Uchumba wa Mondi, Zuchu mapya yaibuka

Muktasari:
- Mondi na Zuchu walianza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na kuuweka wazi tangu mwaka 2021 na kuanzia hapo ikawa hakuna siri tena ni fulu kujiachia mara kuvaa nguo sare, mara kuonekana kwenye kumbi za starehe wakiwa pamoja, huku wakijiachia kimahaba.
HAYA ni mazito! Licha ya hivi karibuni Khadija Kopa, mama mzazi wa nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Zuchu na kuliambia Mwanaspoti kuwa yuko tayari kupokea barua ya posa ya staa Diamond Platnumz, kumeibuka mambo mpya kwa wawali hao.
Mondi na Zuchu walianza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na kuuweka wazi tangu mwaka 2021 na kuanzia hapo ikawa hakuna siri tena ni fulu kujiachia mara kuvaa nguo sare, mara kuonekana kwenye kumbi za starehe wakiwa pamoja, huku wakijiachia kimahaba.
Wawili hao mara kadhaa waluikuwa wakionyeshwa kupitia video kadhaa wakiwa nyumbani kwa Mondi au sehemu nyingine mbalimbali wakiwa pamoja kimahaba.
Hata hivyo, tangu mwaka huo uanze kumeibuka na changamoto za hapa na pale katuika penzi hilo, ikiwamo mara kadhaa watangaze kuachana kisha kurudiana, mwishowe hivi karibu Siku ya Valentiane, Mondi alimposti Zuchu katika akaunti yake ya instagram na kumuandika ujumbe wa kumwambia ajiamini kwani anampenda sana na toka awe na mahusiano na wanawake wengine hakuwahi kupenda mwanamke kama Zuchu hivyo asisikilize maneno ya watu wakasababisha waachane.

Pamoja na yote hayo, mapya yameibuka baada ya usiku wa kuamkia leo Feb 19, 2025, Mondi amejikuta akituhumiwa na baadhi ya kurasa za wanamitandao kwa kosa la kumsaliti Zuchu kwa bintimmoja ajulikanaye kwa jina la Rita kwa Video zilizosambaa mitandaoni.
Rita aliyewahi kuwa video Queen wa wimbo wa Diamond Platnumz uitwao, 'My Baby' uliotoka 2023, katika moja ya video zilizosambaa akijirekodi akijitambulisha yeye ni 'Mrs. Naseeb Abdul' na video zingine wakiwa faragha na Diamond.
Baada ya hayo, Mondi aliibuka na kuandika kwenye ukurasa wake wa insta story leo hii Alhamisi, kwa kujitetea video hizo ni za muda mrefu takriban miaka miwili imepita na huyo Rita kweli alikuwa naye lakini kwa sasa wameshachana tangu mwaka huo na atahakikisha kwenda mahakamani kushitaki kwa tukio hilo la usambazwaji wa hizo video.
Hata hivyo, wapo baadhi ya watu wakidai, inawezekana hilo lililoibuka likawa ni la kweli na kuna mtu amevijisha hizo video au ni sehemu ya drama ya kiki ama kuzima tukio la ndoa ya Hamisa Mobetto na Aziz Ki linalotrend kwasasa.
Mwanaspoti imepita katika akaunti za wawili hao na kubaini mambo yanazidi kuwa makubwa, hasa kwa Rita kuanika ukweli kwamba wameachana na Mondi, Novemba mwaka jana kisa ikiwa kodi, jambo linalozidi kuonyesha kuwa wawili hao wameamua kulipuana mtandaoni.

MSIKIE KHADIJA KOPA
Kabla ya kusambaa kwa video hiyo inayoonyesha kwamba Mondi na Rita walikuwa mtu na mtue, mama wa Zuchu ambaye ni Malkia wa Mipasho nchini, Khadija Kopa alifanya mahojiano na Mwanaspoti na kusema ishu ya uchumba wa MOndi na bintie na taarifa kwamba kuna posa ilipelekwa ili ndoa ifuate.
Ndio moja ya stori kubwa mwezi huu ni ndoa ya Diamond Platnumz na Zuchu huku wengi wakijiuliza kama itakuwepo au ni drama tu kama walivyozoea kwa wasanii hao wa Bongo Fleva.
Nyota hao ambao anafanya vyema kwenye muziki ndani na nje ya nchi, wamekuwa wakifuatiliwa sana na mashabiki na wadau wa muziki kutokana na ukaribu hao na mara kadhaa wamekuwa wakihusisha na ndoa na kudaiwa mambo yanaenda vizuri na jambo litatimia.
Hata hivyo, kilichokuwepo ni posa ya Diamond na ilianza kama utani wengi wakijua ni kiki tu na msanii huyo anataka kutoa wimbo katika 'Valentine Day' iliyofanyika Ijumaa ya wiki iliyopita.
Kukawepo kwa habari posa hiyo ilipelekwa lakini ikakataliwa ndiyo maana hakukuwa na chochote, lakini mama mzazi wa Zuchu, Khadija Kopa alifunguka ukweli wa jambo hilo kwa kusema habari hizo hazina ukweli wowote.
"Kwanza niwaambie watu mambo ya ndoa huwa mpangaji ni Mungu na kuhusu habari za wazazi tumekataa barua ya posa siyo za ukweli, sisi hatujaona barua yoyote kutoka kwa Diamond, zaidi ya kusikia tu huko mitandaoni," alinukuliwa Khadija Kopa na kuongeza;
"Halafu watu wanataka waelewe hili, furaha ya Zuchu ndiyo furaha yangu na familia yake, sasa sisi tukatae posa kwa ajili ya nini? Maana hadi mipango ya posa hiyo inapangwa ni lazima mwanamke husika ajue, sasa kama wamekubalina watoto, kwa nini wazazi wapinge?
"Tena sio tu barua ya posa kwa Diamond, sisi tunapokea barua ya mtu yeyote atakayehitaji kumposa Zuchu, kwa nini waseme Diamond tu? Kikubwa Zuhura (Zuchu) akikubali sisi hatuna pingamizi, ndoa ni heshima bana na ni jambo la kheri. Hivyo achana na wapiga midomo ya mitandaoni hao waongea tu."
Mwimbaji huyo nyota wa muziki wa taarabu amesema katika mambo anayopenda, ni kutoingilia mambo ya Zuchu pindi anapoandika vitu vya kuachana mitandaoni zaidi ya kumjenga kuwa na uvumilivu katika maisha.

"Naviona vitu anavyoandika Zuchu, sasa mie siwezi kumuingilia...mambo ya kitoto hayo, ila kama mzazi huwa nampa somo la uvumilivu katika maisha ndiyo nguzo kubwa kwake," amesema Khadija wa kundi la TOT Taarabu.
Zuchu na Diamond inadaiwa ni wapenzi wa muda mrefu mbali na kufanya kazi ya muziki pamoja katika lebo ya WCB, huku kila mara wakidaiwa kutibuana na kurudiana na juzi kati Siku ya Valentine, Mondi aliandika ujumbe mzito wa mahaba kwa mpenziwe huyo kuonyesha wapo sana pamoja, kabla ya kilichoibuka sasa. Ngoja tuone!