Azam FC, Yanga kumaliza ubishi Dar

Muktasari:
- Hata hivyo ikafuata Simba, jamaa wakapigwa kidude, hapo ke-lele zikapungua kidogo kwa vile Mnyama msimu huu wapo vizuri, kisha zikafuata JKT Tanzania na Coastal Union.
ILIANZA kunyukwa Kagera Sugar, baadhi ya mashabiki wakasema Wanankurukumbi wameotewa kwani walikuwa hawajakaa sawa. Ikapigwa KenGold, KMC na Pamba Jiji, wimbo ukawa huo huo kwamba, Yanga ni kama iliwaotea vibonde hao.
Hata hivyo ikafuata Simba, jamaa wakapigwa kidude, hapo ke-lele zikapungua kidogo kwa vile Mnyama msimu huu wapo vizuri, kisha zikafuata JKT Tanzania na Coastal Union.
Juzi kati Yanga ikapangwa kukutana na Singida Black Stars, iliyo ya moto, wale mashabiki waliokuwa wakiiponda Yanga, wakaibuka na kusema sasa imekutana na kiboko yao.
Kama utani, Singida ikapigwa nyumbani na leo Jumamosi ni zamu ya Azam FC itakayokabiliana na wababe hao wa soka nchini.
Sio mechi nyepesi hata kidogo, kwani Azam ili-yokimbizana na Yanga msimu uliopita na kuja kuchemsha mwishoni kwenye ubingwa wa Ligi Kuu, imetoka kuikanda KenGold mabao 4-1, timu iliyoi-toa jasho Yanga kwa kufungwa 1-0 kwa mbinde, hu-ku mpira uliokuwa ukielekeza wavuni kusawazisha bao hilo uligoma.

Hii ikiwa na maana mchezo wa leo unaikutanisha timu yenye kufunga mabao machache, dhidi ya timu iliyotoka kugawa dozi nene katika pambano liotaka-lopigwa kuanza saa 12:00 jionui kwenye Uwanja wa Azam Complex.
Mchezo huo maarufu kwa jina la Dar es Salaam Dabi, Yanga itakuwa mwenyeji wa Azam huku rekodi zikionyesha mechi mbili za mwisho kukutana, Yanga imeibuka kidedea huku mara zote hizo ikibeba kombe mbele ya Azam.
Ilikuwa Juni 2 mwaka huu katika fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) iliyochezwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar ambapo dakika 120 matokeo yalikuwa 0-0, katika penalti Yanga ikashinda 6-5. Baada ya hapo, wakakutana tena kwenye fainali ya Ngao ya Jamii Agosti 11, mwaka huu, dakika 90 zil-imalizika kwa Yanga kushinda 4-1. Leo kazi ipo pale Chamazi. Azam ikiwa ndio timu pekee katika mechi za mashindano iliyogusa wavuni wa vinara na ma-bingwa hao wa nchi kwa misimu 30 sasa.

Ugumu na ushindani wa mchezo wa leo unakuja kwa namna ambavyo makocha wawili wa timu hizo wanavyokwenda kukutana huku kila mmoja hesabu zake ni kulinda heshima na kujiweka pazuri zaidi kwenye msimamo wa ligi. Yanga wanaongoza ligi wakiwa na pointi 24, Azam inashika nafasi ya nne na pointi zake 18. Ikishinda inafikisha 21 ambapo itakuwa tofauti ya pointi tatu na Yanga ambayo yenyewe inahitaji kuongeza gepu na wapinzani wake.
Kocha Miguel Gamondi akizungumzia timu yake ya Yanga kuelekea mchezo huo, alisema kikosi kipo tayari kukutana na Azam baada ya kurejea kutoka Zanzibar walipotoka kuifunga Singida Black Stars bao 1-0.
Gamondi alisema wanatarajia mchezo mzuri na mgumu dhidi ya Azam akienda kukutana na timu ambayo inafundishwa na kocha wanayefahamiana vizuri.

“Tumesafiri na kurudi hapa (Dar es Salaam) tumefan-ya maandalizi ya kurudisha utulivu wa mwili, tupo tayari kucheza mechi nyingine ngumu,” alisema.
“Siku zote tumekuwa na nidhamu ya kuwaheshimu wapinzani wetu, tunakwenda kukutana na Azam ambayo ni timu nzuri, ina wachezaji wazuri na kocha mzuri ambaye nilifanya naye kazi miaka 25 iliyopita
“Itakuwa mechi yenye ushindani, nadhani timu mbili bora zitashindana katikati ya uwanja, itakayokuwa vizuri kushinda nyingine itashinda, tunataka kushinda ili tuendelee kulinda ubora wetu na kuweka hai malengo yetu.” Kocha wa Azam, Rachid Taoussi alisema inakwenda kucheza mchezo mkali lakini kikosi chake ni miongoni mwa timu bora Tanzania inayoundwa na wachezaji wa kimataifa.

Taoussi alisema Azam itakwenda kucheza mchezo huo ikitumia falsafa yake ambapo tayari wanajua uimara na mapungufu ya Yanga ambayo pia ina wachezaji na kocha bora. “Hii ni mechi ngumu lakini Azam timu kubwa pia hapa Tanzania, ina wachezaji wakubwa saba mpaka nane wanaocheza timu za taifa, kwa hiyo tunakwenda kucheza mechi ngumu dhidi ya Yanga,” alisema Taoussi.
“Tutakwenda kucheza kwa kutumia falsafa yetu, nina miezi miwili sasa hapa Tanzania, nawajua wachezaji wa timu pinzani lakini pia tumewafanyia tathimini wapinzani wetu, wana timu nzuri yenye wachezaji wazuri na kocha mzuri.
“Mimi na kocha wa Yanga (Gamondi) tunafahamiana sana, tumewahi kufanya kazi pamoja Wydad miaka ya nyuma, lakini sisi ni wataalam tutapambana uwanjani na kusahau urafiki wetu kwa dakika 90.”

Nini Kitatokea? Hapa Mwanaspoti linakupitisha kati-ka mambo ambayo yanatarajiwa kutokea katika mchezo huo ambao Prince Dube aliyeitumikia Azam kwa misimu minne, anakwenda kukutana na waajiri wake wa zamani kwa mara ya pili, wakati Feisal Salum ‘Fei Toto’ naye akiwahi kuitumikia Yanga kwa misimu mitano, anakutana tena na chama lake la zamani.
Gamondi, Taousi
Msimu huu timu hizo tayari zimeufungua kwa kuku-tana katika fainali ya Ngao ya Jamii huku Azam ikipoteza kwa mabao 4-1, lakini pia iliufunga msimu uliopita katika fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) Azam ikipoteza tena kwa penalti 6-5 baada ya da-kika 120 matokeo kuwa 0-0.
Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi ameonekana ku-wa mbabe mbele ya Azam lakini mara zote hizo alipambana na Youssouph Dabo ambaye tayari ameondoshwa huku nafasi yake ikichukuliwa na Ra-chid Taoussi.
Ubabe wa Gamondi mbele ya Azam umebaki kuwa deni kwa Taoussi ambaye leo ana kazi kubwa ya kupindua matokeo hayo mabaya iliyoyapata timu yake mechi mbili za mwisho. Taoussi ambaye amei-ongoza Azam kucheza mechi nane za Ligi Kuu Bara tangu akabidhiwe kikosi hicho, kuna mwanga fulani amekuwa akiuona licha ya kuanza taratibu.

Katika mchezo wa kwanza dhidi ya Pamba Jiji nyumbani, alipata suluhu, kabla ya kuja kuikandami-za KMC kwa mabao 4-0. Lakini pia ameshuhudia kichapo kimoja kutoka kwa Simba walipofungwa 2-0 na suluhu nyingine kutoka kwa Mashujaa.
Matokeo ya mechi zingine alizoongoza kocha huyo raia wa Morocco yapo hivi; Azam 1-0 Coastal Union, Namungo 0-1 Azam, Tanzania Prisons 0-2 Azam na Azam 4-1 KenGold.
Taoussi anakutana na Yanga ya Gamondi ambayo haijaonja ladha ya sare wala kipigo tangu kuanza kwa msimu huu katika mechi zake zote za ki-mashindano ambazo ni 14 zikiwemo mbili za Ngao ya Jamii, Ligi ya Mabingwa Afrika (4) na Ligi Kuu Ba-ra (8).
Bacca, Job
Yanga ina rekodi ya kucheza mechi nane mfululizo za Ligi Kuu Bara bila ya kuruhusu nyavu zake kuti-kiswa. Katika safu yao ya ulinzi, Dickson Job na Ibra-him Bacca ndiyo waliocheza mechi nyingi sam-bamba na kipa wao, Djigui Diarra ambapo wote wamecheza saba kati ya nane. Bacca na Job wame-fanya kazi kubwa ya kumlinda Diarra asifikiwe kirahi-si na wapinzani, hivyo leo mabeki hao wana kazi nyingine ya kuendeleza hicho walichokianza, hivyo wapo mtegoni.
Blanco kuvunja mwiko?
Mshambuliaji wa Azam FC, Jhonier Blanco raia wa Colombia anatarajiwa kuongoza safu ya ushambuli-aji baada ya Nassor Saadun kuwa na majukumu ndani ya Taifa Stars.
Ukimuondoa Blanco mwenye bao moja katika ligi msimu huu, pale Azam kuna Adam Adam ambaye naye ni mshambuliaji, huyu amekuwa hana nafasi kubwa sana ya kucheza kulinganisha na wenzake.
Blanco ambaye anabaki kuwa chaguo la kwanza eneo la ushambuliaji, kuna jambo anatakiwa kulifan-ya.
Mcolombia huyo kwa nafasi yake anatakiwa kupam-bana kufunga bao ambalo litaweka rekodi mbili, kwanza kuitibulia Yanga ambayo haijaruhusu kufungwa hadi sasa, pili kuvunja mwiko wa washambuliaji wa Azam kushindwa kufunga mbele ya Yanga.
Mara ya mwisho mshambuliaji wa Azam kufunga katika mchezo dhidi ya Azam alikuwa Prince Dube aliyefanya hivyo Oktoba 23, 2023 wakati Azam iki-fungwa 2-1. Baada ya hapo, zimechezwa mechi tatu na kushuhudiwa Azam ikifunga mabao matatu kupitia viungo, washambuliaji hakuna aliyefunga.
Ipo hivi: Machi 17, 2024 Azam ilishinda 2-1 kwa mabao ya Gibril Sillah na Feisal Salum ‘Fei Toto’ am-bao ni viungo wa ushambuliaji, kisha Juni 2, 2024, mechi iliisha 0-0 ikiwa ni fainali ya Kombe la FA ndani ya muda wa kawaida na Agosti 8, 2024, Azam ilifungwa 4-1 katika fainali ya Ngao ya Jamii, mfun-gaji wao alikuwa Feisal Salum ‘Fei Toto’.
Hata hivyo, Azam msimu huu mabao 12 iliyofunga, manne yamefungwa na washambuliaji, mabeki (4) na viun-go (4), hivyo imeyagawa mabao yake kwa namna hiyo. Katika mabao yao 12, washambuliaji waliofun-ga ni Saadun (3) na Blanco (1), huku viungo walio-funga ni Idd Seleman (2), Feisal Salum (1) na Gibril Sillah (1), huku mabeki Lusajo Mwaikenda (2), Na thaniel Chilambo (1) na Cheikh Sidibe (1) nao wakitupia.