Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dili iliyokufa - 39

HADITHI - 39 Pict

ILIPOISHIA

Kabla ya hapo nilikuwa nikiomba hadi shilingi laki mbili kwa  mume  wangu niliyemkimbia na pia  niiliona hazitoshi lakini huko kwa mganga niliona elfu thelathinizingetosha. Nilikuwa nimebadilika sana.

   Mgannga akanipa shilingi elfu thelathini.

   “Sikiliza nikwambie. Wakati unatoka usiwambie wenzako  kuwa unakwenda kununua vitu. Wambie unakwenda kumsalimia ndugu yako fulani. Umesikia?”

   “Sawa. Sitawambia”

   “Ukiwambia wataona wivu halafu wataanza  kukuchukia”

   “Kweli”.

SASA ENDELEA...


“HAYA nenda uwahi kurudi. Angalia usiende safari nyingine yule  mume wako wa kwanza asije akakuona”

   “Hata akiniona sina  haja naye”

   “Lakini mimi sipendi akuone”

   “Hataniona, muda  huu yuko kazini kwake”

   “Sawa.  Basi nenda”

   Wakati huo tulikuwa tumo chumbani. Nikavaa nguo zangu za kutokea kisha nikatoka uani na kuwambia wale wenzangu kuwa ninakwenda  kumsalimia mdogo wangu ambaye alikuwa anaumwa.

   “Ni wapi?” Mke mkubwa akaniuliza.

   “Anaishi  Majengo”

   “Hutafika mjini?”

   “Hapana, sitafika”

   “Utarudi saa ngapi?”

   “Ni kiasi tu cha kumsalimia na kurudi. Sitakaa sana”

   “Haya mwaya. Kama mzee amekuruhusu nenda tu”

   Nikatoka. “Mwanamke anauliza maswali kama polisi!” nikajisemea kimoyomoyo peke yangu huku nikichanganya mwendo kuelekea kwenye kituo cha daladala. Nilipofika  kwenye kituo nikapanda daladala iliyonishusha stendi. Pale pale stendi nilisajili laini nyingine ya simu yangu kwani tangu nilipotoroka kwa mume wangu, simu yangu niliizimaili mume wangu asinipigie na kuniuliza niko wapi.

   Baada ya kumaliza zoezi hilo nikachapuka kuelekea kwenye maduka  ya wachaga yalioko barabara ya kumi na tatu.    Nikaingia  katika duka moja na kununua vitu nilivyokuwa navitaka  kisha nikaharakisha  kurudi stendi ili nipande daladala ya kuniirudisha Mwahako.

   Nilikuwa nimepiga kama hatua tano hivi,ghafla nikaona mtu amesimama mbele yangu kama aliyekuwa akinisubiri.

   Moyo  wangu  ukapiga, paa! Unajua alikuwa nani? Alikuwa Mudi, yule rafiki wa mume  wangu. Alikuwa amesimama akinitazama kwa shauku. Sikuwa na hakika  kwamba  alikuwa anajua kuwa niliondoka nyumbani kwa rafiki yake au  alikuwa hajui.

Laiti kama ningemuona mimi kabla ya yeye ningemkwepa.

Lakini alikuwa amewahi kuniona mimi na kusimama kunisubiri. Ikabidi na mimi nisimame nimsalimie.

“Ah ni wewe shemeji au macho yangu?” akaniuliza.

“Ni mimi” nikamjibu huku sauti yangu  ikiwa imenywea.

“Habari za siku?” akaniuliza huku akinipa mkono.

“Nzuri, sijui zako” nikamjibu.

“Uko wapi siku hizi. Mume wako aliniambia uliondoka nyumbani bila  kumuaga na hata hajui uko wapi”

“Niko humu humu  mjini”

“Ni kweli uliondoka nyumbanni kwake?’

“Ni kweli”

“Kwanini sasa shemeji umemkimbia mwenzako, amekukosea nini?”

“Ana shida sana yule bwana, Nimemvumilia nimechoka. Nimeona  niondoke tu nisalimishe masiha yangu”

“Ana shida gani. Hebu nidokeze kidogo nikamrekebishe”

“Shida ni nyingi tu. Kwanza ni malaya. Kila siku anarudi nyumbani saa nane usiku. Unapomuuliza anakujia juu na kukuonesha dharau. Pesa yake haionekani. Ukimuomba  pesa anakwambia sina. Kila siku hana  pesa. Sasa mimi nitaishije na mtu wa aina ile?”

“Eh…!  Umempa wakati mgumu kwa sababu anahangaika sana. Na kubwa lililomtia wasiwasi ni kwamba hajui umekwenda wapi. Amekwenda polisi kupiga ripoti….” Alipotaja polisi nikashituka kidogo.

“Polisi amefuata nini?”

“Amekwenda kupiga  ripoti ya kupotea kwa mke  wake. Hivi ninavyokwambia polisi pia wanakutafuta. Haikutosha alikwenda pia  kwa waganga”

“Mganga mmoja akamwambia mke wako ameolewa na mganga baada ya kuzugwa akili yake kwa dawa na hawezi kurudi mpaka  huyo mganga mwenyewe ategue dawa zake”

Maneno hayo yalikuwa ni sahihi kwamba nilikuwa nimerogwa na yule mganga ili nibaki pale nyumbani kwake bila kujielewa. Na kwamba kupata akili kwangu kulitegemea mganga huyo ategue dawa zake yeye mwennyewe ndipo ningeweza kupata akili na kuondoka nyumbani kwake.

Kwa kauli ile ya Mudi ni kwamba  hao waganga ambao mume wangu aliwafuta walishindwa kutegua dawa hizo na ndio maana walimwambia mume wangu, ni  mpaka huyo mganga aliyenitegea dawa hizo azitegue mwenyewe.

Ningekuwa na fikira za kawaida ningejiuliza kama kweli yule mganga angetegua dawa hizo kwa hiyari yake wakati ananihitaji? Na kama asingehiyari kuzitegua ningeendelea kuishi naye hadi lini?

Lakini badala ya maneno hayo ya Mudi kuzindua akili yangu na kunipa hisiakwamba  nimerogwa kweli na ndio maana  ninaishi kwa yule mganga,  nikaruka kimanga.

“Si kweli.  Sijarogwa na mganga yeyote. Na wala sijaolewa na mganga. Niko kwa rafiki yangu  mmoja huko Chumbageni”  nilimwambia yakiwa ni maneno ya uongo mtupu. Niliamini ni kweli kwamba mtu unaporogwa unakuwa huna akili kabisa.

“Kwa hiyo huna mpango wa kurudi kwa mume wako?” Mudi akaniuliza.

“Kwa kweli sina mpango huo. Pale nyumbani ndio nimeshaondoka na sitarudi tena. Bora na atafute mke mwingine, asinitarajie mimi tena na wala asihangaike kunitafuta”

“Hebu nielekeze huko Chumbageni kwa  rafiki yako unakoishi”

“Huko ni siri yangu, simwambii mtu”

“Kwanini shemeji unafanya hivyo? Mimi nakusihi urudi kwa mumeo mmalize tofauti zenu. Matatizo ya wanandoa humalizwa kwa mazungumzo tu na sio kukimbiana”

“Matatizo yetu sisi yalishashindikana kumalizwa kwa mazungumzo. Shemeji usisumbuke, mimi sitarudi tena kwa rafiki yako. Yeye atafute mke mwingine. Hivi anavyonikosa ndio atajua thamani yangu”

“Sasa nikikutana naye nimwambieje?”

“Mwambie vyovyote utakavyojihisi kumwambia ila hilo la kurudi kwake mwambie alisahau”

“Waonaje, nitafute wazee tuje huko unakoishi tuwapatanishe. Ninakwambia hivyo kwa sababu huyu jamaa anahangaika sana kwa sababu yako na kwa weli anatia huruma”

“Mimi simtaki tena hata kama mtakuja kutupatanisha, ni kazi bure. Tena mwambie aache kulipeleka suala langu polisi, mimi si mhalifu. Tulipokubaliana tuishi hatukuenda polisi na hivyo tulivyoachana asiende polisi. Kwaheri shem, nachelewa gari…”

Kule kuagana kwetu pia kulikuwa ni vichekesho. Baada  ya kuwambia ‘Kwaheri shem, nachelewa  gari’ nilionodoka nikamuacha hapo hapo barabarani ameduwaa akinitazama. Kama angekuwa na akili ya kutosha angejua kuwa nilikuwa nimezugwa.

Na kilichoniondoa haraka wakati ule tunazungumza niliyakumbuka  maneno ya yule mganga aliponiambia nisichelewe kurudi.

Nilichapuka hadi kituo cha daladala. Hapo nikasimamakusubiri daladala inayokwenda Mwahako.

Kila mara  nilikuwa natazama nyuma kumuangalia Mudi. Nilijiambia kama ningemuona ananifuata nyuma nyuma ningemkwepa na kumkimbia. Sikutaka ajue nilikuwa nakwenda wapi au nitapanda daladala ya kwenda wapi. Nikamuona  amesimama mahali pale pale tulipokutana lakini alikuwa anazungumza kwenye simu.

Hisia zangu zikaniambiakwamba alikuwa amempigia simu mume wangu na kumwambia kuwa amekutana na mimi barabarani na nimeachana  naye na kuelekea kwenye kituo cha daladala.

Nikajiambia kwamba iwapo mawazo yangu ni sahihi,  kama nitachelewa hapo kituoni kwa dakika chache tu, mume wangu angewasili na kunikamata.

Kama daladala ya kwenda Mwahako ingechelewa, ningeondoka haraka kituoni hapo na kwenda kupanda bodaboda. Lakini kwa bahati  njema wakati nawaza vile, nikaoina daladala inakuja.

Ilikuwa imejaza abiria na mimi nilikuwa sipandi  daladala ambayo abiria wamesimama lakini kwa kutaka kumkimbia mume wangu nilijipakiahivyo hivyo.  Daladala ikaondoka.

Niiporudi nyumbani kwa mganga sikukuta watu pale uani, nikaingiachumbani mwangu haraka na kuuweka mfuko wangu kitandani.

Baada ya kuuweka mfuko huo nikatoka tena kwenda  msalani. Wakati natoka msalani ndio nikakutana na mke mkuu wa mganga.

“Oh umesharudi?” akanniuliza.

“Nimerudi dada….”

“Umerudi  saa ngapi?”

“Nimerudi muda  huu huu tu”

“Hawajambo?”

“Hawajambo”

Mganga alikuwa kwenye chumba cha mke mkuu. Aliposikia sauti yangu akatoka na kuniuliza.

“Umesharudi?”

“Nimerudi, nilikuwa nimekwenda  msalani”

“Huyo uliyekwenda kumsalimia hajambo?” Mganga aliniuliza hivyo kwa kuzuga ili wake zake wasijue kama nilikwenda  madukani.

“Hajambo, anawasalimia”

Mganga huyo akajifanya kama anakwenda msalani. Nilijua kwamba alikuwa anavunga tu ili mke wake asijue kuwa alitoka chumbani baada ya kusikia sauti yangu. Alitaka mke wake ajue kuwa alitoka chumbani ili aende msalani.