Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ilkay Gundogan na Sara nje ya dakika 90

GUNDOGAN Pict

Muktasari:

  • Kilichovutia zaidi katika ushindi huo uliowahakikishia Man City kushiriki UEFA msimu ujao, ni jinsi Gundogan alivyofunga bao la kwanza kwa mtindo wa acrobatic ikiwa ni baada ya mkewe Sara Arfaoui kumtakia heri katika mechi hiyo.

MANCHESTER City ilicheza mechi ya mwisho ya Ligi Kuu England (EPL) 2024/25 katika dimba la Craven Cottage ambapo waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fulham FC aliyopachikwa wavuni na Ilkay Gundogan na Erling Haaland.

Kilichovutia zaidi katika ushindi huo uliowahakikishia Man City kushiriki UEFA msimu ujao, ni jinsi Gundogan alivyofunga bao la kwanza kwa mtindo wa acrobatic ikiwa ni baada ya mkewe Sara Arfaoui kumtakia heri katika mechi hiyo.

Muda mfupi kabla ya mechi hiyo kuanza, Sara aliposti Instagram picha yao waliyopiga katika uwanja wa Ethiad na kusema kila wakati anamuunga mkono  Gundogan hadi katika mchezo huo wa mwisho wa ligi.

Lakini nje ya dakika 90 maisha yao yapo vipi?, hawa walikuwa na uhusiano tangu mwanzoni mwa 2021 ila waliamua kuweka siri hadi Julai ambapo Sara kupitia Instagram aliitangazia dunia kuwa wao ni wapenzi na kufikia Agosti, naye Gundugan akafanya hivyo pia.

GUNDO 01

Mnamo Machi 2022, kiungo huyo wa kati wa Ujerumani aliyeichezea timu ya taifa michezo 82, alifichua kuwa amefunga ndoa na Sara huko nyumbani kwao Copenhagen ikiwa ni takribani miezi mitano baada ya kuchumbiana.

Kwa sasa tayari wana watoto wawili katika familia yao, wa kwanza ni wa kiume, Kais aliyezaliwa Machi 2023, na wa pili ni wa kike, Ella aliyezaliwa Februari mwaka huu.

Kabla ya kukutana na Gundogan, Sara alikuwa mtangazaji na mwanamitindo aliyefanikiwa sana katika kazi yake, huku pia akishiriki katika filamu kadhaa na alikuwa staa wa reality show katika televisheni. 

Hata hivyo, tangu aolewe na Gundogan kisha kuhamia Manchester, maisha ya Sara ilibidi yachukue mwelekeo mwingine ambao ni kuwa karibu na mumewe na kuitunza familia kitu kilichofanya kuipa kisogo kazi yake kwa muda. 

GUNDO 02

Akizungumza na Mail Sport mnamo Februari mwaka huu, Sara alisema ilikuwa ngumu kutoka kwenye kazi yake hadi kuwa mama wa familia kwa sababu licha ya kuwa mtangazaji, anazungumza lugha sita kitu kilichompatia safari nyingi kama mwanamitindo.

Sara alisema watu walimfahamu hapo awali kama staa wa vyombo vya habari lakini alipokuwa mke, kuna tabia ya waandishi wa habari kuonyesha wake za wachezaji kwa njia fulani kwamba maisha yao lazima yawe katika mtindo fulani.

"Nilipoteza kidogo hali yangu ya kujiamini, nilipoteza ule uwezo wa kuzungumza bila kufikiria. Kwa hiyo ndio ipo hivyo, kwa sehemu ni ngumu kidogo, kwa sababu lazima pia ujijenge upya na kupata utambulisho wako mwenyewe," alisema

GUNDO 03

Alisisitiza kuwa licha ya huko nje kuwepo mtazamo kuwa wake za wanasoka maarufu wanaishi maisha ya raha kila wakati, mambo hayapo hivyo kwa sababu nao wanahitaji kufanya shughuli zao na sio kuwa nyuma tu ya mafanikio ya wenzao wao.

"Siku zote watu huwa wanafikiri tuna kila kitu kwa sababu tuko na mtu huyu aliyefanikiwa. Lakini mtu aliyefanikiwa ana kazi yake mwenyewe, hivyo akifanikiwa, amefanikiwa yeye, haileti mafanikio kwako," alisema Sara na kuongeza.

"Kujitazama na kuhisi kama ninafanya kitu ni hisia nzuri zaidi kuliko kuwa na mtindo wa maisha kwa sababu ya mtu mwingine. Kufanya mambo peke yako na kufanikiwa ni muhimu zaidi. Ni muhimu kujivunia wewe mwenyewe na huwezi kujivunia wakati hufanyi kazi," alisema.

GUNDO 04

Alisema alipokuwa Manchester kabla ya Gundogan kuhamia Catalonia, Hispania ili kuichezea FC Barcelona na baada ya msimu mmoja kurejea tena katika jiji hilo, ilionekana kama maisha yake yote yalikuwa kwenye soka na sio kazi zilizompa umaarufu hapo awali.

"Kwa sababu marafiki zangu walikuwa watu wa soka, watu ambao nimekutana nao kupitia mume wangu, halafu sikuwa nafanya  kitu chochote ambacho kingeweza kunitambulisha katika ulimwengu wangu wa huko nje zaidi ya huu," alisema Sara.

Sara alisema anaikumbuka kazi yake ya uigizaji kwa sababu ilimpa nafasi ya kuonyesha kidogo jinsi nilivyo, sio tu yale ambayo watu walisoma kumuhusu, bali ilikuwa ni fursa ya kuonyesha utu wake hata kidogo.

GUNDO 05

Mrembo huyo ni mtangazaji wa televisheni ambaye amewahi kufanya kazi na kituo cha Rai Italia, na pia alikuwa mshiriki katika reality show ijulikanayo kama Les Princes et Les Princesses de l'Amour iliyoruka mwaka 2020.

Ukitazama ukurasa wake wa Instagram wenye wafuasi zaidi ya milioni 1 hujiulizi mara mbili iwapo ni mwanamitindo, Sara kila kitu kwake mtandaoni kinajieleza kwa jinsi anavyoutangaza mtindo wake wa maisha ya kuvutia.

Mnamo Januari 2022, mwanamitindo huyo alionekana kwenye Jarida la L'Officiel Arabia, na Juni 2023, mtangazaji wa BT Sport, Des Kelly alimuomba kupiga naye picha wakiwa mubashara kwenye televisheni.

Pia ameonekana katika video ya wimbo wa mwanamuziki kutokea Italia, Riki akimshirikisha CNCO, Dolor de cabeza (2018) ambayo hadi sasa imetazamwa zaidi ya mara milioni 32 katika mtandao wa YouTube ulioanzishwa Februari 14, 2005 huko Marekani.