Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wolper na ndoa zilizoingia shubiri

Wolper Pict

Muktasari:

  • Wolper ameliambia Mwanaspoti kuwa, baada ya kuandika kwenye akaunti yake ya Instagram kuwa ameachana na mume wake, Rich Mitindo, na yuko mbioni kufuatilia talaka, watu wengi wamempigia simu na wengine kuandika kwenye mitandao kuwa ni kiki, lakini sio kiki bali ni kitu cha ukweli.

“HII sio kiki” ndio kauli ya Jacqueline Wolper wakati akizungumza na mwanaspoti kuhusu taarifa ya kuvunjika kwa ndoa yake aliyoitoa hivi karibuni.

Wolper ameliambia Mwanaspoti kuwa, baada ya kuandika kwenye akaunti yake ya Instagram kuwa ameachana na mume wake, Rich Mitindo, na yuko mbioni kufuatilia talaka, watu wengi wamempigia simu na wengine kuandika kwenye mitandao kuwa ni kiki, lakini sio kiki bali ni kitu cha ukweli.

Nyota huyo wa Bongo Movie anasema amechoka kufanya siri kuhusiana na ndoa yake ndio maana ikamlazimu kuandika kwenye mtandao, na hili jambo sio la leo wala jana kikubwa watu waheshimu kile kitu ambacho amekiandika.

“Ifikie hatua watu waheshimu uamuzi unaofanywa na watu, na mimi huwa sifanyi kitu kwa mihemko wala kukurupuka, nina akili timamu na najitambua, sasa wale watu wanaolazimisha kuwa nilichoandika kwenye akaunti yangu ni kiki basi wanaweza kukaa pembeni kwenye jambo hili.

“Hii sio kiki, kwa umri niliofikia sio mtu wa kufanya jambo hadi nitumie kiki, sasa nifanye kiki ya kutaka kufanya nini? Kama biashara yangu ya Wolsher inajiendesha bila kiki,” anasema Wolper.

Januari 5, 2025 Wolper kupitia ukurasa wake wa Instagram alitangaza kuachana rasmi na mume wake huyo, ambaye wamejaaliwa kupata watoto wawili -- mmoja wa kike na mwingine wa kiume.

Aliandika: “Hellow Mashabiki zangu, marafiki na Watanzania wote mnao nitakia mema.

“Ni kwa masikitiko mengi sana mmekuwa mkinitumia message, links, na clips mbalimbali, huku mkinishauri, kuniombea na kunitia moyo. Nimepokea msg zenu zote kwa moyo wa shukrani sana. Na Mungu awabariki wote mnao nitakia mema, na hata wale wenye nia tofauti na njema pia mbarikiwe.

“Lakini naomba niwatoe wasiwasi na shaka juu ya furaha na amani ya moyo wangu. Mimi na mzazi mwenzangu Rich (Baba P) hatupo pamoja (TUMEACHANA). Nipo kwenye process za Divorce/Talaka. Hivyo, mashauri yote na huruma juu ya mambo yanayoendelea na mzazi mwenzangu, msiyalete kwangu tena. Ni mtu ambaye yupo huru kufanya chochote kinacho mpendeza.

“Na hii niseme tu si kwa ubaya haijalishi mtalipokeaje wengine lakini maisha halisi ya ndoa yangu nayajua mimi na mwenzangu kwahiyo tutabaki kuheshimiana kama wazazi na kulea watoto wetu lakini suala la mahusiano ya ndoa hilo halipo!

“Nawapenda sana nashukuru kwa msg zenu nyingi za kunitia moyo kutokana na mambo mnayoyaona huko lakini niwaambie tu mimi nipo sawa na muache kunihusisha na mambo yanayoendelea kwa mzazi mwenzangu kwasababu hayanihusu na nisingependa kuongelea hayo.”

WL 01

Wolper na Rich Mitindo walifunga ndoa hiyo Novemba, 2022 katika Kanisa la St. Peter’s lililopo jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, Wolper na Rich, si mastaa wa kwanza kuachana. Mwanaspoti linaorodhesha baadhi ya ndoa za mastaa ambazo ziliingia shubiri:


SHILOLE

Msanii na mjasiriamali, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amevishwa pete ya uchumba na anajiandaa kuingia katika ndoa yake ya nne baada ya ndoa zake tatu za awali kuvunjika.

Awali, aliolewa na dereva wa malori wakati akiwa na umri wa miaka 17, ambaye alikuja naye Dar es Salaam akitokea kwao Igunga ambako alikuwa tayari amepata mtoto wa kwanza. Akazaa mtoto mmoja kwenye ndoa hiyo, akiwa ni wa pili kwake. Baadaye mwaka 2009 akaachana na mwanaume huyo kwa talaka akimtuhumu kumpiga hadi kumdhuru mguu wake wa kulia.

Desemba 2017 ilikuwa ndoa ya pili kwa Shilole, ambapo alifunga na Ashraf Uchebe ambaye waliachana Oktoba 2020 baada ya kuvuja kwa picha zikimuonyesha akiwa amejeruhiwa usoni. Akaolewa ndoa ya tatu Aprili 2021 na aliyekuwa mpigapicha wake, Rommy 3D, ambaye ilipofika Mei 2024 wakaachana.


WL 02
WL 02

SHAMSA FORD

Hivi sasa Shamsa yuko kwenye ndoa na msanii mwenzake Hussein Lugendo ‘Mlilo’ na wamebarikiwa kupata mtoto mmoja. Lakini kabla ya ndoa hii, staa huyu wa filamu nchini, alifunga ndoa na Rashidi Said ‘Chidi Mapenzi’ ambaye ni mfanyabiashara wa maduka ya nguo Septemba 2016. Baadaye waliachana.


AUNT EZEKIEL

Staa wa filamu za Bongo, Aunt Ezekiel alifunga ndoa na Mtanzania aishie Dubai, Sunday Demonte, Oktoba 18, 2012. Katika ndoa hiyo, Demonte aliwakilishwa na rafiki yake, kisha sherehe ya nguvu ilifanyika baadaye Dubai.

Aunt Ezekiel aliamua kuachana na imani yake ya Kikristo na kuingia Uislam, ili afunge ndoa na  Demonte. Hata hivyo, miezi kadhaa baadaye ndoa hiyo ilianza kupoteza muelekeo hasa baada ya Aunt kuonekana Bongo muda mwingi kuliko nyumbani kwake Dubai, lakini baadaye ikathibitika wazi kuwa wameachana.


IRENE UWOYA

Staa wa filamu za Kibongo, Julai 11, 2009, alifunga ndoa na msakata kabumbu Hamad Ndikumana (sasa marehemu) katika Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam.

Baada ya ndoa hiyo, sherehe yenye hadhi ilifanyika kwenye Hoteli ya Giraffe View, Mbezi – Kawe, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu kibao wakiwemo mastaa mbalimbali.

Ndikumana, raia wa Rwanda, wakati akifunga ndoa na Irene,  alikuwa akiishi jijini Nicosia, Cyprus ambapo alikuwa akicheza mpira katika Klabu ya AEL Limassol na baadaye Apop Kinyras Peyias FC.

Baada ya ndoa yake, aliongozana na Irene hadi huko na kuanza maisha yao ya ndoa. Hata hivyo, ndoa hiyo ilivunjika Novemba, 2011 baada ya Irene mwenyewe kukiri kuwa amekuwa akiishi na Ndikumana kwa mazoea tu, lakini moyoni hakuwa akimpenda!


WEMA SEPETU

Mwaka 2013, aliwahi kufunga ndoa na mwanamume mmoja ajulikanaye kwa majina ya Yussuph Jumbe, lakini haikudumu, sababu ikitajwa mama yake mzazi Wema hakuitaka ndoa hiyo akidai Yussuf hatamfaa Wema.


STAMINA

Msanii wa hip-hop, Mei 2018 alifunga ndoa na mwanamke mmoja aitwaye Veronica Peter, ndoa hiyo ilifungwa katika Kanisa la Katoliki, Morogoro, lakini ilipofika Januari 2020 ndoa hiyo ilivunjika. Baadaye Stamina aliandika nyimbo kuzungumzia ndoa hiyo iliyovunjika.


WL 03

CHAZ BABA 

Msanii wa muziki wa dansi nchini kutokea bendi ya Twanga Pepeta, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ Septemba 2018 alibadli dini yake ya Ukristo na kuhamia Uislamu rasmi na kuitwa AbdulMalick, ili apate kuoa mke mwingine aitwaye Mariam Chavala baada ya mwanamke wa kwanza Rehema Sospeter ambaye alifunga naye ndoa mwaka 2013 katika kanisa la St. Peter Oysterbay jijini Dar es Salaam kutengana.

Chaz Baba ndoa yake na Mariam haikudumu muda mrefu na baada ya hapo Chaz aliamua kurudi katika dini yake na kumrudia mke wake wa kwanza Rehema Sospeter.


FLORA MVUNGI

Nyota huyo wa filamu yeye aliamua kubadili imani yake ya kidini kutoka Ukristo hadi kuwa Mwislamu ili mradi aolewe na Hamis Ramadhani ‘H-Baba’. Flora alifahamika kama Khadija na walibahatika kupata watoto wawili, Afrika na Tanzanite, walifunga ndoa mwaka 2013 na ilipofika 2017 ndoa hiyo ilivunjika.