Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CARLOS KAISER: Tapeli aliyesajiliwa bila ya kucheza mpira kwa miaka 14

TAPELI Pict
TAPELI Pict

Muktasari:

  • Haya yalikuwa ni maneno ya Carlos Henrique Raposo maarufu kama Carlos Kaiser ambaye aliwahi kuwa mchezaji mpira kwa zaidi ya miaka 20, akicheza timu za mataifa mbalimbali duniani ikiwamo Mexico, Ufaransa na hata kwao Brazil ambazo alisaini nazo na hakuwahi kucheza hata mechi moja katika kipindi chote hicho.

“KLABU zinawadanganya watu wengi, hivyo mimi pia nilihitaji kuwadanganya. Hawakuweza kunifukuza, timu zote  nilizojiunga nazo zilisherehekea mara mbili, wakati niliposaini na kisha nilipoondoka.”

Haya yalikuwa ni maneno ya Carlos Henrique Raposo maarufu kama Carlos Kaiser ambaye aliwahi kuwa mchezaji mpira kwa zaidi ya miaka 20, akicheza timu za mataifa mbalimbali duniani ikiwamo Mexico, Ufaransa na hata kwao Brazil ambazo alisaini nazo na hakuwahi kucheza hata mechi moja katika kipindi chote hicho.

Carlos ambaye aliitwa jina la Kaiser akifananishwa mna mchezaji wa zamani wa Ujerumani, Franz Kaiser alitumia njia mbalimbali kuhakikisha  anasaini na kutocheza mechi yoyote katika timu zote alizopita.

Leo tumekusogezea stori ya mwamba huyu ambaye hadi leo bado historia yake inaishi katika mpira wa miguu.


TP01
TP01

HISTORIA YAKE

Carlos Kaiser alizaliwa mwaka 1963 huko Rio de Janeiro, Brazil na alikulia katika Jiji hilo ambalo linasifika katika suala zima la soka na hata familia yake ilikuwa ni mashabiki wakubwa wa mpira wa miguu.

Alizaliwa katika familia ambayo mama yake alikuwa  ni mlevi wa kupindukia na hilo ndilo lililokuwa likimpa njaa na shauku ya kutafuta pesa kwa njia yoyote ili kujipatia mkwanja na kujiondoa katika hali ya umaskini.

Akiwa mdogo alijaribu kucheza mpira wa miguu lakini ilishindikana kwa sababu hakuwa na kipaji, hivyo akaamua kuja na njia mbadala kwa sababu alifahamu ingekuwa ngumu kwake yeye kutoboa kama angefuata utaratibu  wa kawaida.

Alicheza katika timu za vijana za Batafogo na Flamengo kuanzia mwaka 1972 hadi 79 na baada ya hapo akaanza rasmi sasa kazi ya kudanganya na kushawishi timu zimsajili, kisha asicheze hata mchi moja.


TP02
TP02

MBINU ALIZOTUMIA

Kaiser alikuwa na njia nyingi za udanganyifu na anasimulia mchezaji wa zamani wa Brazil, Bebeto kwamba jamaa ulikuwa ukimpa ruhusa ya kumsikiliza tu, basi umekwisha.

“Maneno yake yalikuwa mazuri sana kiasi kwamba kama ungemruhusu kuyasema, basi ilikuwa umekwisha, alikuwa akikuongelesha. Hauwezi kuepuka kuingia katika mtego wake.”

Mbinu alizokuwa anazitumia ni kutafuta nafasi ya kuongea na marais wa timu na kuwaonyesha CV yake aliyokuwa ameipamba kwa taarifa nyingi za uongo.

 Katika mazungumzo yake alikuwa akisema kwamba alikuwa akitakiwa hadi na timu kubwa barani Ulaya kama Barcelona na ilikuwa ngumu kugundua kwa wakati huo kwa sababu hakukuwa na mitandao ya kijamii.

Pia alitumia waandishi wa habari aliowalipa kutaka wamfanyie mahojiano kupitia magazeti na televisheni ili kuzidisha hali ya watu kumuongelea sana.

TP05
TP05

Muda mwingine alikuwa akiwapa hadi mashabiki pesa ili wataje jina lake, mambo haya yalikuwa yakiwashawishi viongozi wa timu aliyohitaji wamsajili na mwisho walimpa mikataba.

Pia alikuwa akijenga urafiki na wachezaji wakubwa wa Brazil ambao alihakikisha anakuwa nao karibu akipiga nao picha na muda mwingine kuzunguka nao ili iwe rahisi kwake kupata timu kwa kuwa walimkutanisha na viongozi mbalimbali wa timu za Brazil na nje ya hapo.

Kuna wakati alipoenda Ufaransa, kujiunga na Gazelec Ajaccio, timu iliandaa mazoezi kwa ajili ya utambulisho wake na mashabiki walikuwa wanaruhusiwa kwenda kutazama, ili kuepuka aibu alichukua mpira na kuupiga kwa mashabiki kisha akabusu nembo ya jezi jambo lililosababisha aondolewe uwanjani.

Akiwa Ufaransa ukaribu wake na waandishi ulisababisha aandikwe kama mfungaji bora wa timu hiyo na akatumia sifa hiyo kurudi nayo Brazil kisha akaishawishi timu ya Bangu imsajili.

Hata hivyo, rafiki yake wa karibu Fabio “Fabinho” Barros alisema Kaiser hakujiunga na Ajaccio kama alivyoeleza bali alijiunga na Corsica na jezi ya Ajaccio aliyoitumia kulaghai watu ilikuwa ni ile aliyompa yeye ambayo walipiga picha wote lakini Kaiser alitumia picha, gazeti na leseni feki ya uchezaji iliyokuwa inaonyesha alicheza Ajaccio.


TP03
TP03

ALIVYOKWEPA KUCHEZA

“Wachezaji wengi wa mpira wa miguu wanapoenda katika mechi huwa wanataka kuingia uwanjani na kusaidia timu kushinda na wao kufunga magoli. Lakini mimi nilikuwa nakiangalia kitu kingine, jinsi gani naweza kuepuka kupiga mpira kwa gharama yoyote. Hicho ndicho nilichokuwa nikifikiria, na ningefanya chochote ili kuepuka hiyo,” alisema Kaiser katika mahojiano yake mwaka 2018.

Mara baada ya kusaini katika timu, gumashi huyu alianza kwa kusema hatocheza mechi kwa kudai amefiwa na bibi yake angalau mara nne, pia alikuwa wakimlipa mchezaji wa timu ya vijana kumjeruhi na kisha alimuomba rafiki yake ambaye ni daktari wa meno aandike risiti ya uongo, akidai kwamba matatizo yake ya mguu yalihusiana na meno yake. 

Timu moja iliwahi kumuomba mganga wa kienyeji amtibie wakidhani kwamba majeraha yake yametokana na mambo ya kishirikina, lakini Kaiser alimwambia mganga huyo kwamba: ”Chukua pesa uende, usijisumbue kufanya chochote kwa sababu nimepanga kukaa nje na kuwa na majeraha katika maisha yangu yote.”

Kuna wakati Kaiser alimpiga shabiki ngumi usoni ili apate kadi nyekundu kabla ya hata kuingia uwanjani wakati anaichezea timu ya Bangu ya Rio de Janeiro. 

Alipoitishwa kufafanua alichofanya kwa mmiliki wa klabu jamaa huyu alisema shabiki aliyempiga ngumi alikuwa akimtukana rais wa timu hiyo ndio maana aliamua kumpiga kwani rais wa timu kwake ni kama baba yake wa pili, hivyo alifanya hivyo ili kulinda heshima ya rais wake anayemkubali ‘kinyama’. 

Mmiliki huyo akaingia kwenye mfumo. Alifurahishwa sana, akamuongeza mkataba na akampa na nyongeza ya mshahara mara mbili.

Kaiser alieleza: ”Nilijuwa nikiwa karibu na rais naweza kubakia katika timu muda wowote ninaohitaji.’’


TP04
TP04

KWANINI HAKUFUKUZWA

Wachezaji wengi aliokuwa anacheza nao timu moja walijua alichokuwa akikifanya, lakini hakuna aliyezungumza kwa sababu walimwona Kaiser kama mtu muhimu kwao kutokana na yale aliyokuwa akiwafanyia.

“Alikuwa tayari kila wakati kufanya mambo ya kuwafurahisha wachezaji wenzake,” anasema Carlos Alberto Torres, nahodha wa timu ya Brazil iliyoshinda Kombe la Dunia la 1970.

Kaiser alijua kwamba alihitaji kupata watu watakaomlinda na kwa sababu hiyo alitumia sana wachezaji wenzake kuhakikisha anakuwa salama.

Baadhi ya maandiko yanamtambua kama ‘mlezi wa mpira wa miguu,’ Kaiser alikubali kulaumiwa kwa ajili ya wachezaji wenzake pale walipoingia kwenye matatizo, pia alikuwa akiwatafutia wanawake na kuwapeleka katika kumbi za starehe.

Inaendelea kesho