Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zuchu anatazamwa zaidi YouTube Kenya kuliko Tanzania

INAWEZA kushangaza lakini ndivyo ilivyo, Staa wa Bongofleva anayefanya vizuri chini ya WCB Wasafi, Zuchu anatazamwa zaidi katika mtandao wa YouTube nchini Kenya kuliko hata kwao Tanzania.

Utakumbuka Zuchu ndiye msanii wa kike aliyetazamwa zaidi YouTube Tanzania kwa muda wote akifuatiwa na Nandy, kwa ujumla anashika nafasi ya nne baada ya Diamond Platnumz, Rayvanny na Zuchu.

YouTube ni mtandao wa kucheza video ulioanzishwa Februari 14, 2005, huko San Mateo, California nchini Marekani na kwa miaka sasa umekuwa ukiwalipa wasanii wa muziki kwa kuweka matangazo katika maudhui yao.

Data za YouTube zinaonyesha katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, video za Zuchu zimetazamwa (views) zaidi ya mara milioni 75 YouTube kwa Kenya tu, wakati nyumbani kwao, Tanzania amepata 'views' milioni 28 ikiwa asilimia 21 ya kile alichopata Kenya.

Jiji la Nairobi ndilo linaongoza kwa kumpatia Zuchu 'views' nyingi zaidi zikiwa ni milioni 50, huku jiji lake la nyumbani, Dar es Salaam likifuatia ambapo limempatia 'views' milioni 26 kwa kipindi hicho.

Zuchu ambaye 2022 alipata jumla ya 'views' milioni 160 YouTube, hii ni ishara kuwa anatengeneza fedha nyingi katika mtandao huo Kenya ukilinganisha na nchi nyingine.
Tovuti ya Dittomusic.com, wanakaridia msanii anapofikisha 'views' milioni 1 YouTube anaweza kutengeneza Dola690, wastani wa Sh1.6 milioni, hivyo utaona kwa kiwango gani Zuchu ana fedha zake nyingi Kenya.

Hata hivyo, kiasi hicho cha fedha kitategemea wanaotazama video husika wanatokea nchi gani maana kila nchi huwa na kiwango chake cha malipo kutokana na idadi ya wateja wanaopeleka matangazo kampuni ya Google ambao ndio wamiliki wa YouTube.

2021, Zuchu alikuwa ndiye msanii wa kike aliyetazamwa zaidi YouTube Kenya akipata 'views' zaidi ya milioni 67, huku mashairi (lyrics) ya wimbo wake, Sukari yakiongoza kwa kutafutwa katika mtandao wa Google nchini humo mwaka huo.
Na hadi kufikia nusu ya mwaka 2022 Zuchu alikuwa amepata zaidi ya 'views' milioni 55 YouTube akiwa ni msanii wa tano kutazamwa zaidi katika mtandao huo nchini  Kenya.

Hadi Juni 2023 video ya wimbo wa Zuchu 'Sukari' ilikuwa imepata zaidi ya 'views' milioni 36 Kenya na hadi sasa ndio video iliyotazamwa zaidi YouTube nchini humo kwa muda wote. Hadi sasa video hiyo imefikisha 'views' milioni 91.5, hivyo asilimia 32 ya jumla kuu inatoka Kenya.

Utakumbuka video hiyo iliyotoka Januari 30, 2021 anashikilia rekodi kama video ya msanii solo iliyotazamwa zaidi Afrika Mashariki na Kati, imetanguliwa na video ya wimbo wa Fally Ipupa (DR Congo), Eloko Oyo yenye 'views' milioni 92.6, hii ilitoka Aprili 7, 2017.

Video ya Sukari ambayo ndio iliyotazamwa zaidi Afrika 2021 ikipata 'views' zaidi ya milioni ya 60, pia ndio video iliyotazamwa zaidi Kenya kwa mwaka huo ikipata 'views' milioni 32.
Katika orodha ya video 10 Zuchu aliingiza video mbili, Sukari na Nyumba Ndogo iliyokamata nafasi ya saba, kwa ujumla Tanzania iliingiza video tano katika 10 bora na nne zilikuwa za WCB Wasafi, huku Kenya ikitoa video tano pia.
Utakumbuka katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, Zuchu ni msanii wa tatu wa kike kutazamwa zaidi YouTube akiwa na 'views' zaidi milioni 500.9, ametanguliwa na Sinach mwenye 'views' milioni 762.8 na Yemi Alade mwenye 'views' milioni 727.1.

Zuchu aliyetoka kimuziki Aprili 2020 baada ya kutambulishwa WCB Wasafi, amewapita wasanii kama Tiwa Savage mwenye 'views' milioni 468.5 na Ada Ehi 'views' milioni 422.8.
Ikumbuwe 2022, Zuchu alikuwa ndiye msanii wa kike aliyetazamwa zaidi YouTube nchini Tanzania akiufunga mwaka kwa kukusanya 'views' milioni 160, kwa ujumla alishika nafasi ya nne akiwa ametanguliwa na Diamond (views milioni 448), Rayvanny (milioni 207) na Harmonize (milioni 206).

Hata hivyo, Zuchu sio msanii pekee wa kike wa Afrika anatazamwa zaidi YouTube Kenya kuliko nchini mwake, kuna wengine na mmoja wapo ni Ayra Starr kutokea Nigeria.
Mfano Oktoba 2022 video ya wimbo wa Zuchu 'Kwikwi' ilipata 'views' milioni 1.2 YouTube Kenya, wakati Tanzania ilipata 'views' 700,000 tu, huku  Ayra Starr akipata 'views' 770,000 Kenya na kwao Nigeria akipata 'views' 400,000.

Utakumbuka wasanii wa Kenya waliotazama zaidi YouTube kwa muda wote hakuna hata mmoja aliyemfikia Zuchu, wasanii hao ni Otile Brown (views milioni 344.1), Sauti Sol (milioni 296.0), Willy Paul (milioni 223.9), Bahati (milioni 219.0), Diana B (milioni 153.7), Nyashinski (milioni 118.5), Khaligraph Jones (milioni 92.3) na Nadia Mukami (milioni 71.1).