Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hasira za Hanstone kwa Diamond hazimsadii

Muktasari:

  • Kama humfahamu Hanstone ni yule msanii wa kiume aliyeimba ‘vesi’ ya pili ya wimbo wa Iokote wa Maua Sama.

OYA! Kuna siku nilikuwa nimefulia vibaya sana. Kila nikiangalia pale ninapoweka vichenji vyangu kweupe kabisa hakuna kitu. Nilipotulia vizuri nikaanza kukumbuka majina ya watu ninaowadai.

Nikachukua simu nikawapigia na kweli nikapata chochote kitu. Kila mshikaji amewahi kupitia hali kama hii. Imenikumbusha mbali mpaka kwa msanii anayeitwa Hanstone.

Kama humfahamu Hanstone ni yule msanii wa kiume aliyeimba ‘vesi’ ya pili ya wimbo wa Iokote wa Maua Sama.

Na kama unamfahamu basi utakuwa na taarifa kwamba dogo aliwahi kuwa kwenye orodha ya wasanii waliokuwa wakisubiri kutambulishwa katika lebo ya WCB Wasafi chini ya Diamond. Tetesi na fununu zinasema kwamba kabla ya Wasafi kumtambulisha D-Voice, Hanstone ndiye aliyekuwa anatarajiwa, lakini kwa sababu fulani mipango hiyo haikutimia.

Sitaki tujikite sana kwenye hilo. Nataka tuzungumzie mvua ya maneno aliyoimwaga dogo huko Instagram kuhusu lebo hiyo pamoja na bosi wake. Ameandika mengi sana ikiwemo madai kwamba alikaa kwenye lebo hiyo kwa miaka mitatu bila kupata msaada wowote. Anasema lebo ilikuwa inamwambia alete nyimbo bila kujali anazirekodi wapi wala kumpa bajeti ya kufanya muziki. Na hata akizipeleka, bado walikuwa wanazikataa kwa hofu kwamba zitamfunika bosi wa lebo, yaani Diamond ambaye pia ni msanii.

Kuna sehemu Hanstone anaandika (nanukuu, lakini si neno kwa neno): “Nimeshiriki kwenye utunzi wa ngoma zako hata kama si kwa asilimia mia. Unajiita msanii namba moja Afrika, lakini unaogopa wasanii wenzako wenye vipaji vikubwa. Unaogopa kusajili msanii atakayekuzidi. Ndiyo maana hata ukagombana na wasanii wako wa zamani walipoanza kuonyesha juhudi na mafanikio yao ya kimuziki. Na ndiyo maana mpaka leo unasajili wasanii wa kawaida tu ukiamini hata wafanye nini hawawezi kukuzidi. Na intaneshino haitopata soko ng’o. You fear the real talent (unaogopa wasanii wenye vipaji vikubwa).”

Hanstone ni mmoja wa wasanii wangu pendwa. Wimbo wake 'Nitazoea' ulikuwa ndio wimbo niliousikiliza zaidi kwenye Spotify  2024. Hii inamaanisha naamini ana kipaji kikubwa. Lakini kusema ukweli, maneno yote aliyoyaandika yanaonekana kama hasira za wazi za mtu anayehisi dunia haimlipi kulingana na kipaji chake. Zaidi ya hayo, inaonekana anaamini matatizo yote yalianza baada ya kukosa nafasi ya kusajiliwa na Wasafi.

Hii ni kwa sababu kama Hanstone anadhani Diamond hakumsajili WCB kwa kuhofia kwamba atamfunika nini kinamzuia Hanstone kuwa mkubwa zaidi ya Diamond nje ya Wasafi? Kipaji chake hakikubaki Wasafi - bado anacho. Ndiyo tunarudi palepale kwenye hali ya kufulia na kuanza kukumbuka majina ya watu unaowadai.

Ningekuwa Hanstone ningekomaa na muziki wangu hasa ukizingatia kwamba bado ni kijana mdogo. Pia ningekubali ukweli kwamba si kila msanii atasajiliwa na Wasafi na wala siyo lazima uwe Wasafi ili ufanikiwe. Marioo, Nandy, Billnass, Jux, Abi, Young Lunya, Alikiba wote hawa hawajawahi kuwa Wasafi, lakini wanapiga maisha yao kwa kufanya muziki. Kama kweli ana kipaji ajikite kwenye kipaji chake na aachane na yaliyopita.