.

Timu hiyo iliamini kwamba haikutakiwa kuwa kadi nyekundu kama alivyoamua mwamuzi, jambo ambalo kwao walitaja kuwa ni sababu ya timu kufungwa.

Vyovyote ilivyokuwa, mchezo huo ulikuwa na hamasa ya aina yake kutoka kwa mashabiki na wadau, hivyo ulichezwa kwa presa ya aina yake.