VIDEO: Alichokifanya Diamond kwa Tiffah baada ya familia kutinga Sauzi

Summary

  • Tiffah ambaye ni mtoto wa msanii maarufu nchini Tanzania, kesho Jumapili anasherekea siku ya kuzaliwa kwake nchini Afrika Kusini. Anafikisha miaka saba.

Dar es Salaam. Familia ya msanii maarufu wa muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul 'Diamond Platnmuz' imetua nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kusheherekea siku ya kuzaliwa ya mtoto wake Latifa Naseeb 'Tifaah.'

Tiffah ambaye ni mtoto wa kwanza na wa kike pekee wa msanii huyo anasherekea siku hiyo kesho Jumapili Agosti 7, 2022 akiwa anatimiza miaka saba.

Familia hiyo iliondoka jana Ijumaa jijini Dar es Salaam, ambapo ndipo inapoishi na tayari wameonekana wameshafika nchini humo ambapo Diamond alikuwa tayari katangulia huko.

Hata hivyo wakati ugeni huo mkubwa wa Tiffah ukiingia, mtoto huyo mwenye umri wa miaka saba leo Jumamosi Agosti 6, 2022 ameonekana akiwa na baba yake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond aliyekuwa amevalia kaptura nyeusi, beloni jeusi na sendozi nyeusi huku mtoto wake Tiffah akiwa amevalia tracksuit nyekundu na raba nyeupe wameonekana kwenye video wakiwa wanapanda ndege na amendika…”Nairobi in a second.”

Kati ya wanafamia waliokwenda ni pamoja na mama wa Diamond Platnumz, Snura, baba yake wa kufikia Uncle Shamte, Dada yake Esma Platnumz na watoto wake, dada yake Queen Darleen na mtoto wake  na watu wengine ambapo ugeni mzima huo umeonekana kuwa na zaidi ya watu 11.

Mpaka sasa Diamond ana watoto wanne akiwemo Tiffah, Nillan wote akiwa kazaa na Zari.

Wengine ni Daillan aliyezaa na mwanamitindo Hamisa Mobeto na Naseeb Junior aliyezaa na msanii Tanasha Dona ,raia wa Kenya.