Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dili iliyokufa - 36

HADITHI - 35 Pict

ILIPOISHIA

 Nikakaa kwenye jamvi. Kimoyomoyo nilikuwa najiuliza kwanini hawa  waganga wa kienyeji hawaboreshi mazingira yao wakati wanapata pesa  nyingi. Kila siku tunakaa chini tu.

   Mganga alikuwa amekaa mbele yangu.

   “Haya niambie umefanya zile dawa?”  mganga  huyo akaniuliza.

   “Nimefanya”

   “Umemtilia kwenye chakula?”

   “Nimemtilia  kwa siku tatu kama ulivyoniagiza”

   “Na wewe umekula hicho chakula?”

   “Ilibidi nile ile siku ya kwanza. Unajua niliitia kwenye mchuzi. Akaniambia mchuzi mchungu, hebu uonje. Nikauonja”

   “Lakini haina madhara hata kama  umeuonja”

   “Na siku ya pili nilimtilia kwenye juisi akanywa kidogo kisha akaninywesha na mimi.”

SASA ENDELEA...

“SAWA kabisa. Maana yake ni kuwa anakupenda”

   “Kweli eh?”

   “Kweli kabisa.  Anachokula yeye anataka ule na wewe”

   “Tuseme hivi sasa ananipenda?”

   “Wewe ndio uniambie kwa sababu ndiye unayeishi naye”

   “Mimi naona bado kidogo. Jana nimemuomba pesa ameniambia mpaka mwisho wa mwezi”

   “Sasa wewe ulitakaje?”

   “Nilitaka anipe hapo hapo”

   “Sasa kama  hana atakupa nini?”

   “Sio kama hana. Pesa anazo isipokuwa anajishauri tu kuwa anipe au asinipe”

   “Hana ujanja, tutashughulika naye mpaka tutamuweka sawa”

   “Mimi nataka vile nikimuomba pesa anipe hapo hapo”

   “Huko ndiko unakoelekea, usiwe na wasiwasi. Wewe kidogo una nuksi ya jini, tukiiondoa tu, atakuona kama kioo”

   “Kumbe nina nuksi eh?”

   “Unayo nuksi ya jini dume, itabidi leo twende huko mzimuni tukaiondoe”

   Hata sikumuuliza huko mzimuni ni wapi na kama ni lazima twende huko,  nikajikuta nikimjibu.

   “Haya  twende”

   “Subiri niandae dawa zangu” 

   Baada ya robo saa hivi akaniambia.

   “Tayari, sasa tunaweza kwenda”

Alikuwa  ameshika  mfuko wake uliokuwa na dawa.

   Tukatoka. Aliwambia wale wanawake kwamba tulikuwa tunakwenda mzimuni.

   Tukaanza safari ya kuelekea huko mzimuni. Tulitembea kwa miguu nikidhani palikuwa karibu. Kumbe palikuwa na kipande kirefu cha  mwendo.

Palikuwa ni kwenye pori. Hakukuwa  na  barabara isipokuwa njiaza kupita kwa miguu.

Tulitokea mahali ambapo palikuwa na mibuyu mitatu iliyoota pamoja na kuunda alama ya V huku ikiwa imezungukwa na kichaka. Kando ya ile mibuyu palikuwa na nyumba ndogo iliyojengwa kwa miti na udongo na kuezekwa kwa makuti ya mnazi.

“Tumeshafika. Mzimu wetu ndio huu hapa” Mganga akaniambia.

Palikuwa na kijinjia chembamba kilichoelekea ndani ya kile kichaka  kilichoundwa na ile mibuyu. Mganga akasimama  mbele ya kile kichaka kisha akapiga hodi.

Baada ya kupiga hodi akaingia ndani ya kichaka hicho.

“Na mimi nije?” nikamuuliza.

“Nisubiri hapo hapo halafu nitakwambia uje”

“Sawa” nikamjibu.

Mganga aliingia kwenye kile kichaka na kupotea. Akiwa humo ndani ya kichaka niliisikia sauti yake akizungumza. Sikuweza kujua alikuwa akizungumza na watu au na majini.

Nilimsikia akisema.

“Nyinyi watawala wa mzimu huu. Nimewaletea mgeni mwenye shida zake. Nawaomba musaidie kutatua matatizo yake na mumewe”

Sauti ya mganga ikapotea kidogo kisha nikaisikia tena ikisema.

“Shida yake, hasikizani na mume wake. Nimeona ana nuksi inayosababisha mume wake asimpe pesa na pia asiwe na mapenzi naye”

Sauti ya mganga ikapotea tena. Baada ya sekunde chache ikasikika tena.

“Mnasema nuksi yake haiwezi kuondoka mpaka kwa kitendo mashuhuri?” sauti ya mgana ilikuwa kama inayouliza.

Nikahisi huenda alikuwa akisemeshana  na majini wa mzimu huo. Lakini sauti za majini hao alikuwa akizisikia yeye mwenyewe.

Sauti yake Ikasikika tena.

“Kitendo mashuhuri kama kitendo gani?”

Pakapita ukimya mwingine wa sekunde chache kabla ya sauti ya mganga huyo kusikika.

“Yaani mimi nifanye naye tendo la ngono hapa hapa kwenye mzimu?” alikuwa kama anauliza.

Halafu baadaye akasema.

“Nimeelewa” Akaongeza tena.

“Basi nitamwambia mlivyoniambia. Hakuna tatizo. Nyinyi ndio waganga”

Baada ya hapo sikuisikia  tena sauti ya mganga huyo. Nilikuja kumshitukia mganga huyo ametokeza pale kwenye kinjia.

“Njoo” akaniambia huku akirudi alikotoka.

Nikamfuata. Mwili wangu ulikuwa umejaa  baridi ya hofu. Yale maneno ambayo alikuwa akisemeshana na hao majini wake niliyaelewa. Alitakiwa afanye tendo la ngono na mimi. Hilo peke yake likanitia baridi.

La pili lililokuwa llimenitia  hofu ni lile aeneo tuliloingia, lilikuwa linatisha. Baada ya kupiga  hatua chache tu tukatokea mahali pa wazi. Ukiwa mahali hapo unakuwa kama upo ndani ya kibanda cha nyasi. Kutaza kibanda hicho ni mashina ya ile mibuyu mitatu.

Ile mibuyu ilikuwa imetundikwa kila kitu kinachotisha. Ilikuwa imetundikwa mafuvu ya watu na  wanayama. Mifupa ya mikono na miguu, ilikuwa ikining’inia  kilaupande.

Ngozi za wanyama, shuka za rangi mbali mbali na tunguri, vilikuwa vimening’inizwa kwenye mibuyu. Kulikuwa na makorokoro mengine ambayo sikuyaelewa yakiwemo majongoo makubwa yaliyozagaa katika  eneo lote.

Katikakati ya eneo  hilo palikuwa na kitu kama kichanja kilichotemgezwa kwa miti. Juu ya  kichanja hicho palitandikwa ngozi iliyokuwa imewambwa kamangoma.

Mganga aliponiingiza katika eneo  hilo aliniambia.

“Sasa unatakiwa uvue nguo zako zote, ulale hapa juu ya ngozi ushughulikiwe”

Nilishindwa hata kuuliza nishughulikiwe nini, nikajikuta ninavua  nguo bila kupenda nikabaki uchi wa mnyama! Mganga aliniona kila kitu  bila kificho. Nikamuona na  yeye anavua nguo zake na kubaki uchi wa mnayama!

Alichukua ule mfuko aliokwenda nao akatoa tunguri  na kujipaka  dawa sehemu yake ya siri kisha akairudisha ile tunguri kwenye mkoba.

“Sasa lala  kichalichali hapa juu ya ngozi, tuondoe matatizo yako”

Nikapanda pale kwenye  kichanja na kulala kichalichali. Mganga naye akapanda. Kilichofuatia hapo umeshakijua. Naona aibu hata kukieleza. Baada ya hapo mganga akaniambia nivae nguo zangu nikavaa, na yeye akavaa nguo zake.  Akaniambia.

“Shika huu mfuko, twendezetu”

Nikaushika ule mfuko wake wenye vifaa vya uganga tukatoka katika  lile eneo na kuanza mwendo mwingine wa kurudi.

Tulirudi mpaka nyumbani kwa mganga. Tulipofika ndio sikutaka  kuondoka tena nyumbani kwake.. Nikabaki hapo hapo. Sikukumbuka tena kule kwa mume wangu.

Amini usiamini nilihshinda pale hadi jioni nikala ugali na wale wanawake ninaowakuta pale nyumbani.

Kile kitendo tulichokwenda kukifanya kule, kilibadili mawazo yangu kabisa. Nikajiona nimekuwa mke wa mganga.

Yule mganga kwa  kujua alichokifanya, hakuniuliza ni kwanini siondoki pale nyumbani kwake.

Ajabu ni kwamba baada ya kula ugali, nilichukua vyombo na kuuliza mahali pa kuoshea vyombo. Nilipooneshwa nikaenda kuviosha.

Ilipofika usiku mganga  aliwaita wale wanawake ninaowakuta pale nyumbani. Siku za kwanza nilipokuwa nakuja pale nyumbani nilikuwa ninakuta wanawake watatu. Lakini baadaye nikawa nawakuta  wanawake wawili.

Wanawake hao walipoitwa na mganga, wakaambiwa wakae chini pamoja na mimi. Tukakaa. Mganga akanitambulisha kwamba wale walikuwa ni wake zake. Mke mkubwa na mke mdogo.

Aliniambia mke mkubwa alikuwa anitwa Mwanasozi. Mke mdogo aliitwa. Mwadawa.

Mganga baada ya kunitambulisha wale  wanawake,na wao akawatambulishakwangu. Aliwambia mimi nilikuwa mke wake wa tatu.

“Pale mlipoona tunaondoka. Tulikwenda kufunga ndoa mzimuni. Niliambiwa na mzimu nimuoe. Kwa hiyo  mtakuwa mnakaa naye hapa”

Yale maneno yalikuwa  ya uongo lakini ajabu ni kuwa yule mganga  alipokuwa akiwaeleza wake  zake  uongo huo, nilikuwa nacheka cheka  kwa  furaha.

Majina ya wanawake hao sukuwahi kuyasikia popote maishani mwangu. Baada ya mganga kumaliza maelezo yake, Mwanasozi mke mkubwa wa mganga huyo  akanikaribisha kwa  kuniambia.

“Tunakukaribisha kwa  mikono miwili mwenzetu. Kama  ulivyofahamishwa sisi ndio wake wenzako. Tutakuwa  pamoja, tutashirikiana na kusaidiana na mume wetu katika kazi zake ikiwemo  kumhudumia yeye”

Akaendelea kuniambia.

“Kwa sasa hivi wewe ni mgeni. Unaweza kuona taabu kuishi hapa lakini baadaye utazoea kwani hata sisi tulikuwa hivyo hivyo lakini baadaye tumezoea, tunajiona tuko nymbani”

Aliponiambia hivyo  nikamshukuru na kumuahidi kuwa nitashirikiana nao katika raha na taabu.

“Sitamuheshimu mume wangu peke yake, nitawaheshimu hata  nyinyi wake wenzangu mlionitangulia” nikamwambia.

Mke mdogo naye akanikaribisha  na kuniambia amefurahi kuona wamepata mwenzao  tena msichana.  Naye akaahidi kushirikiana na mimi na kunipa muongozo nitakaouhitaji.