Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CHEDA: Fei na Maxi wana madini miguuni

CHEDA Pict

Muktasari:

  • Hata Hassan Haji ‘Cheda’ humwambii kitu kwa Feitoto na anasema wanaosema hivyo, hawabahatishi kwani ‘fei’ ana uwezo mkubwa.

KILA mchezaji anatamani kucheza na Feisal Salum ‘Feitoto’. Ndiyo, uwezo wake mkubwa umewakalisha hadi wachezaji wa kigeni ambao wamekuwa wakiimbwa sana. kwa kifupi ukihoji wachezaji, wengi na kuwauliza ni nani angependa acheze naye timu moja wanamytaja Feitoto.

Hata Hassan Haji ‘Cheda’ humwambii kitu kwa Feitoto na anasema wanaosema hivyo, hawabahatishi kwani ‘fei’ ana uwezo mkubwa.

“Fei Toto ni kiungo bora kwa sasa. Amekuwa bora bila kujali anacheza timu gani.”


CHED 05

YEYE NA FEI TANGU KITAMBO WASHKAJI

“Mimi nimekua naye na mara zote tulikuwa tunahamasishana soka ndiyo kitu kitatupa maisha. Mwenzangu kapata bahati ya kuwahi kucheza Ligi Kuu Bara kwa mafanikio, najivunia yeye na naamini nami nitafikia mafanikio hayo,” anasema  kiungo wa Cheda, ambaye alifunga bao la ushindi kwenye mchezo wa fainali  yamichuano ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Burkina Faso, Zanzibar Heroes ikiishinda mabao 2-1 na kubeba kombe.

“Tulikuwa tunapena moyo soka litatutoa tupambane hivyo siwezi kumtaja kama ndiye alinifanya nipende soka,” anasema.

Cheda anasema kutokana na ubora wa Feitoto amekuwa akimtazama kwa kuwa sasa anampa changamoto ya kumfanya apambane zaidi na yeye aweze kufikia mafanikio kama aliyoyapata.


LILE SHUTI FAINALI MAPINDUZINI FEI MTUPU

Unakumbuka bao la jiooooni alilofunga kwenye fainali na kuipa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi Zanzibar Heroes, basi anafichua hiyo ni kawaida na ujanja wote aliuzoa kwa Feitoto.

“Mafanikio ya ufundi wa mchezaji mwenzangu Feitoto wa kupiga mashuti ya mbali nikiwa namfuatilia nimekuwa nikifanyia kazi, hivyo ile haikuwa bahati.  Nilifurahi kufunga bao la aina ile ambalo liliipa timu yangu mafanikio,” anasema.


CHED 04

BAO LA MAOKOTO

Anasema bao lile licha ya kumpa fedha kutoka kwa wadau mbalimbali, alipokea simu nyingi za pongezi na miamala ilimiminika.

“Nilipigiwa simu nyingi za pongezi na kupokea miamala ambayo siwezi kuweka wazi ni kiasi gani halitakuwa jambo jema.”

Cheda alifunga kwa shuti kali bao hilo lililoipa ubingwa Heroes baada ya kona iliyochongwa na na Feitoto na kuokolewa ndani ya boksina kutoka nje ya 18 na kufanya yake.


CHED 03

THIERY NA FABREGAS

Wakati mastaa wengi wakivaa namba za  jezi kwa maana tofauti huku wengine wakivaa miezi au tarehe zao za kuzaliwa, kwa upande wa Cheda kaweka wazi anavaa namba 14 kwa sababu ya Thiery Henry ambaye alianza kumfuatilia tangu akiwa na umri mdogo.

“Napenda kuvaa jezi namba 14 kwasababu ya kiungo mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Henry alikuwa ananivutia aina ya uchezaji wake hadi nikajikuta natamani kuvaa jezi namba yake hadi sasa,” anasema na kuongeza;

“Mbali na Henry, pia nilikuwa navutiwa na uchezaji wa Fabregas ambaye pia amepita Arsenal na Barcelona, huyo alikuwa ananivutia namna alivyokuwa anacheza na kunifanya nipende soka ambalo naamini litanipa maisha.”


CHED 02

MAXI, GEGO MADINI MGUUNI

Ligi Kuu Bara imebarikiwa kuwa na viungo wengi wazuri wazawa na wageni na kuwa vivutio kwa mashabiki na Cheda anawataja anaowakubali zaidi ni Maxi Mpia Nzengeli na Habib Idd ‘Gego’.

“Kuna nyota wengi wanafanya vizuri, wazawa na wakigeni na nimekuwa nikivutiwa na aina ya uchezaji wao. Pia nawatazama kama darasa la kujifunza vitu kutoka kwao kulingana na ubora walionao,” anasema na kuongeza;

“Mchezaji mzawa ambae napenda aina yake ya uchezaji ni Habib Idd ‘Gego’ wa Singida Black Stars na mchezaji wa kigeni ni Maxi Nzingeli. Wamebarikiwa vipaji, ni viungo ambao wana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira mguuni na kuachia kwa uharaka pasi zao zikifika kwa usahihi.”


CHED 01

KISA MILIONI 2 KACHA SHULE

Sio kila staa anaefanya vizuri uwanjani ilikuwa rahisi kwake kufikia mafanikio aliyonayo na kuimbwa na mashabiki ama wadau mbalimbali, wanapitia changamoto ambazo zinawapa ubora wa kuonyesha vipaji vyao kama anavyothibitisha Cheda.

“Haikuwa rahisi mimi kuingia kwenye soka, wazazi wangu walikuwa wanatamani kuona nafanikiwa kutokana na masomo, hawakutaka kunipa tumaini kwenye soka lakini niliamini katika ndoto hadi sasa nacheza,” anasema na kuongeza;

“Nimesoma hadi kidato cha nne na mara baada ya kuhitimu niliamua kuwekeza nguvu kwenye soka, nimecheza timu nne na iliyonipa jina ni Chrisc Zanzibar na Zimamoto ambayo imenileta bara sasa nakipiga Mashujaa.”

Anasema baada ya kutoka timu ya madaraja ya chini alijiunga na Zimamoto ambayo ilikuwa inacheza Ligi kuu wakamsajili kwa Sh2 milion ambazo ameweka wazi aliwapa wazazi wake na nyingine kutoa sadaka.


POPOTE FRESHI

Ni nadra sana kuona nyota wengi wanacheza nafasi zaidi ya tatu uwanjani, lakini kwa Cheda anaweza na anazimudu zote kwa usahihi.

“Mbali na nafasi ninayocheza sasa naweza kucheza nafasi zaidi ya tatu uwanjani na nimeshawahi kufanya hivyo, kiungo mshambuliaji, mkabaji na beki namba mbili, zote naweza kuzicheza kwa usahihi kabisa,” anasema Cheda ambaye anafafanua maana ya jina lake la utani ‘Cheda’, limetokana na mchezaji wa zamani wa Manchestar United, Federico Macheda na kuamua kufupisha kwa kujiita Cheda.