Prime
Aquila beki FGP anayemkubali Msuva

KATIKA maisha ya utafutaji kwenye kila kazi anayomuingizia kipato mwanadamu yoyote haiwezi kukosa changamoto.
Ualimu, Udaktari, Uruban, Mwanasheria, Polisi wote kwenye majukumu yao wanakutana na changamoto ambazo zinawafanya wapambane nazo ili waweze kuingiza kipato.
Kwa miaka ya hivi karibuni soka nalo limegeuka biashara kwa wachezaji kujipatia kipatop pale wanaposajiliwa na hata kulipwa mishahara huku na wao pia wakikutana na changamoto.
Beki wa kushoto Fountain Gate Princess, Aquila Gaspar amethibitisha hilo huku akikiri kuwa changamoto wanazokutana nazo ndio zinawafanya wapambane zaidi ili kuweza kufikia malengo.
Mwanaspoti limepata nafasi ya kuzungumza na beki huyo ambaye amefunguka mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumtaja Saimon Msuva kuwa ni miongoni mwa mastraa waliomfanya afike alipo sasa.
MSUVA ANAVYOMPA NGUVU
Msuva mwenye miaka 29 ndiye mchezaji wa mwisho kwa Yanga kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara, alifanya hivyo msimu miwili mfululizo 2014/15 na 2015/16 kabla kwenda Morocco kucheza soka la kulipwa.
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva anayecheza soka la kulipwa Saudi Arabia akiwa na Al-Qadsiah, miaka ya nyuma alikuwa anakipiga Yanga na na kugeuka mwiba kwa mashabiki kila timu yake inapokutana na Simba alikuwa akiambulia zomea zomea changamoto ambayo imewapa nguvu mastaa wengi wa sasa.
"Natamani kukutana sana Msuva kwakuwa ni mchezaji ambaye alinifanya kucheza soka bila ya kukata tamaa pamoja na changamoto tunazokutana nazo uwanjani;
"Siku ya kwanza mimi kwenda uwanja wa taifa Msuva akiwa Yanga wakati huo mashabiki waliimba wakisema toa huyo toa huyo lakini haikuchukua mda mshambulioaji huyo aliibuka mfungaji bora msimu ulofata naaakaondoka kucheza nje huwa namtumia kama mfano mkubwa sana katika mizunguko yangu naamini hata iweje ila kesho yenye leo nzuri haitabaki kuwa mbovu," anasema.
Anasema Msuva asingeamini katika kupambana na kuufanya mpira ndio maisha yake angekatisha ndoto yake kwani angehisi kuwa kuzomewa ni kufanya vibaya milele.
SOKA LAMKUITANISHA NA WATU
Kuna majukumu yanakufanya ukutane na watu ambaop hukuwahi kutarajia kukutana nao lakini kutokana na kazi uliyo chagua kufanya inakufanya ukutane na watu wengi kutoka mataifa mbalimbali.
Mlinzi huyo wa kushoto anasema alifanikiwa kucheza misimu yote tangu kuanzishwa kwa Ligi Kuu ya Wanawake hivyo ilisaidia kukutana na wachezaji wengine mbalimbali na kujijengea uzoefu wa kucheza mpira vizuri.
"Kwa upande wangu nikacheza misimu yote tangu kuanzishwa kwa Ligi kuu ya wanawake 2016 msimu wa kwanza, nilikuwa nacheza timu ya Kigoma Sister's, nikacheza Mlandizi Queens na msimu uliofuata nikacheza Simba Queens na sasa nautumikia Fountain Gate Princess;
"Nimekutana na watui wengi ambao sikutarajia kama ningeweza kukutana nao siowezi kuwataja wote lakini mafanikio yamenikitanisha na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan nikiwa Simba." anasema.
WADHAMINI NA HAMASA
Aquila anasema soka la wanawake hapa nchini, imepiga hatua kubwa kwa sababu wachezaji wengi wamekuwa wanafanya vizuri katika mashindano mbalimbali tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Anasema kipindi hicho hakukuwa na wadhamini wengi ukilinganisha na kipindi cha sasa, wadhamini kwa mpira wa miguu kwa wanawake wameongezeka.
Hali hii inawapa hamasa wanawake wengi kuzidi kufanya juhudi katika mechi ili watimize malengo yao waliyokuwa wamejiwekea.
Mlinzi huyo wa kushoto anatoa wazo lake kuwa wanawake wengi wanamchukulia mpira wa miguu kama kazi, siyo kama zamani wachezaji walikuwa wanacheza kama kujifurahisha.
Hivi sasa wanawake wengi wanafanya mazoezi wanatumia muda mwingi kujifunza nakutafuta mazingira rafiki kwao ili kukuza vipaji vyao.
"Nashukuru waandishi wa habari nchini kwa kuhakiksha jamii inapata taarifa kwa kusoma na kuona, hata kusikiliza hivyo imekuwa rahisi kwa wazazi na walezi wengi kuwaruhusu watoto wao kucheza mpira wa miguu bila kujali Jinsia,"anasema.
MISIMU SABA TIMU NNE
Soka la wanawake lina misimu minne sasa tangu limeanzishwa 2016 huku Simba akitwaa mataji matatu Mlandizi, JKT Queens mara mbili mfululizi, Simba mara tatu na msimu ulioisha JKT Queens kabeba taji hilo tena.
"Soka ndio maisha nayoishi kwasasa naendesha maisha yangu kupitia mpira niko nakila kitu mtoto wakike anachopaswa kuwa nacho katika umri huu naweza jitegemea kikubwa zaidi mpira unanifanya nitimize ndoto;
"Nimeshatwaa taji nikiwa Simba malengo yangu ni kuendelea kupata mafanikio nikiwa kwenye soka hivyo nimewekeza nguvu zangu kwenye soka nina matumaini makubwa ya kufanikiwa kupitia soka nimeanza kucheza tangu soka la linaanzioshjwa na ninajivunia nilichokipata." anasema.
MALENGO
Aquila anasema uongozi wa timu una malengo makubwa na uko na mkatamanio makubwa kuona kila mchezaji anakuwa na maisha yanayoelewekea ya kujitegemea mwenyewe.
Anasema uongozi huo hutoa semina ambazo zinakuwa na mchango mkubwa kwa wachezaji ambazo zinawajengea uwezo katika kazi zao.
“Hivi sasa nipo na vijana ambao niliowaajiri kunisaidia kazi zangu kwa kuwa siwezi kufanya kila kitu mwenyewe, hivyo nilitumia fursa ya semina na hivi sasa ninageuka kuwa fursa kwa vijana wengine,”anasema.
Anafafanua kuwa, nje na mpira hivi sasa anafanya kazi na Hlucky & Martin Beverages Company Limited ambao ni watengenezaji na wasambazaji wa vinjwaji kama Kombucha Sweet Wine na Mobimba Spirt Drink waliopo Karagwe, Kagera.
CHANGAMOTO
Anasema siku zote changamoto lazima ziwepo na hii inatokana na timu za wanawake kutopewa ushirikiano wanapokuwa wanacheza mpira uwanjani, mfano ujio wa mashabiki unakuwa ni wa hali ya chini.
Anafafanua kuwa Klabu nyingi kutokuwa na uwezo wa kudumu kuendelea katika Ligi na kukosa wadhamini.
"Nafikri tatizo la kiuchumi nchini, limekuwa ni lenye kuu ya changamoto katika timu za mpira wa miguu wa wanawake licha ya tatizo la uchumi bado timu hazina mashabiki,"anesma.
SOKA LINALIPA
Mlinzi huyo wa kushoto anawashauri vijana wenzake jambo la kwanza ni kumuomba Mungu kwa kila jambo unalolitaka kulifanya, kingine uvumilivu na heshima kwa watu wote mdogo na mkubwa.
"Nawapenda sana, vijana wenzangu, wachezaji wenzangu wa Fountain Gate Princess, ushauri wangu kwao ni hakuna kisichowezekana kama wataalamu chochote kinawezekana.
"Watambue kuwa mpira hivi sasa umekuwa mkombozi wa familia mbalimbali za wachezaji mifano ipo mingi tu katika nchi yetu ya Tanzania, ukiamua kubadilika na kufika malengo yao bado muda hautoshi.
Anasema anawashauri kutokata tamaa , katika maisha tuache tabia ya kukata tamaa muda unaanza kujifunza unachotakuwa nikujiamini na kuamini watu wako wa karibu.
MCHEZAJI MKUBWA
"Malengo yangu namuomba Mungu anifanye niwe bora anipe kitu ambacho kitanisaida kadri maisha yanavyozidi kwenda, anipe uzima nisiwe kama nilivyokuwa zamani nizidi hapa sasa.
Malengo yangu hasa ni kuwa mchezaji mkubwa mwenye mafanikio, nikipata fedha niwekeze katika miradi mbalimbali, kumbuka wapo wachezaji wengi wamekuwa wakicheza mpira na muda wao wa kustaafu ukifika wanakuwa hawajajiwekeza na chochote katika familia zao hata kwa jamii hivyo wanakuwa na maisha ambayo siyo mzuri.
Mimi ninatamani kucheza mpira kwa malengo ili niweze kupata mafanikio ya kiuchumi baadae ikiwezekana niajiri vijana wenzangu katika shughuli ambazo nitakuwa nazifanya hapo baadae.
WASIFU
Jina: Aquila Gaspar
Kuzaliwa: Kagera
Umri: 23
Nafasi: Beki
Klabu: Fountain Gate Princess
Alikopita: Kigoma Sisters, Mlandizi Queens, Simba Queens,