Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Si mchezo… Mondi kawabeba sana wasanii hawa kimtindo!

DIAMOND Pict

Muktasari:

  • Kutokana na sababu hiyo na nyinginezo, imesababisha Diamond kushirikishwa na wasanii wengi hasa wale wa Bongo Fleva tangu mwaka 2012 hadi 2025, na hii ni orodha ya wasanii baadhi waliomshirikisha Diamond kwenye nyimbo zao kuanzia mbili.

SABABU ya ushawishi na ukubwa wa chapa yake katika muziki, wasanii wa ndani na nje wamekuwa wakipigana vikumbo ili kufanya kolabo na Diamond Platnumz maana kila ambaye alipata nafasi hiyo, basi wimbo wake ilipata mapokezi mazuri.

Kutokana na sababu hiyo na nyinginezo, imesababisha Diamond kushirikishwa na wasanii wengi hasa wale wa Bongo Fleva tangu mwaka 2012 hadi 2025, na hii ni orodha ya wasanii baadhi waliomshirikisha Diamond kwenye nyimbo zao kuanzia mbili.

DIA 01

Jux - Sugua & Ololufe Mi

Hadi sasa Jux anayefanya vizuri na EP yake, A Day To Remember (2025), amemshirikisha Diamond katika ngoma zake tatu, Sugua (2019), Enjoy (2023) na Ololufe Mi (2024), zote nikitengenezwa na S2kizzy kutokea studio za Pluto Republic.

Utakumbuka video ya wimbo 'Enjoy' imetazamwa zaidi ya mara milioni 100 YouTube na kumfanya kuwa msanii wa nne Bongo kuwa na video yenye nambo hizo baada ya Diamond (Yope Remix, Inama, Waah!, Jeje na Nana), Harmonize (Kwangwaru) na Zuchu (Sukari).

DIA 02

Mbosso - Baikoko & Yataniua

Kutokana na kuvunjika kundi la Yamoto Band, Mbosso alijiunga na WCB Wasafi hapo Januari 2018, kupitia albamu yake ya kwanza,

Definition Of Love (2021) aliweza kumshirikisha Diamond katika nyimbo mbili, Baikoko na Karibu.

Haikuishia hapo, katika EP yake ya kwanza, Khan (2022) iliyochaguliwa kuwania tuzo za TMA 2022, Diamond akapewa nafasi tena kupitia wimbo 'Yataniua' ambao ulileta utata kwa madai umefafana na ule wa Asake wa Nigeria, Peance Be Unto You (2022).

DIA 03

Shetta - Nidanganye & Kerewa

Kutoka kuwa dansa Misifa Camp kwa Dully Sykes hadi kuishika Bongofleva haikuwa kazi rahisi kwa Shetta, ila kolabo yake ya kwanza na Diamond, Nidanganye (2012) ikafanya vizuri sana na kumfanya kusahau misoto maana ilimpa maokoto sio kitoto.

Mafanikio ya wimbo huo yakapelekea Shetta kumshirikisha Diamond katika wimbo mwingine, Kerewa (2014) ambao video yake iliyofanyika Afrika Kusini kwa Director Godfather iligharimu Dola10,000 ikiwa ni video ya kwanza kwa Shetta kutoa fedha nyingi.

DIA 04

Lava Lava - Far Away & Kibango

Mnamo Mei 2017 ndipo Lava Lava alitambulishwa WCB Wasafi akiwa ni msanii watano baada ya Harmonize (2015), Rayvanny (2016), Queen Darleen (2016) na Rich Mavoko (2016), huyu alipanda daraja maana mwanzo alikuwa katika bendi ya Diamond.

Ila ilimchukua muda mrefu hadi kufanya kazi na Diamond sababu walianza kutoa nyimbo za lebo, Zilipendwa (2017), Jibebe (2018) na Quarantine (2020), ndipo kolabo zao zikafuata, Far Away (2021), Bado Sana (2021), Tuna Kikao (2023) na Kibango (2024).

DIA 05

Chid Benzi - Mpaka Kuche & Tunaishi Nao

Katika historia Diamond ndiye wa kwanza kumshirikisha Chid Benzi ambaye alisikika katika wimbo wake 'Nalia Na Mengi' kutoka katika albamu yake ya kwanza, Kamwambie (2010) ambayo ndio hasa ilimtoa kimuziki.

Baada ya kupitia changamoto za kimaisha, Chid Benzi alitaka kurudi kwa kushindo ndipo akampa shavu Diamond na AY katika wimbo wake, Mpaka Kuche (2014), na baada ya takribani miaka 10 wakatoa ngoma nyingine, Tunaishi Nao (2023).

DIA 06

Harmonize - Bado & Kainama

Staa huyo wa Konde Music Worldwide akiwa bado ndani ya WCB Wasafi, alimshirikisha Diamond katika nyimbo tatu, mbili kati ya hizo ni Bado (2016) na Kwangwaru (2018) ambao ndiyo wa kwanza kwake kwa video yake kutazamwa mara milioni 100 YouTube.

Haikuishia hapo, Harmonize akaja kumpa shavu Diamond na Burna Boy wa Nigeria katika wimbo wake 'Kainama' unaopatikana katika EP yake kwanza, Afro Bongo (2019) ambayo iliwakutanisha wasanii wengine kama Mr. Eazi, Patoranking na Yemi Alade.

DIA 07

Linex - Nitaificha Wapi & Salima

Wengi watawakumbuka Linex na Diamond kwa kufanya kazi pamoja katika mrandi wa Kigoma All Stars ulitoa wimbo maarufu, Leka Dutigite (2012) wakiwa na Mastaa wengine kama Mwasiti, Banana Zorro, Ommy Dimpoz, Baba Levo, Chege, Peter Msechu n.k.

Kabla ya hapo, Linex alikuwa amemshirikisha Diamond katika wimbo wake, Nitaificha Wapi (2012), kisha ikafuata ngoma nyingine, Salima (2015) ambayo video yake ilileta mgogoro kati ya Director Adam Juma na Linex ambaye alidai haikutoka vizuri. 

DIA 08

Zuchu - Litawachoma & Walewale

Baada ya hapo Aprili 2020 kutambulishwa WCB Wasafi akiwa ni msanii wa pili wa kike baada ya Queen Darleen, haikuchukua muda mrefu Zuchu aliweza kumshirikisha Diamond katika nyimbo zake mbili zilizotoka kwa mpigo.

Nyimbo hizo ni Cheche (2020) na Litawachoma (2020) ambazo ndizo hasa zilimtangaza zaidi kimuziki, kisha baadaye sana akaja kumshirikisha tena Diamond katika ngoma yake 'Walewale' kutoka katika albamu yake ya kwanza, Peace and Money (2024).

DIA 09

Nay wa Mitego - Muziki Gani & Mapenzi au Pesa

Rapa huyo kutokea Free Nation alimshirikisha Diamond kwenye ngoma yake, Muziki Gani (2013) ambayo ilifanya vizuri sana na kumuongezea mashabiki wengi hasa wa kike na kumpatia dili kutoka moja ya kampuni za simu za mkononi.

Baadaye Nay akaona kufanya kolabo na Diamond ni bidhaa inayouzika kwa urahisi ndipo wakaachia wimbo mwingine, Mapenzi au Pesa (2016) ingawa haukuweza kufanya vizuri kama ule wa mwanzo na hata video yake hawakuitoa. 

DIA 10

Rayvanny - Mwanza & Nesa Nesa

Hadi sasa Rayvanny na Diamond ndio wasanii wa Bongofleva walioshirikiana zaidi kwa kipindi cha miaka nane iliyopita, wametoa pamoja nyimbo kama Salome, Iyena, Mwanza, Tetema, Timua Vumbi, Amaboko, Woza, Nitongoze, Yaya na Nesa Nesa

Rayvanny amemshirikisha Diamond katika nyimbo nane, Mwanza (2018), Tetema (2019), Timua Vumbi (2019), Amaboko (2020), Woza (2020), Yaya (2023), Nesa Nesa (2024) na Nitongoze (2022) ulioshinda tuzo ya TMA 2022 kama Wimbo Bora wa Kushirikiana.