Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sio PSG tu, hata Rima anaitaka Ballon d’Or ya Dembele

DEMBELE Pict

Muktasari:

  • Hata hivyo, kiu haipo kwa PSG pekee, bali hata kwa Rima Edbouche, mke na mama mtoto wa Dembele ambaye amekuwa na kiwango bora msimu uliomalizika akichangia mabao 48 katika michezo 54 na kuisaidia klabu yake kunyakua mataji manne.

BAADA ya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza, sasa kiu ya mashabiki wa Paris Saint-Germain (PSG) ni kuona mchezaji wao, Ousmane Dembele anashinda tuzo ya mchezaji bora duniani ya Ballon d’Or.

Hata hivyo, kiu haipo kwa PSG pekee, bali hata kwa Rima Edbouche, mke na mama mtoto wa Dembele ambaye amekuwa na kiwango bora msimu uliomalizika akichangia mabao 48 katika michezo 54 na kuisaidia klabu yake kunyakua mataji manne.

Licha ya kukabiliwa na upinzani kutoka kwa Lamine Yamal, Raphinha na Mo Salah, bado Dembele anapewa nafasi kubwa zaidi ya kushinda Ballon d’Or hasa baada ya kutwaa Ligi ya Mabingwa Ulaya wakiiadhibu vikali Inter Milan kwa kipigo cha mabao 5-0.

Lakini, Rima Edbouche aliyetajwa hapo awali ni nani hasa na ana mchango gani katika maisha ya Dembele? Kaa mkao wa kula uletewe za ndani kutoka katika familia hii isiyokuwa na mambo mengi.

Kulingana na vyanzo vya ndani, Rima anatokea jamii ya Waberber na alizaliwa 1999 huko Douar Aghbalou, Kusini-magharibi mwa Morocco, lakini vyanzo vingine vinadai bibie alizaliwa huko Castelfranco Veneto, Kaskazini-mashariki mwa Italia.

DEMBE 04

Baba yake Rima anajulikana kama Brahim Edbouche na mama Fatima Bouzidane ingawa hakuna taarifa nyingi kuwahusu pamoja na ndugu zake wengine.

Chanzo cha awali kinaeleza kuwa familia yake iliamua kuondoka Morocco na kwenda Ufaransa ambapo aliishi maisha yake yote ya utotoni na kusoma huko hadi chuo kikuu kisha kuingia katika ulimwengu wa mitindo.

Rima alikutana na Dembele nchini Ufaransa wakati alipokuwa na klabu yake ya utotoni, Rennes kati ya 2010 na 2016, kabla ya kuhamia Borussia Dortmund ya Ujerumani alikocheza hadi 2017, kisha kujiunga na FC Barcelona ya huko Hispania.

Tangu walipokutana waliweka uhusiano wao kuwa wa faragha zaidi kiasi kwamba habari za Dembele kufunga pingu za maisha mnamo 2021, wakati huo akiichezea Barcelona, zilileta mshtuko katika ulimwengu wa soka.

DEMBE 01

Wawili hao tayari wana binti mmoja ambaye jina lake halijafahamika hadi sasa kutokana na wao wenyewe kufanya siri, na mtoto huyo aliripotiwa kuzaliwa Septemba 16, 2022, katika moja ya hospitali huko Catalonia, Hispania.

Harusi yao ilikuwa ya kitamaduni zaidi, sio tu muziki ulikuwa wa Morocco, lakini video na picha zilionyesha bibi harusi akiwa amevalia vazi la jadi kutoka nchini humo lijulikanalo kama caftan huku bwana harusi naye akivaa kitamaduni.

DEMBE 02

Kitu kingine kilichovutia katika harusi hiyo ni bibi harusi kubebwa kwenye mabega ya wanaume waliovaa mavazi meupe huku akiwa ameketi katika kiti cha mbao kilichopambwa kwa rangi za kuvutia.

Kadri video za harusi hiyo zilivyozidi kusambaa ndivyo watumiaji wengi wa mitandao wa kijamii huko Morocco walizidi kumpongeza Dembele mwenye asili ya Mauritania kwa kufanya harusi kitamaduni nchini humo.

Harusi hiyo ilifanyika Desemba 24, 2021 ambapo marafiki wachache wa Dembele akiwemo Dayot Upamecano wa Bayern Munich na wachezaji wenzake wa zamani wa Barcelona ​​walihudhuria hafla hiyo.

Dembele amezungumza mara kwa mara kuhusu umuhimu wa familia na wengi wamegundua kuwa matokeo chanya ya ndoa yake na Rima yamekuwa na msukumo mkubwa kwa mchezaji huyo kuendelea kufanya vizuri uwanjani.

DEMBE 03

Kwa hakika Rima ni ngome isiyoyumba, uwepo wake katika maisha ya Dembele umekuwa chachu ya utulivu na usaidizi wa kutumia kipaji chake kung’ara uwanjani kama alivyofanya msimu uliomalizika ambapo alifunga mabao 35 na kutoa asisti 13.

Rima kuna kipindi alikuwa mmoja wa wanawake wa Kiislamu wenye ushawishi mkubwa kwenye mtandao wa TikTok, akikusanya wafuasi zaidi ya 300,000 na kupata likes milioni 3.3 kwenye akaunti yake ambayo sasa haipatikani tena. Kwa sasa anatumia Instagram kwa kiasi chake akiwa na wafuasi zaidi ya 161,000. Anatumia jukwaa hilo kutangaza chapa yake, Razalae ambayo inajishughulisha na mitindo ya Kiislamu ambayo imemfanya kutambulika na wengi.

Hata hivyo, Rima maisha yake ya mtandaoni ni tofauti kabisa na wenza wa wachezaji maaarufu duniani, mathalan ukurasa wake wa Instagram hauna picha zake wala za familia yake zaidi ya kazi zake za mitindo. Chapisho ambalo linahusu maisha yake binafsi ni moja tu ambalo aliliweka hivi karibuni baada PSG kutwaa kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambapo  alihudhuria mchezo huo pamoja na mtoto wao na walifanikiwa kulishika kombe.

Baadhi ya picha alizoposti Rima zinamuonyesha akiwa dimba la Allianz Arena ilipopigwa fainali hiyo, huku nyingine zikionyesha wachezaji wakisheherekea kisha akaandika ‘wikiendi ya mabingwa’. Bila shaka atafanya hivyo tena pindi Dembele akishinda Ballon d’Or 2025 au wakati ujao.