Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wastara bado alia na wanaume wakware wanaomtokea

Wastara

Muktasari:

Wastara alisema tangu kufiwa na mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’ amekuwa katika changamoto katika utendaji wake hususan utafutaji wa masoko baada ya kutengeneza filamu.

MWIGIZAJI mjane Bongo, Wastara Juma ‘Stara Super Woman’ bado anaandamwa na wanaume wenye uchu wa ngono na kumweka katika wakati mgumu.

Wastara alisema tangu kufiwa na mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’ amekuwa katika changamoto katika utendaji wake hususan utafutaji wa masoko baada ya kutengeneza filamu.

Msanii huyo alifafanua kuwa anapokuwa na kazi inamsumbua kwa sababu mara nyingi uuzaji wa filamu unatawaliwa na rushwa ya fedha sambamba na ya ngono.

Wastara alisema mtu anayejiheshimu na kukwepa ngono hutengwa na kuwekewa vikwazo ili afuate masharti ya wahusika.

“Najikuta nikiwa katika wakati mgumu sana, kwani nilipokuwa na Sajuki nilifanya kazi kwa asilimia 20 tu na faida niliiona, lakini sasa nafanya kazi kubwa lakini nabanwa katika mauzo, labda kwa sababu siutoi mwili wangu, najipenda na kujiheshimu na nawapenda watoto wangu,” alisema Wastara.