Wasanii, nyimbo zilizosikilizwa zaidi Spotify mwaka 2021

Wasanii, nyimbo zilizosikilizwa zaidi Spotify mwaka 2021

Zaidi ya wasanii 100 wa muziki kutoka Tanzania waliochia ngoma mpya mwaka huu wameingiza ngoma zao kwenye mtandao mkubwa zaidi duniani wa kusikiliza muziki wa Spotify.

Tukielekea kufunga mwaka, mtandao huo wenye makao makuu yake Stockholm, Sweden umetoa orodha inayoelezea wasanii 10 wa Tanzania waliosikilizwa zaidi nchini pamoja na ngoma zilizosikilizwa zaidi Bongo.


DIAMOND PLATNUMZ

Kwa mujibu wa Spotify Diamond Platnumz anashikilia nafasi ya juu katika orodha ya wasanii waliosikilizwa zaidi Tanzania. Akiwa na wastani ya kupata wasikilizaji 638,640 kwa mwezi. Kwa wastani huo, ni sawa na kusema kwamba mpaka kufikia Novemba mwaka huu, Watanzania zaidi ya 7 milioni wamemsikiliza Diamond kwa 2021.

Pia wimbo wake wa Iyo unashilikia nafasi ya kwanza katika orodha ya ngoma za Tanzania zilizosikilizwa zaidi Spotify kwa mwaka huu, huku nyimbo zake za mwaka jana, Jeje na Waah pia zikiwa kwenye orodha hiyo. Jeje ikishika nafasi ya 7, Waah nafasi ya 8.


HARMONIZE

Bosi na msanii wa Konde Gang, Rajabu Kahali maarufu Harmonize anashikilia nafasi ya pili akiwa na wastani wa wasikilizaji 426,257 kwa mwezi; ambayo ni sawa na kusema mpaka mwezi wa kumi na moja 2021, Harmonize amesikilizwa zaidi ya mara 4.6 milioni.


RAYVANNY

Akiwa na albamu moja aliyoiachia mwaka huu na singo zaidi ya tatu, mkali wa masauti kutoka Wasafi, Rayvanny anashikilia nafasi ya tatu akiwa na wastani wa wasikilizaji 411,098 kwa mwezi; ambayo ni sawa ni 4.5 milioni.

Na kushangaza zaidi, wimbo wake wa Number One aliouachia mwaka jana akimshirikisha Zuchu unashikilia namba 9 kwenye orodha ya ngoma zilizosikilizwa zaidi Tanzania mwaka huu.


NANDY

Kwenye orodha ya wasanii wa kike wa Tanzania waliosikilizwa zaidi mwaka huu kwenye mtandao wa Spotify Nandy anashikilia nambari moja, lakini ni wa nne kwenye orodha ya jumla akiwa na wastani wa wasikilizaji 194,365 kwa mwezi ambayo ni sawa na 2.1 milioni ndani ya miezi 11 ya mwaka 2021, yaani Januari mpaka Novemba.


ALIKIBA

King Alikiba anashikilia nafasi ya tano akiwa na wastani wa wasikilizaji 165,353 kwa mwezi; ambayo ukihesabu kuanzia Januari mpaka Novemba 2021, ni sawa na kusema Kiba amesikilizwa mara 1.8 milioni.

Aidha, ngoma yake ya Ndombolo kutoka katika albamu yake ya Only One King aliyoiachia mwaka huu imeingia kwenye orodha ya ngoma 10 za Tanzania zilizosikilizwa zaidi kwenye mtandao huo; inashika nafasi ya tano.


MBOSSO

Muhindi wa Kibiti, Mbwana Kilungi A.K.A Mbosso Khan anashikilia nafasi ya nne akiwa na wastani wa kusikilizwa mara 82,758 kwa mwezi. Ambayo ni sawa na 910,338 tu kwa miezi 11 ya mwaka 2021.

Pia ngoma yake ya Baikoki aliyomshirikisha Diamond inashikilia nafasi ya 4 kwenye ngoma za Bongo zilizosikilizwa zaidi.


ZUCHU

Zuhura anashikilia nafasi ya sita akiwa na wastani wa wasikilizaji 77,432 kwa mwezi, ambayo ni sawa na kusema kwa mwaka mzima wa 2021 (ukiacha mwezi Desemba) amepata wasikilizaji 851,752.

Aidha wimbo wake wa Sukari unashikilia namba 3 kwenye orodha ya ngoma za Tanzania zilizosikilizwa zaidi mwaka huu.


MARIOO

Namba nane inashikiriwa na Toto Bad, Marioo akiwa na wastani wa wasikilizaji 55,784 kwa mwezi, ambayo kwa miezi kumi na moja ya mwaka huu, ni sawa na kusema amekusanya jumla ya wasikilizaji 613,624.

Pia wimbo wake wa For You uliotoka mwezi Aprili mwaka huu unashikilia nafasi ya sita kwenye ngoma za wasanii wa Tanzania zilizosikilizwa zaidi 2021.


DARASSA

Darassa anakuwa msanii wa kwanza wa Hip Hop kuonekana kwenye Top 10 hii ya Spotfy mwaka huu, lakini kwa ujumla anashikilia namba 9 akiwa na wastani wa wasikilizaji 53,123 kwa mwezi; sawa na 584,353 kwa miezi 11 ya mwaka 2021.

Hata hivyo, wimbo wake wa Loyalty aliomshirikisha Nandy na Marioo ukitinga namba mbili katika orodha ya ngoma za wasanii wa Tanzania zilizosikilizwa zaidi Bongo.


JUX

King of Hearts anafunga orodha hii akiwa na wastani wa wasikilizaji 42,333 kwa mwezi ambayo ni sawa 465,663 kwa mwaka.


NYIMBO ZILIZOSIKILIZWA ZAIDI

Diamond Platnumz - IYO (feat. Focalistic, Mapara A Jazz, & Ntosh Gazi)

Darassa - Loyalty (feat. Marioo & Nandy)

Zuchu - Sukari

Mbosso - Baikoko

Alikiba - Ndombolo (feat. AbduKiba, K2ga & Tommy Flavour)

Marioo - For You

Diamond Platnumz - Jeje

Diamond Platnumz - Waah! (feat. Koffi Olomide)

Rayvanny - Number One (feat. Zuchu)

Marioo - Mama Amina