Whozu: Penzi la Wema limenisaidia kimuziki

Muktasari:
- Akizungumza na Mwanaspoti alisema amenufaika sana na umaarufu wa Wema ambae ni staa mkubwa katika tasnia ya filamu na mambo ya urembo.
MWIMBAJI wa Bongo Fleva, Whozu amesema kuingia katika uhusiano wa mapenzi na Wema Sepetu kumemsaidia mambo mengi katika maisha yake.
Akizungumza na Mwanaspoti alisema amenufaika sana na umaarufu wa Wema ambae ni staa mkubwa katika tasnia ya filamu na mambo ya urembo.
“Kuwa na mahusiano na Wema Sepetu kumenisogeza sana, kwa sababu ni staa wa filamu kutoka kitambo sana na hata kwenye mambo ya urembo. Mimi nilikuwa najulikana, lakini nilivyokutana na Wema kuna vitu vingi vimeongezeka katika maisha yangu,” alisema Whozu.
Pia Whozu amekana habari zinazodaiwa pindi wanapoachana na Wema huwa analia sana hadi kushindwa kula.
"(Kicheko) we hivi vitu nani amekwambia? Hakuna kitu kama hicho bana, sasa kwanini nilie jamani, ila huwa nakosa raha tu sababu ni mtu ambaye nimeshazoeana naye kwa kila kitu halafu mnakuja kutengana tena kwani vitu utakuta vya uwongo uwongo na hii ni kawaida, huwezi kufurahia kuachana na mtu unayempenda," alisema Whozu.