Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkubwa Fella afunguka bifu la wasanii

FELLA Pict

Muktasari:

  • Fella ambaye kwa sasa hali yake kiafya anaendelea vizuri huku akizidi kufanya mazoezi ya hapa na pale, ameliambia Mwanaspoti kuwa mashabiki wanapenda kuingilia kati vitu wasivyovijua kiundani, jambo ambalo sio zuri na linaivuruga sanaa.

MENEJA wa Diamond Platnumz, Mkubwa Fella, amewataka mashabiki kuacha kama yalivyo masuala ya bifu za wasanii kwani hakuna anayejua mwanzo wa kazi zao wala chimbuko la bifu hizo.

Fella ambaye kwa sasa hali yake kiafya anaendelea vizuri huku akizidi kufanya mazoezi ya hapa na pale, ameliambia Mwanaspoti kuwa mashabiki wanapenda kuingilia kati vitu wasivyovijua kiundani, jambo ambalo sio zuri na linaivuruga sanaa.

FEL 01

“Ukweli ni kwamba hawapaswi kungumzia bifu za wasanii, hii inakuwa kama wanachochea wasanii kuwa na bifu milele au kushindwa kufanya kazi zao kwa ufasaha, kwa hiyo hupaswi wewe kama shabiki kuingilia vitu ambavyo huvijui, na niwaambie tu wakati mwingine hawa wasanii huwa wenyewe wanafahamiana vizuri pindi wanapokuwa na mgongano ama huwa wanajua nini wanataka kukifanya kwa wakati huo, kwa hiyo wewe shabiki unaingia kati unaanza kumtetea msanii huyu na kumtukana yule wakati hamfahamu chanzo.”

FEL 02

Mkubwa Fella, amezungumza haya baada ya Mwanaspoti kumuuliza anachofahamu kuhusu mvutano uliotokea katika mitandao ya kijamii kati ya wasanii Diamond Platnumz na Mbosso hadi kurushiana maneno kwenye mitandao ya kijamii zaidi ya mwezi mmoja uliopita. Wimbo unaotamba 'Pawa' wa Mbosso, ulionekana kuwa kitovu cha malumbano yaliyohusisha mashabiki wa pande zote mbili.