Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

AKILI ZA KIJIWENI: Usishangae tukashindwa kumtumia Mama Samia

TANZANIA huwa tunapata sana bahati ya kupata marais ambao wanapenda michezo na wanaonyesha nia ya kuifanya ipige hatua.

Rais Julius Nyerere katika utawala wake ndio nchi ilijenga viwanja vingi lakini hata timu zetu zikaanza kushiriki mashindano ya kimataifa.

Akaja Rais Ali Hassan Mwinyi ambaye naye katika nyakati yake baadhi ya viwanja vilijengwa lakini pia tukashuhudia timu ya taifa 'Taifa Stars', wanariadha na mabondia wakifanya vizuri katika mashindano ya kimataifa wakichagizwa na sapoti kubwa ya serikali.

Baadaye ukaja utawala wa Rais Benjamin Mkapa. Mwanzoni yule mwamba alionekana kama sio mpenzi sana wa michezo lakini muda mfupi kabla ya awamu yake kumalizika akatushtua kwa kujenga uwanja mkubwa wa kisasa wa soka ambao sasa unapata heshima kubwa Afrika.

Nchi katika awamu ya nne ikabahatika kumpata Jakaya Mrisho Kikwete. Huyu mapenzi yake na michezo hayakujificha tangu alipokuwa waziri na alifanya mengi makubwa ikiwamo kulipa makocha wa timu za taifa.

Awamu iliyopita tukawa na John Magufuli ambaye alianzisha utaratibu wa kutoa fungu la kuhudumia timu za taifa.
Na sasa tuna Rais Samia Suluhu Hassan. Ana muda mfupi madarakani lakini amefanya mengi makubwa michezoni.
Kaendelea kuhudumia timu za taifa, anadhamini mashindano ya soka wanawake Afrika Mashariki na Kati na pia anasaidia wanamichezo wa michezo mingine.

Bahati mbaya ya marais hawa ni kuwa na watu wengi wanaowazunguka ambao wanaonekana hawana maslahi makubwa na sekta ya michezo. Hawaitazami kama moja ya vyanzo imara vya uchumi na ajira kwa nchi.
Wanaishia kuwapa ushauri wa kufanya vitu vya kawaida michezo ambavyo haviachi alama kubwa ingawa wakuu hawa wa nchi wenyewe wanaonekana wana utayari wa kufanya hii sekta ipige hatua.

Mfano Rais Samia chini yake tunaweza kuwa na shule na vituo vikubwa vya michezo, viwanja na kumbi kubwa za michezo na matukio ya sanaa na kadhalika.

Lakini utashangaa hadi pale atakapomaliza muda wake madarakani, watu wa sekta nyingine ndio wakamtumia vizuri huku sisi wa michezo tukibaki nyuma.