Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zuchu anavyopita njia za Mondi kimtindo

Zuchu Pict
Zuchu Pict

Muktasari:

  • Na sasa ikiwa ni miaka minne tangu kusainiwa, Zuchu, binti wa Khadija Kopa anaendelea kupita njia za bosi wake, Diamond Platnumz kwa lengo la kuhakikisha muziki wake unakua na kufika mbali hasa kimataifa.

MWIMBAJI wa Bongofleva, Zuchu ambaye ni msanii wa pili wa kike ndani ya WCB Wasafi baada ya Queen Darleen, amekuwa na mafanikio makubwa katika kipindi kifupi ukilinganisha na wasanii wengi waliosainiwa katika lebo hiyo.

Na sasa ikiwa ni miaka minne tangu kusainiwa, Zuchu, binti wa Khadija Kopa anaendelea kupita njia za bosi wake, Diamond Platnumz kwa lengo la kuhakikisha muziki wake unakua na kufika mbali hasa kimataifa.

Zuchu ndiye msanii wa kwanza kutambulishwa na kuachia EP, I Am Zuchu (2020), amefanya kolabo na wasanii wakubwa, namba zake za mauzo mtandaoni zipo juu na ameshinda tuzo zaidi ya 10 zikiwemo saba za muziki Tanzania (TMA). 

Hata hivyo, katika mafanikio hayo nyuma yake kuna uwepo wa Diamond, lakini kubwa zaidi ni kile kinachoonekana ni uwezo wa Zuchu kujiongeza, yaani kupita njia zile alizopita Diamond, mshindi wa tuzo tatu za MTV EMAs.

ZU01
ZU01

Kuna mambo mengi Diamond amefanya katika muziki wake na ukija kutazama upande wa pili kwa Zuchu unayakuta, ni kuanzia wanavyotoa nyimbo zao hadi kuzitangaza.

Mathalani Juni 2023, Zuchu aliachia video ya wimbo wake ‘Nani Remix’ akimshirikisha Innoss’B kutokea DR Congo, katika video hiyo ameonekana mama yake mzazi, Khadija Kopa.

Ikumbukwe Khadija Kopa ambaye ni Malkia wa muziki wa Taarabu nchini Tanzania alianza kazi ya sanaa mwaka 1990 katika kikundi cha Culture Musical Club huko visiwani Zanzibar.

Katika video hiyo Kopa amecheza kama mzazi ambaye anaenda kumuodhesha binti yake (Zuchu) katika famili ya kifalme, na mwishowe anavikwa taji la umalkia.

Kitendo cha Zuchu kufanya video na mama yake ni mwendelezo tu wa kile alichofanya Diamond mwaka 2015 ambapo mama yake mzazi, Bi Sandra maarufu kama Mama Dangote alitokea kwenye video ya wimbo wake, Utanipenda.

ZU02
ZU02

Na katika video hiyo Mama Dangote alicheza uhusika wa maisha atakayoishi siku ambayo Diamond atakapofilisika kimuziki na kiuchumi na aliyekuwa mpenzi wake na mzazi mwenzake, Zari The Bosslady alitokea pia.

Hakuna ubishi kuwa Zuchu anataka kufanikiwa kama Diamond au kurithishwa mafanikio hayo. Hiyo ni kwa sababu anaendelea kufanya kolabo na wasanii ambao Diamond tayari alishafanya nao kazi hapo awali.

Mfano ni staa wa Nigeria, Adekunle Gold ambaye alishirikishwa na Diamond katika wimbo wake ‘Sona’ kutoka kwenye EP yake ya kwanza, First of All (2022) iliyotoka ikiwa na nyimbo 10.

Baadaye Zuchu akaja kumshirikisha Adekunle Gold katika wimbo wake, Love (2022), muda mfupi baada ya kufanya vizuri na mradi wake, 4:4:2 uliokuwa na nyimbo mbili, Fire na Jaro.

Zuchu haukuishia hapo, ndipo akahamia kwa Innoss’B ambaye tayari alishafanya kazi na Diamond katika wimbo, Yope Remix (2019) ambao ndio wimbo wa Diamond wenye namba kubwa YouTube.

Kwa kifupi baada ya kuona Diamond kafanya remix na Innoss’B, naye Zuchu akafanya hivyo hivyo, anapita tu njia za Diamond kimtindo, kama haendi lakini ndio anaondoka hivyo na kuzidi kuvuna mashabiki wa kazi zake.

ZU03
ZU03

Utakumbuka Yope Remix ndio wimbo wa Diamond wenye mafanikio makubwa katika mtandao wa YouTube ambapo video yake imetazamwa (views) zaidi ya mara milioni 238, hii ndio video pekee ya muziki iliyotazamwa zaidi Tanzania na Afrika Mashariki.

Katika mradi wake, 4:4:2 uliotoka Julai 2022, Zuchu aliweka wimbo ‘Fire’ ambao anadai alipanga kumshirikisha Diamond lakini tayari alishamshirikisha katika nyimbo zake mbili hapo awali ambazo ni Litawachoma (2020) na Cheche (2020).

Lakini tayari naye Diamond alishwahi kutoa wimbo unaoitwa ‘Fire’ hapo Novemba 2017 akimshirikisha Tiwa Savage wa Nigeria, ni wimbo aliokuja kuujumuisha katika albamu yake ya tatu, A Boy From Tandale (2018). 

Zuchu aliamua kuupa mradi wake huo jina la 4:4:2 kutokana wimbo wake wa kwanza ‘Fire’ una herufi nne, pia wa pili ‘Jaro’ una herufi nne, hivyo kutoka kwa pamoja zote mbili zipo kunakamilisha maana ya 4:4:2.

Ikumbukwe wakati Diamond akiwa ndiye msanii wa kiume wa Bongofleva anayeuza zaidi kwenye majukwaa ya kidijitali ya kutiririsha (streams) muziki, Zuchu ndiye msanii anayefanya hivyo upande wa wasanii wa kike akiwa bado hajatoa albamu.