Vanessa, Rotimi watarajia mtoto wa kiume

Tuesday September 07 2021
vanesa pic
By Nasra Abdallah

Staa Vanessa Mdee na mchumba wake, Rotimi kupitia mitandao ya kijamii wa Instagram wameposti ujumbe unaoshiria kuwa wanatarajia kupata kupata mtoto wa kiume hivi karibuni.

SOMA ZAIDI - Jux: Vanessa wa nini, sitaki shobo nishamblock

Hayo yamebainika leo Jumanne Septemba 7, 2021 kupitia kurasa zao ambapo kwa nyakati tofauti waliposti picha mbalimbali zikimwonyesha Vanessa kuwa mjamzito.

Mahusiano ya wawili waliyaweka wazi mwaka 2019 ikiwa ni miezi michache tangu alipoachana na aliyekuwa mpenzi wake wa muda mrefu, msanii wa Bongo fleva, Juma Jux.

vanesa pic 1

Wawili hawa waliamua kuyaweka wazi mahusiano yao mwaka 2019 na Desemba 2020,  Rotimi ambaye ni mwanamuziki  na muigizaji mwenye makazi yake nchini Marekani, alimvalisha pete mrembo huyo.

Advertisement

Licha ya nyakati tofauti kuwepo kwa tetesi za kuwa mjamzito, Vanessa alikanusha hilo na kuwalaumu waliokuwa wanasema hilo  kuwa wamesababisha mama yake kupaniki.

SOMA PIA: Vanessa avishwa pete ya uchumba

Rotimi ameandika "Zawadi kubwa imekuwa ni wewe, umebadilisha maisha yangu na sasa tumeungana  milele kumlea mtoto wetu,"

“Naomba mtoto wetu awe na moyo wako, akili, na imani yako, ninaahidi kukulinda wewe na mtoto  wetu kwa kila nilichonacho,” ameeleza

Kwa upande wake Vanessa ameandika "Zawadi kubwa kuliko, asante Yesu kwa kutuchagua, kutuheshimisha…tuna furaha sana,” ameandika Vanessa.

Advertisement