Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Clara Luvanga mechi moja tu yampa namba Ulaya

ILE ndoto aliyokuwa akiiota mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Serengeti Girls U-17, Clara Luvanga imetimia.
Clara aliwahi kufanya mahojiano na Mwanaspoti na kusema anatamani kucheza soka la kulipwa Ulaya hususan, England ambapo kwa sasa binti huyo amefanikiwa kujiunga na Klabu ya Dux Logrono ya Hispania kwa mkataba wa miaka mitatu.
Timu hiyo inashiriki Ligi ya Wanawake Daraja la Kwanza ambayo ni ya pili kwa ukubwa inayojulikana kama Reto Iberdrolana ikiwa chini ya Kocha Gerardo Garca Lean, ambaye ni beki wa zamani wa Villarreal, Valencia na Real Socieadad pamoja na timu C na B za Real Madrid.
Clara ambaye asili yake ni Mhehe wa Iringa alianza soka katika timu za mitaani kabla hajajiunga na Mapinduzi Queens iliyokuwa ikishiriki Ligi Daraja la Kwanza hadi kufanikiwa kuipandisha Ligi Kuu na baada ya msimu mmoja akajiunga na Yanga Princess.
Mwanaspoti limekufanya mahojiano na Clara kuhusiana na maisha nje ya Bongo.

MAISHA MAPYA
Anasema kila hatua anayopiga lazima anakutana na changamoto lakini hazimkatishi tamaa.
Straika huyo anasema anayafurahia maisha ya Hispania japo ni mapema kusema.
Anasema tangu amefika anapata ushirikiano na wachezaji wenzake pamoja na benchi la ufundi kwani tayari amepata rafiki wa kuzungumza naye.
“Changamoto hazikosekani kila sehemu utazipitia ili ukomae muhimu tangu nimetua hapa nashukuru ninapewa ushirikiano na wenzangu pamoja na benchi la ufundi nayafurahia maisha japo nina muda mchache tangu nimewasili,” alisema Clara ambaye ameanza kuzoea hali ya hewa ya nchi hiyo pamoja na vyakula.

MECHI MECHI TU
Mshambuliaji huyo anasema baada ya kucheza mechi ya kwanza ya Ligi dhidi ya UD Logronos ambayo walishinda 7-0 inampa ramani ya ligi nchini humo ipoje.
Katika ushindi huo, Clara amehusika na bao moja ambalo alifunga akitokea benchi dakika ya 67 na kumfanya kocha wa timu kuendelea kumwanini na kumpa dakika nyingi za kucheza.
Clara anasema katika kikosi hicho kina ushindani wa hali ya juu jambo linalomfanya aendelee kupambania namba.
“Mechi ya kwanza imenipa taswira kunifanya nipambane kwani katika kikosi chetu kuna wachezaji wengi wazuri,” anasema Clara.

LUGHA CHANGAMOTO
Anataja changamoto kwake ni lugha ya Kihispania ambacho kwake ni kigeni. Anasema anapitia shida hasa wakati wa kuzungumza lakini kwa lugha ya mpira akiwa mazoezini anaelewa vizuri.
“Napata shida sana hasa wakati wa kuzungumzia mambo mengine ila sasa naanza kuwaelewa lakini nikiwa mazoezini na hata kwenye mechi naelewana vizuri kwasababu wanatumia lugha ya mpira,” alisema Clara.

HISPANIA NI NJIA
Anasema bado ndoto yake kubwa ni kucheza England lakini alipo sasa itakuwa njia ya kufika anapotaka.
England. Hapa nilipo sio mbali na ninapokwenda kikubwa kumuomba Mungu tu,” anasema binti huyo.

WAMPA SHAVU
Anasema kuna watu wengi ambao wako nyuma yake wamemfanya aonekane na kusajiliwa nje. Anamtaja Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said na makamu wake, Arafat Haji kumruhusu aende kutafuta maisha sehemu nyingine.
Kocha wa zamani wa Yanga Princess, Edna Lema, Bakar Shime ambaye amempa nafasi ya kucheza na kuonekana kimataifa.
“Watu ni wengi sana wamenipa sapoti kufika nilipo nawashukuru Yanga na Thabit Kandoro wamenisaidia sana,” alisema Clara.
 
MWONEKANO
Anasimulia kuwa changamoto anayopitia kuhusu mwonekano wake watu kuufanbanisha na mwanaume kwamba haumuathiri kitu.
Anasema mwanzoni ilikuwa ngumu kukubaliana na hali hiyo namna ya watu wanavyomuongelea lakini kwasasa anachukulia kawaida.
“Nikifikiria wazazi wangu walinipa jina la Clara nawapuuza tu.”

ANA MCHUMBA
Straika huyo pia ana mchumba kama wasichana wengine.