Drama za Aziz KI, Hamisa zinaendelea

Muktasari:
- Wikiendi iliyopita akiwa kwenye ndege, Hamisa aliandika ujumbe kuwa anarudi Tanzania, ndipo Aziz KI akakomenti kwa kuandika 'arudi kwake haraka kwani ameshammisi', ndipo Hamisa akamjibu akomae na mpira kwanza, mapenzi baadae.
Ni swali ambalo mashabiki wa wawili hao wanajiuliza, kwani ni ikiwa ni siku moja tu baada ya Hamisa Mobetto kukwea pipa na kurudi Tanzania akitokea kwa mumewe, Stephane Aziz KI, nyota huyo wa zamani wa Yanga anayekipiga Wydad Casablanca ameonyesha kummisi mkewe huyo.
Wikiendi iliyopita akiwa kwenye ndege, Hamisa aliandika ujumbe kuwa anarudi Tanzania, ndipo Aziz KI akakomenti kwa kuandika 'arudi kwake haraka kwani ameshammisi', ndipo Hamisa akamjibu akomae na mpira kwanza, mapenzi baadae.
Kauli hiyo ya Hamisa imezua maswali mengi, huku watu wakijiuliza kama ni siku moja tu Aziz KI kuwa mbali na mke wake, je ataweza kuitumikia Wydad kwa ufanisi kwa namna walivyokuwa wakigandana kabla na baada ya kuoana mapema mwaka huu.
Hata hivyo, Mwanaspoti lilimsaka Hamisa na kuzungumza naye na alifafanua juu ya jibu lake hilo kwa Aziz KI, lilivyoleta maswali kwa mashabiki zao na alisema haya:
"Jamani mimi nimejibu kama jibu la kawaida tu kwa mtu na mkewe kukumbushana vitu muhimu, hivyo yule ni mume wangu na wajibu wangu kumwambia 'afocus' katika kazi kwani mapenzi yapo na mimi nipo tu, ndiyo maana nilienda na nimerudi, nimempa nafasi ya kujiandaa na mechi zinazofuata, sema nae anapenda muda wote niwe nawe karibu (kicheko), " alisema Hamisa.
Hamisa amerudi Dar es Salaam kuendelea na majukumu yake kama kawaida huku akidai muda mwingi atautumia kuweka sawa mambo yake ya biashara na kazi za kampuni hata kama akiondoka tena atakuwa anapumzika bila wasiwasi wa kuwaza kazi za watu.
Wawili hao walioana Februari mwaka huu katika ndoa iliyokuwa gumzo kwa mashabiki wa soka na hasa mtandaoni kabla ya hivi karibuni Aziz KI kupata dili la usajiliwa na Wydad inayoshiriki Fainali za Kombe la Dunia la Klabu zinazofanyika Marekani na akiwa na timu hiyo na Hamisa alikuwa naye bega kwa bega tangu alipoenda kusaini mkataba Morocco.