Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sweet Fella: Ruksa Mkubwa Fella kuchangiwa kwa atakayeguswa

MKEWE Pict

Muktasari:

  • Sweet amesema, anajua kuugua kwa mumewe, ni ibada na kwamba yupo pamoja naye bega kwa bega hadi dakika za mwisho, ila kwa yeyote atakayeguswa familia iko tayari kupokea chochote.

MKE wa Saidi Fella, Sweet Fella, amewaomba Watanzania walioguswa na kuumwa kwa mumewe, Mkubwa Fella, ruksa kujitokeza kumsaidia ili aweze kurejeshwa India kwa mara ya pili kwa ajili ya matibabu zaidi, kwani hali yake bado haiko sawa kabisa.

Akizungumza na Mwanaspoti, Sweet amesema, amepata malalamiko mengi kuwa familia hawataki watu watoe msaada wala kwenda kumuona, kitu ambacho taarifa hii haiko sawa kabisa.

Sweet amesema, anajua kuugua kwa mumewe, ni ibada na kwamba yupo pamoja naye bega kwa bega hadi dakika za mwisho, ila kwa yeyote atakayeguswa familia iko tayari kupokea chochote.

FEL 01

"Hakuna kitu kibaya, mtu unauguza halafu yanazuka maneno maneno mengi ambayo yanakuwa ya uongo, binafsi pamoja na familia hakuna mtu aliyekataza Mkubwa Fella asisaidiwe na Watanzania, yuko ndani  huu ni mwaka mmoja sasa toka arudi India kwa matibabu, anaendelea na matibabu ya hapa na pale ana kliniki anaenda kwa wiki mara 2, anafanya mazoezi kila siku asubuhi ambapo kwa mwezi ni Sh 1.2 milioni."

"Kuna dawa anaendelea nazo kutumia ili aweze kukaa sawa, lakini mbali na hayo anatakiwa kurudi India kwa mara ya pili kwa ajili ya kuendelea na matibabu, hivyo hatuwezi kataza msaada kwa watu walioguswa na huku kuumwa kwake, hivyo ni ruksa kwa walioguswa na hali hiyo na wanaotamani kusaidia gharama za matibabu na safari ya India. Mchango wowote unaweza kutumwa kupitia namba 0713781414 ambayo ni namba ya kwake Mkubwa Fella," amesema Sweet.

FEL 02

Taarifa za kuumwa kwa Mkubwa Fella' ziliibuka kwenye mitandao ya kijamii Januari 2025 kuwa amepoza miguu huku wengi wakidai Diamond amemtelekeza.

Hata hivyo, baada ya kupata taarifa hizo Mwananchi ilimtafuata nyumbani kwake Mbagala Kata ya Kilungule, jijini Dar es Salaam na kuzungumza na baadhi ya ndugu zake waliodai hali yake haikuwa nzuri hata kuzungumza na mtu kwa muda mrefu alikuwa anashindwa.

Machi,4, 2025 Mwananchi iliripoti hali ya kiafya ya Mkubwa Fella aliyekuwa akisumbuliwa na presha na kupooza miguu. Hata hivyo, Fella alisema afya yake imezidi kuimarika baada ya kutoka India kupata matibabu, ambapo huko India gharama zote aligharamia Diamond Platnumz.

FEL 04

Ilipofika Mei, 2025 Fella alisema kutokana na hali yake kuwa mbaya kwa matatizo hayo. Alikata tamaa ya kupona, lakini kwa wakati huo anamshukuru Mwenyezi Mungu kwani anaendelea vizuri.

."Nina furaha kwani kwa sasa naendelea vizuri, hali yangu inaimarika kila siku na nimeanza kufanya mazoezi ya kutembea kila ifikapo jioni.

"Ukweli nimeumwa sana yaani nina furaha kwani kwa sasa naendelea vizuri, hali yangu inaimarika kila siku na nimeanza kufanya mazoezi ya kutembea kila ifikapo jioni.

FEL 05

"Yaani nimeumwa hadi nikawa nimekata tamaa ya kupona, ila namshukuru Mungu sana hadi sasa naweza kuongea na wewe hivi na kutembea vizuri kwa kufanya mzoezi, ilikuwa balaa," amesema Mkubwa Fella.

Januari 6, 2026 Sweet Fella, aliandika kwa akaunti yake ya Instagram kuwa, anapamba mwenyewe kumuuguza Mkubwa Fella, ila haoni watu wake wa karibu hata kumjulia hali kama ilivyokuwa zamani alikuwa akipigiwa simu za kila wakati usiku wa manane kumuamsha Fella aende kuwasaidia kazi zao hao watu wa karibu.

Katika hao aliwataja watu ambao wapo kipaumbele kutoa sapoti ni Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Mbosso, Meneja Said Kessy na Muddy K  rafiki wa karibu wa Mkubwa Fella.