Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dili iliyokufa - 37

HADITHI - 38 Pict

ILIPOISHIA

Aliponiambia hivyo  nikamshukuru na kumuahidi kuwa nitashirikiana nao katika raha na taabu.

“Sitamuheshimu mume wangu peke yake, nitawaheshimu hata  nyinyi wake wenzangu mlionitangulia” nikamwambia.

Mke mdogo naye akanikaribisha  na kuniambia amefurahi kuona wamepata mwenzao  tena msichana.  Naye akaahidi kushirikiana na mimi na kunipa muongozo nitakaouhitaji.

SASA ENDELEA...
 

Wanawake hao hawakuniuliza natokea wapi na kwanini  kwanza  nilikuwa mteja wa mganga huyo na kisha ghafla nikawa mke wake. Pia hawakuniuliza kama nilikuwa na mume au la.

Ilimradi  mimi niliona furaha na fahari  kutangazwa kuwa  mke wa mganga huyo. Hata sikuwaza  nitayawezaje maisha ya pale wakati  nilizoea kuishi  katika nyumba  za kisasa zenye mazingira ya kimjini.

Yaani mpaka leo ninaposimulia mkasa huu najisikia vibaya na moyo wangu unafadhaika lakini ni lazima niseme ukweli kuwa  yalinifika na sitayasau hadi siku ya kufa kwangu.

Unaweza kuona hilo lilikuwa tukio  kubwa na la kushangaza. Kumbe hilo lilikuwa dogo tu. Kubwa lilikuwa linanisubiri huko mbele ya safari.

Baada ya hapo nikaoneshwa chumba nitakachokuwa ninalala. Hakikuwa na kitanda. Kilikuwa na godoro la sufi ambalo lilitandikwa chini pamoja  na  chandarua kilichokuwa kimechakaa na kujaa moshi wa kibatari kilichokuwa kinatumika humo chumbani.

   Kwa vile siku ile ilikuwa siku yangu ya kwanza, wake wenzangu walikwenda kunionesha walikokuwa wanachota maji. Pale hapakuwa na bomba la maji. Bomba lilikuwa  mwendo wa nusu kilometa. Kila mmoja alikuwa na ndoo yake kichwani.

   Tulienda na kurudi safari sita. Tukajaza pipa la  maji kisha kila mmoja akachota maji yake ya kuoga usiku huo.

   Baada ya kuoga nikaingia chumbani mwangu. Kwa vile nilikuwa mkaza mganga mpya, zamu ya kulala na mume ilikuwa yangu.

   Chumba kilikuwa kinanuka mafukisho lakini niliyaona kama manukato. Ile shuka niliyopewa kutandika kitandani pamoja na ya kujifinika zilikuwa ni zile kaniki na shuka nyeupe ambazo mganga huyo kama ilivyo kwa waganga wengine huwaagiza wateja wao kama moja ya vitu vya uganga.

Shuka hizo inawezekana alifinikiwa mteja wakati unaaguliwa au zilivaliwa na mganga mwenyewe.

  Bila shaka baada ya shuka hizo kutumika kwenye uganga ziliwekwa bila kufuliwa na ndizo hizo nilizopewa mimi. Zilikuwa zikinuka harufu mbaya ya madawa na moshi wa sigara kali ambazo yule mganga hupenda kuvuta.

   Vile natandika shuka mojawapo kitandani, nilipiga chafya mara mbili kutoka  na ukali wa ile harufu. Baada ya kutandika. Nilijifunga kaniki nikashusha chandarua. Kwanza alitangulia kuingia mume wangu ndani ya chandarua kisha nikaingia mimi.

   Hakukuwa na mto. Mto ni ngumi yako. Mbu walikuwa wengi lakini walivumia nje ya chandarua. Hawakutupata.

  Kibatali kilikuwa kwenye kimeza kilichokuwa pembeni kikitoa moshi. Nikamuuliza mume wangu“Nikizime?”

   “Kiwache” akaniambia.

   Niligundua mle chumbani kulikuwa na panya wengi waliokuwa wakipita huku na huku. Nilikuwa na wasiwasi kwamba wangeweza kukikumba kile kibatali wakati tumelala  na kinaweza kusababisha nyumba kushika moto.

   “Panya hawatakikumba kile kibatari usiku?” nikamuuliza yule mganga.

   “Hawawezi kukikumba. Kwanza hao si panya”

   “Ni nani?”

   “Ni askari wangu. Hao ndio wanaolinda nyumba  yangu”

   “Panya wanaweza kulinda nyumba?”  nikamuuliza.

   “Hao si panya”

   “Ni nani?”

   “Ni majini”

   “Mmh…! Majini ndio panya?”

   “Wamejigeuza tu ili nijue kama wapo”

   “Kumbe….!

   “Ngoja niwafukuze waende zao” akaniambia  kisha akawambia wale pamya.

   “Haya nendeni, sisi tunataka kulala. Hatutaki kelele!”

   Nilimuona yule mganga kama mwehu anayezungumza na panya lakini baada ya hapo panya hao waloitoweka. Sikuwasikia tena.

   Mganga akajiingiza  ndani ile ya shuka,tukawa tumejifinika pamoja. Kila mara nilikuwa natoa uso wangu nje ya shuka na kupiga chafya kutokana na ukali wa ile harfufu.

   Kama kwamba yule mganga alijua ni kwanini nilikuwa napiga chanfya kwani alinyamaza kimya, hata akuniuliza “una nini?”

   “Wewe ndo umeletaa nuru mpya ndani ya nyumba yangu, umekuwa kama ua la moyo wangu” Mganga huyo akaniambia tukiwa ndani ya shuka tumekumbatiana.

   Licha ya kwenda kuoga, mwili wake ulikuwa ukinuka harufu ya sigara pamoja na mafukisho yake. Ile harufu ilifanya mdomo wangu ujae mate. Nilishindwa kuyatema. Nikayaacha yatoke yenyewe mdomoni kama ute.

   Mganga aliponimbia nimekuwa kama ua la moyoni mwake nilitaka kumjibu lakini nilishindwa kwa vile kinywani mwangu mlikuwa na mate, nikabaki  kutabasamu.

   Mganga huyo alinipa kazi pevu tukiwa ndani ya shuka lakini ningefanyaje wakati nilishakuwa mke wa mtu. Sikumkumbuka tena mume wangu na hata sikumuwaza akilini mwangu. Akili yangu ilikuwa imebadilika kabisa.

   Baada ya patashika na nguo kuchanika ya mimi  na mganga kwenye sita kwa sita tukalala. Usiku mwingi  nikazinduka usingizini. Mwenzangu alikuwa akikoroma. Mkoromo wake ulisikika hadi nje  ya chumba  na   kunisababishia hofu. Jinsi alivyokuwa anakoroma nilihisi kama sauti za vyura wawili waliokuwa wakishindana kukoroma.

   Sasa kizaa zaa hakikuwa kwenye mkoromo wa mganga huyo, wale panya walirudi tena usiku na bila shaka kelele zao ndizo zilizoniamsha usinngizini. Walikuwa wakipita huku na huko. 

   Kwa vile mganga huyo aliniambia panya hao walikuwa majini niliogopa sana. Kwa kweli sikulala tena hadi kunapambazuka.

   Wenzangu waligonga mlango na kuniita. Nikatoka. Niliwaona wameshika ndoo.

   Wakanisalimia kisha wakaniambia.

   “Kumekucha. Kachukue ndoo yako twende maji” Mke mkuu wa mganga akaniambia.

   Nikarudi chumbani nikavaa vizuri kisha nikatoka. Hapo sijaosha uso wala sijapiga mswaki. Nikaenda kuchukua ndoo yangu na kufuatana na wale wenzangu kueleka kwenye maji. Mzee nilimuacha bado amelala.

   Kulikuwa bado hakujapambazuka sawasawa. Tukaenda kuchota maji. Huko nako tulikuta foleni ya wenzetu. Tukasubiri hadi zamu yetu ilipofika tukachota maji na kurudi nyumbani.

   Tuliyamimina maji hayo kwenye pipa na kwenda kuchota tena. Kwa jumla tulikwenda safari sita,pipa likajaa. Bi mkubwa akaanza kumenya mihogo na kuibandika jikoni.

   Mihogo ilipoiva akabandika sufuria ya chai. Chai ilipochemka aliitia kwenye chupa kisha akabandika uji. Uji ulipokuwa tayari akamchemshia maji ya moto mume wetu ili aende akaoge. Huyo bwana  alikuwa haogi maji baridi asubuhi.

   Wakati mwanaume huyo anaoga, mimi nilikuwa naosha vyombo.

   Sikujua, kumbe ile chai ilikuwa ni ya mume wetu peke yake, sisi tulikuwa tunakunywa uji.

   Mimi niliyezoea kuoga, nilioga saa nne, wenzangu walikuwa wakiendelea kufanya kazi. Laiti ningekuwa na akili timamu ningegundua yale maisha yalikuwa ni ya kitumwa. Lakini kwa vile nilikuwa kama niko kwenye ndoto sikuwa nikielewa chochote. Kila kitu nilikiona sawa.

   Mchana tulipika pure. Ziliiva saa kumi jioni. Njaa ilikuwa inaniuma. Nilishazoea kula  saa saba. Baada ya kula pure nikaenda kuosha vyombo. Nilitaka kwenda kuoga tena, bi mkubwa akanikataza.

   Aliniambia eti  ninaharibu maji.

   “Sisi hapa tunaoga mara moja tu” akaniambia.

   “Na mimi nioge mara moja tu?” nikamuuliza.

   “Kama unaamua kuoga mchana basi utakuwa unaoga mchana tu. Si unaona maji yenyewe ni ya shida”

   “Basi sitaoga, Nitaoga usiku. Asubuhi nitanawa uso tu na kuosha miguu”

   Ndipo nilipojua kanuni za pale nyumbani kwamba watu huoga mara moja tu, tena niligundua kuwa  mtu anaoga kwa  kutumia sabuni kwa wiki mara mbili. Mara nyingine anaoga maji matupu. Sabuni iliyokuwa ikitumika ni ile ya kufulia, kipande cha sabuni ya mche.

   Kwa upande mwingine pia  tulikuwa tukishirikishwa katika masuala ya uganga kama vile kwenda kuchimba mizizi ya dawa au kuchemsha dawa na vitu kama hivyo.

   Baada ya siku tatu nilimlalamikia yule mganga ambaye kwa wakati ule alikuwa ndiyemume wangu kuwa sikuwa na baadhi ya vitu nilivyokuwa ninavihitaji kama vile nguo za ndani za kutosha na nisingeweza kuazima  kwa wenzngu. Pia  nilimwambia sikuwa na baadhi ya vipodozi ambavyo  nilizoea kuvitumia.

   “Itabidi uende ukanunue” Mganga akaniambia.

   “Sawa, nitakwenda kununua”

   “Utahitaji  shilingi ngapi”

   “Elfu thelathini tu itatosha”

   Kabla ya hapo nilikuwa nikiomba hadi shilingi laki mbili kwa  mume  wangu niliyemkimbia na pia  niiliona hazitoshi lakini huko kwa mganga niliona elfu thelathinizingetosha. Nilikuwa nimebadilika sana.

   Mgannga akanipa shilingi elfu thelathini.

   “Sikiliza nikwambie. Wakati unatoka usiwambie wenzako  kuwa unakwenda kununua vitu. Wambie unakwenda kumsalimia ndugu yako fulani. Umesikia?”

   “Sawa. Sitawambia”

   “Ukiwambia wataona wivu halafu wataanza  kukuchukia”

   “Kweli”