Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ujue wimbo wa kwanza 20 Percent kurekodi kwa Man Water

KWA asilimia kubwa muziki wake umejikita katika kuelimisha na ndicho kilichosababisha kupendwa na wengi, 20 Percent ni miongoni mwa waimbaji wenye tungo nzuri na nyimbo zake zimekuwa shule na dawa ya jamii kwa miaka sasa.Ametoa albamu na kushinda tuzo kupitia nyimbo zake maarufu kama ‘Tamaa Mbaya’ na ‘Ya Nini Malumbano’, ni miongoni mwa wasanii ambao nyimbo zao zilifanya vizuri kwa kiwango cha juu zaidi. Huyu ndiye 20 Percent;.


1. Alijua kuwa ana sauti nzuri ya muziki akiwa madrasa, alipomaliza shule ya msingi aliamua kujikita katika muziki licha ya kufaulu kujiunga na sekondari, kukataa shule na kukimbilia muziki kulifanya kufukuzwa nyumbani na baba yake mzazi.


2. Mwanzo alipoanza muziki alitumia jina la ‘Akili’ ikiwa ni ufupisho wa majina yake ya kuzaliwa ambayo ni ‘Abbas Kinzasa Lipakale’, lakini baadaye akalibadilisha na kuja na ‘20 Percent’ ambalo limempatia mafanikio makubwa.


3. Wakati anaaza muziki alikuwa anarap na wimbo wa kwanza kurekodi unaitawa ‘Hadhi Inashuka’ uliotengenezwa na Complex, wimbo wa pili kurekodi unaitwa ‘Kufa Kufaana’ uliotengenezwa na Roy, maprodyuza wa nyimbo zote ni marehemu kwa sasa.


4. Dickson Ponella ‘Dizzo’ ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Vipindi E FM Radio ndiye Mtangazaji wa kwanza kucheza nyimbo za 20 Percent redioni wakati huo alikuwa Magic FM, kisha akafuata D’jaro Arungu wa TBC FM ambaye alipewa nyimbo hizo na Dizzo.


5. Wimbo uliomtoa 20 Percent kimuziki ni Money Money (2005) na ndio ulibeba jina la albamu yake ya kwanza na nyimbo nyingi katika albamu hiyo amezirudiwa kurekodiwa (second version) baada ya kupata menejimenti mpya.Maprodyuza waliohusika kufanya remix ya ngoma hizo ni Enrico Figueiro, Bizman na Steve White na kazi nzima ilifanyika katika studio ya Sound Crafters.


6. Dully Sykes ndiye msanii wa kwanza mkubwa kwa 20 Percent kumshirikisha ambapo alisikika katika wimbo wake, ‘Tamaa Mbele’ kisha Bushoke katika wimbo, ‘Binti Kimanzi’ ambao ulikuwa remix. Wa kwanza alirekodi na J.I, na nyimbo zote hizo zilikuwa katika albamu ya Money Money.


7. Wimbo ‘Tamaa Mbele’ ndio ya kwanza kwa 20 Percent kurekodi na Man Water ambaye wakati huo bado alikuwa hajafungua studio yake ya Combination Sound. Na hadi sasa Man Water ndiye Prodyuza ambaye amerekodi nyimbo nyingi za 20 Percent na zikafanya vizuri.


8. 20 Percent alipata wazo la kucheza filamu yake, ‘Furaha Iko Wapi’ baada ya kupotea kwenye muziki, katika filamu hiyo aliamua kuweka nyimbo kama ‘Bangi Bangi’ na ‘Mama Neema’ ambazo zilimrejesha katika muziki.


9. Snura wakati huo akifanya kazi  ya upambaji (makeup artist) ndiye aliyempaka ‘makeup’ Shilole ili atokee kwenye video ya wimbo wa 20 Percent, Tamaa Mbaya. Na sasa Shilole na Snura ni wasanii wanaofanya vizuri kwenye Bongofleva, na wote awali walikuwa wakicheza filamu.


10. 20 Percent anashikilia rekodi kama msanii wa pili Bongo kushinda tuzo nyingi za muziki Tanzania (TMA) kwa usiku mmoja, mwaka 2011 alishinda tuzo tano ikiwa ni sawa na Alikiba kwa mwaka 2015  & 2021 na Zuchu 2022. Hadi sasa Diamond Platnumz ndiye kinara wa kubeba tuzo hizo kwa wakati mmoja ambapo mwaka 2014 alishinda tuzo saba.