Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zuchu: Nyie jiandaeni tu kwa pati

ZUCHU Pict

Muktasari:

  • Zuchu na Dimamond walifunga ndoa ya kimya kimya wiki chache zilizopita na kushtua watu wengi, huku baadhi wakiamini ni kiki na wengine wakiwapongeza kabla ya wawili hao kuthibitisha ndoa hiyo.

NYOTA wa Bongo Fleva, Zuchu amesema watu wajiandae kwa pati la baada ya ndoa na siku hiyo watu watakula na kunywa, huku mama yake, Khadija Kopa akiwa akiwafunga midomo waliokuwa wakiwagombanisha na wakwe zao.

Zuchu na Dimamond walifunga ndoa ya kimya kimya wiki chache zilizopita na kushtua watu wengi, huku baadhi wakiamini ni kiki na wengine wakiwapongeza kabla ya wawili hao kuthibitisha ndoa hiyo.

Mwanaspoti lilikutana na Zuchu akiwa na mama yake maeneo ya Mwananyamala na kumpongeza Zuchu kwa kufunga ndoa na Diamond, lakini likitaka kujua kama kutakuwa na sherehe au ni ndoa pekee.

Hata hivyo, Zuchu aliliambia Mwanaspoti yeye na mumewe bado tu kufanya sherehe ili watu wale na wanywe, hivyo kuwataka watu wajiandae.

“Unajua mimi na mume wangu Diamond tulikuwa hatujaamua kuweka wazi tu ndoa yetu au kufanya sherehe kwa sababu tumekaa pamoja muda mrefu sana, yaani kisheria ni mke na mume, ila kuhusu sherehe baada ya kufunga ndoa, siwezi kusema ni lini, lakini watu wasubiri sherehe ipo na watapewa taarifa,” alisema Zuchu, huku Khadija Kopa akiongeza kwa kuwataka watu waache kumzulia mwanae kwa kudai haelewani na Mama Diamond ikiwa hawana uhakika.

"Sasa wamuache mwanangu atulie katika ndoa yake, maana wamemsema sana, mara king'ang'a, mara hapendwi na mkwe wake, sasa hapendwi wao waliona wapi huyo mkwe wake ametamka hayo maneno? Wasitake kuwagombanisha maana wameshindwa katika ndoa wamezua ya kutopendwa ukweni," alisema Khadija Kopa ambaye ni nyota wa muziki wa taarabu nchini.