Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

AKILI ZA KIJIWENI: Bado Kapombe, Zimbwe hawajazeeka

KINACHOFANYIKA kuhusu Shomari Kapombe na Mohammed Hussein ‘Zimbwe’ baada ya Simba kutoka sare ya mabao 2-2 na Power Dynamos ugenini, Jumamosi iliyopita sio sawa na hawatendewi haki wachezaji hao wawili.

Kwanza timu haijafanya vibaya kwa vile imepata matokeo ya sare ya mabao ambayo inawafanya wahitaji hata sare ya 0-0 ama 1-1 , au ushindi wa aina yoyote ule ili waweze kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwa Simba ilivyo na uzoefu na mashindano hayo hasa hatua kama hizi za mtoano naona ina nafasi kubwa ya kupata ushindi wa nyumbani, Oktoba Mosi na kusonga mbele katika mashindano hayo.

Ila kuna hili la Kapombe na Zimbwe ambalo baadhi ya watu wenye mihemko wanajaribu kutuaminisha kuwa wawili hao wamezeeka na wamechoka hivyo Simba inakosea kuwapanga badala ya kuwapa wachezaji wengine nafasi ya kucheza.

Nasema mihemko kwa sababu hoja wanazotoa kututhibitishia kuchoka kwao, ni nyepesi na hazina mashiko kwa vile haziendani na uhalisia wa mchezo wa mpira wa miguu.

Kapombe wanasema amechoka kisa alipigwa chenga na Joshua Mutale wa Power Dynamos ambaye alipiga krosi iliyozaa bao la kwanza la timu hiyo ya Zambia.

Hii inachekesha kwani katika soka, kupigwa chenga ni jambo la kawaida kwa mchezaji na mara nyingi inapotokea nafasi ya kuwakutanisha beki au kiungo wa timu moja dhidi ya mshambuliaji wa upande mwingine anapokuwa na mpira.

Lile bao la kwanza la Power Dynamos halikutokana na Kapombe kupitwa bali pia hata wachezaji wengine wa Simba hasa waliokuwa katika eneo la ulinzi wangeweza kuzuia lisifungwe kama wangewajibika.

Kuhusu Zimbwe wanaishia kusema huwa anapitwa kirahisi lakini hadi sasa hawatuambii huwa anapitwaje na je kwa zile mechi ambazo Simba inashinda huwa hapitwi?

Kapombe na Zimbwe ni binadamu haimaanishi watakuwa na ubora siku zote, kuna nyakati wanaweza wasiwe kwenye fomu zao. Sasa ikitokea hivyo tusije na hoja dhaifu za kuwa wamezeeka na wanahitaji kupumzishwa ili wacheze wengine.